Hizi text za kidini za kufowardiana...!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,523
Salam wakuu,
Za mchana! Kuna huu mtindo umeenea siku hizi wa kufowardiana hizi sms za kidini sijui tuma kwa watu 10 ndani ya dakika kadhaa utapata muujiza na ukipuuzia utalaaniwa. Hizi sms zinanikera sana kwa kweli, halafu hazizingatii swala la salio lako au vp ilimradi tu nilazima kuwaforwardia na wewe wenzako. Mimi hua nazidelete sababu kwanza hazijatoka kwa Sir God mwenyewe, halafu sijawahi kusikia baraka za lazima. Halafu na vile vitisho vyake kwamba sijui uisipotuma utakua na miaka 7 ya shida na tabu. Wai? Kiruuu!
 
Mwishoni huishia na mkwara mbuzi ETI.....Bw. Bujibuji wa JF CC alidharau kutuma ujumbe huu matokeo yake kesho yake akafukuzwa kazi........ Bw. Baba V wa mwisho wa lami Lumo alituma ujumbe huu kwa watu 10 baada ya siku mbili akashinda bahati nasibu ya mamilioni na kupandishwa cheo ofisini kwake .....tuma ujumbe kwa watu wengi kadiri uwezavyo
 

Hahahah af ni kweli mkuu zina biti moja la hatari!
 
mi sizipendi kabisaaaaaa.......msg zozote za kuforwadiana sizipendi
Umeonae wanaoforwad nao wanachosha acha tu maana no editting,zingine wanatuma asubuhi anasema nakutakia usiku mwema,keroooooo waache mara moja kwakweli
 
mi sizipendi kabisaaaaaa.......msg zozote za kuforwadiana sizipendi
Hata mimi huwa sipendi kufowadiwa sms kwani naona muhusika kama hakua na nia ya kunijulia hali au kuwasiliana na mimi. Hizo sms za vitisho hazitokani na Mungu ni kudelete tu. Wengine hadi email unakuta kakufowadia huwa najiuliza kwanini usikae kimya tu kama huna muda wa kuandika mawazo yako . Email type hiii huwa sijibu kabisa.
 

Mimi huwa simalizii hata kuzisoma..
 

Mimi huwa simalizii hata kuzisoma..
 

hahahha nimecheka sana eti Baba V alituma akafanikiwa...tuma kwa watu wengi kadri uwezavyo

U MADE MY MORNING
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…