Why Good Girls remain Single?

Marcovicsavic

Senior Member
Nov 14, 2020
130
298
Mara ya kwanza Nilipokiona kitabu hiki na kusoma Tittle yake, nilianza kutegeneza mawazo yangu kichwani na ku JUDGE A BOOK BY ITS COVER.

Jamaa mmoja alituma PDF ya kitabu hiki kwenye group la WhatsApp.
Jambo la kwanza nililofikiria ni kwamba ingekuwa tu yaleyale ya kuelekeza wanawake wanapaswa kufanya nini na wasifanye nini katika maisha yao ili waje kua wake bora SIO VITU VYANGU!.

Ni nani alisema kila mtu anataka kuolewa?
Kwa nini tunahitaji kuwa na njia fulani ili kufikia malengo haya? Je! Ndoa ndio kitu pekee ambacho wanawake wanatafuta Duniani?

Kama mtu ni mtu mzuri kwa asili, hupaswi kuanza kubadilisha tabia zako ili waweze kuingia kwenye mahusiano au ndoa, kama utabadirika na mahusiano yasipo enda vyema nani wa kulaumu? ,nanje utarudi kwenye tabia zako za zamani?.

Haya ndiyo mambo ya kwanza yaliyonijia kichwani na nilijiuliza kwa nini nisome kitabu cha kike kama hicho.
Nikatemana nacho!.

Nisieleweke vibaya, siwezi kusema ndoa ni jambo baya.
inaweza kuwa jambo zuri zaidi kutokea kwa watu wawili.

Mimi ni mpenda hadithi za mapenzi na naamini kila mtu anahitaji kupenda na kupendwa na pia anahitaji HAPPY ENDING. Lakini sipingi watu ambao wanasubiri kwa hamu kupata upendo wakiwa singo,
Licha ya kua wanaweza kuwa wapweke maishani mwao, na haitakiwi kuwa hivyo.

kwa kusoma kichwa tu, nilianza kujitetea mwenyewe na hinsia zangu, na sasa najuta ,najuta mnoo.

Baadaye, mtu mwingine katika grupu hilo hilo alirudi kumshukuru aliyekuwa ametuma PDF ile. Nikaamua kujaribu kuisoma kwa kweli sio kwa ile minyama aliyo kipakulia, alafu wa kiume sasa!

Kitabu hiki kina msingi wa nadharia kwamba wasichana wabaya huolewa kila Jumamosi wakati wasichana wazuri wengi wanabaki wakiwa hawajaolewa.
Anaposema wabaya sio sura na muonekano bali ni mitazamo tabia na hofu ya Mungu,

Nilitarajia kuwa kitazungumzia jinsi wanawake wanavyohitaji kubadilika ili waweze kukutana na wenza wao. Lakini sivyo ilivyo ile ya kweli sio fake!.

mwandishi, Nelson Asuen, anatoa onyo kwamba kuwa mtu mzuri au mbaya sio tiketi ya kudumu katika uhusiano kwa muda mrefu na kufika ndoa ama kua na ndoa yanye amani na mafanikio.

Pia anasema katika aya ya kwanza ya kitabu kuwa kitabu chake kime toa hasa maoni aliyokusanya na kuyachambua kwa kina kutoka kwa watu wengi sana.

Nilikipenda zaidi kwa sababu Nelson anashauri wanawake kuishi maisha yao na kutofeki.

Anahamasisha wanawake kujifunza jinsi wanaume wanavyofikiria kwa kwenda nao sawa na kutumia muda pamoja nao.

Anasema kuwa mume bora hapatikani tu kanisani au katika kwaya za kanisa au vikao vya jumuia na vijana wa kanisa.

Wanaweza kupatikana pia kwenye
klabu, mikutano ya vijana, na Birthday patry casino etc..

"Wanaume wengi wanavutiwa na wanawake ambao wanajua wanafanya nini, hii iko wazi, kua na mahusiano na binti anae jua anatakiwa kufanya nini wakati gani na kwanini ni rahisi na raha zaidi ya kua na binti asie jua nini anatakiwa kufanya, vijana wana waita WASABATO,

Mwanamke anayejua anafanya wazungu wanaita ‘runs girl’. Mwanamke hawa huchukua muda kuelewa saikolojia ya wanaume na njia za kuwapendeza na huzifata, na kazi ya kukamata moyo wa mwanaume kwao hua rahisi sana kwasababu wanajua nini wanafanya!

Hii ndio saabu maadui wa samsoni hawakwenda Kanisani kutafuta binti na mtii, akamrubuni samsoni bali walienda kwa Kahaba! Yes kahaba anajua aguse wapi aseme nini kwa wakati gani.

Sisemi wanawake wazuri wanapaswa kuwa 'runs girls'. Ninachosema ni kuwa wanapaswa kuwa na mtazamo wao kujifunza jinsi wanaume wanavyofikiria, kuelewa saikolojia zao na kutimiza mahitaji yao."

Ipo wazi kuwa lazima tujifunze jinsi ya kuishi na watu wa jinsia tofauti, nao wanapaswa kujifunza jinsi ya kuishi na sisi. Mwisho wa siku, huu ndiyo msingi wa mahusiano. Kujua jinsi ya kuishi na wengine.

Kitabu kinajadili mtazamo ambao watu wengi wanao,
kwamba ikiwa wanafanya kila kitu sawa, watakutana na Mr Right watapata ndoa nzuri moja kwa moja.

Haipo hivyo!

na inaweza kuharibu.
Hivyo ndio kitabu kinapinga
Wazo kwamba watu wema daima watakuwa na vitu vizuri na kufanikiwa .
,
Ikiwa unachagua kuwa na mawazo chanya unaposoma kitabu hiki, basi kinaweza kuwa cha kuelimisha sana. Hicho ndicho nimekipendea .

Toa mawazo na maoni binafsi kichwani mwako na fikiri kwa kina juu ya ujumbe ambao Nelson anajaribu kufikisha, na utaona kuwa ana hoja.

Itoshe kusema kuwa kitabu hiki kipo kwa ajiri ya wanawake ambao kwa kweli wanataka kuolewa lakini pia si kitu kibaya kuchagua njia nyingine yoyote tofauti na hiyo katika maisha.

JamiiForums-191882621.jpg
 
Hususani weupe au wenye matako makubwa huwa wanadhani kwamba wao ndiyo kila kitu katika hii dunia.

Wakifikisha 30+ Wanaishia kuwa bar maids. Wakifikisha 40+ wanageuka wauza mahindi ya kuchoma kando ya barabara. Walifikia 50+ wanakuwa wamepigika to the fucking extent, wanageuka mashemasi na wafanya usafi kwenye haya makanisa ya manabii wa uongo
 
Back
Top Bottom