Hofu inayowatesa vijana

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
151
250
HOFU
Hofu ya kujaribu katika maisha ndio kitu kikubwa kinachowatesa vijana wengi..
Vijana huogopa kujaribu kuyakabili maisha lakini wana mipango mikubwa ya kufanikiwa..
Hofu ikishatawala ubongo wako inaharibu uwezo wa kufikiria njia za kufanikisha jambo katika maisha yako.
Endapo una hela na unahofia kujaribu kuifanyia biashara fulani kwa hofu ya kwamba hela itaisha na unaeza ukapata hasara, hapo uwezo wako wa kufanikiwa ni mdogo sana...
Usihofie maneno ya watu kwa kusema unafanya nini, ww jaribu kufanya kwanza ushindwe maana wanasema. "Bora kujaribu na ushindwe kuliko ushindwe kabisa kujaribu" hii itakuumiza maishani mwako endapo utahofia kujaribu halaf mwenzako akajaribu na akapata.
Hebu fikiria ingekuwa vipi mtu kama WARREN BUFFET tajiri namba 3 duniani angekuwa na hofu ya kujaribu kwenda ofisini kwa muuzaji hisa mkubwa duniani kipindi hicho BENJAMINI GRAHAM ili amfundishe kuwa kama yeye? Je, BUFFET angekuwa tajiri namba tatu duniani?
Lakini WARREN hakuwa na hofu ya kujaribu aliamini atafanikiwa tu endapo angekutana na BENJAMINI BGRAHAM, akasafiri umbali mrefu mpaka alipo GRAHAM na kwenda kumgongea ofisini kwake japokuwa hakufanikiwa kumkuta GRAHAM lakini alikutana na mtu ambae alikua karibu na GRAHAM na mtu huyo alimuona BUFFET ana nia hana hofu ya kujaribu akamsaidia BUFFET na hatimae BUFFET akafanikiwa kupitia yule msaidizi wa GRAHAM.. Sasa hivi BUFFET ni tajiri duniani..jifunze kupitia Buffet alivojaribu na akafanikiwa na ww sasa ni zamu yako amini unaweza kufanikiwa amini unachokiwekeza kwa sasa kina mafanikio makubwa mbeleni.

Chukua uamuzi sasa mwaka huu mpya 2017 usihofu kujaribu kuyakabili maisha
Usihofu kuhusu hasara yakabili maisha
Usihofu kuhusu marafiki watasemaje yakabili maisha
Usihofu hata wakikusema vibaya wakati huo ukiwa unajaribu watarudi kukusema kwa mazuri ukiwa umefanikiwa ..

share kwa unaowapenda

By Jay Speed
 

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
151
250
Neno zur xana. Japo vijana weng hawapend threads kama hizi ndio maana hata coments unaona ni chache
Na sasa ndio muda sa hihi wa kuwashawishi wasome Vijana ambao hawasomi hivi kwasasa wapo kwao hawafikirii bado wataondoka lini lakini naamini sku akitaka kutoka atatafita mtu wa kumuelewesha hapo ndo unapoona wanaanza kufatilia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom