Siku zote Jeshi lolote lile lenye nguvu duniani,huwa na nguvu muda wa Amani tu,amani ikivurugika hakun commandoo yeyote atakaejisifu kuwa yeye ni commando mwenye mafunzo ya hali ya juu, bali na ukomando wake anaweza akakimbia uwanja wa vita.
Hakuna polisi yeyote duniani waliowahi kushindana na nguvu ya umma na wakashinda, labda ndotoni tu.
KUna uwezekano mkubwa wa zaidi ya asilimia tisini kuwa watu wasiandamane,lakini haitokuwa ushindi kwa wa watawala, bali itakuwa ndio mwanzo wa ushindi kwa wananchi,kwani taratibu roho za watu zinazidi kubadilika,kutoka kuwa raia wa pole hadi raia ambao hawatamani kabisa kuiona serikali iliyopo madarakani.
Muda wa serikali kurudi upande wa Wananchi, la sivyo,siku zao,miezi yao na miaka ya kumaliza utawala ipo karibu mno kutimia
Wasipojirekebisha,watabaki kuwa historia ya moja ya chama kilichotawala kwa miaka mingi Afrika lakini kikadondoshwa na wananchi kwa Aibu kubwa.
Mitano Tena.