Hizi tetesi ni kweli kuhusu Nyerere?

Hizi tetesi ni kweli kuhusu Nyerere?

Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2,304
Reaction score
780
Zamani tunasadikishwa kuwa yule Mzee wetu JK wa kwanza (Mungu amlaze pema peponi) ,alikuwa ni mtaalamu sana wa hizi kamati za ufundi wa mambo ya asili ya mwafrika (uchawi).....

Zipo hadithi mbali mbali tulizokuwa tunasimuliwa kuhusu yeye kwamba:- alikuwa na saa/rada (vyovyote iwavyo) kila alipokuwa anataka kusafiri anakwenda kuiangalia, akikuta ina rangi nyeupe basi ilimaanisha kuwa safari yake ni nzuri....na kama cku hiyo akiikuta ina rangi nyekundu au nyeusi basi hasafiri maana safari hiyo itakuwa na mkosi....

Kuna uzushi mwingine kuwa eti hata kile kifimbo chake kilikuwa ni maalumu kwa ajili yake tu na wasimuliaji wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ipo walikuwa mkutanoni huko Arusha na baada ya mkutano kumalizika akakisahau mezani kile kifimbo watu wakajaribu kukiiba lakin kikagoma kung'oka pale mezani!!

Na watu wakazidi kudai kwamba eti hata kushinda kwa ile vita ya kagera kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na zile kamati zake za ufundi........kuna hayo na madai mengine mengi tu sasa mi binafsi cjafahamu lolote ktk hayo kuna anaejua zaidi?
 
Huo wote ni uzushi tu. Mwalimu hakuwa na tabia za aina hiyo. Mwalimu alikuwa Mkristo Mkatoliki safi. Anaweza kuwa na upungufu wake, lakini kiimani alikuwa timamu kweli kweli. Lakini pia aliheshimu sana mila za asili.

Nakumbuka alishiriki maadhimisho ya mila za Kizanaki kama Wazanaki wengine. Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa pamoja na dini za kimapokeo, bado Waafrika wana mila nzuri zinazopaswa kuenziwa. Huyo ndiye Mwalimu.
 
Changanya akili ya kuambiwa na kile unachokijua kisha ufahamishe ufahamu wako ufahamu kile ulichokifahamu leo.
 
Huo wote ni uzushi tu. Mwalimu hakuwa na tabia za aina hiyo. Mwalimu alikuwa Mkristo Mkatoliki safi. Anaweza kuwa na upungufu wake, lakini kiimani alikuwa timamu kweli kweli. Lakini pia aliheshimu sana mila za asili.

Nakumbuka alishiriki maadhimisho ya mila za Kizanaki kama Wazanaki wengine. Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa pamoja na dini za kimapokeo, bado Waafrika wana mila nzuri zinazopaswa kuenziwa. Huyo ndiye Mwalimu.

Hizi dini ndimo tunamofichia mambo yetu! Hata Kakobe, TBJ, Mzee Wa Upako, Gwajima, Joe David ni wakristu safi sana!
 
Ni kweli, ndio maana alikuwa anatembea na tunguli au kifimbo
 
nasikia yule mzee alikua ni mtata wanasema ata alipo kufa waligundua kwenye saa yake wanasema ilibadika rangi na wanasema kila raisi wa nchi hii lazima awe mkubwa wa wachawawi si unaona viongozi wetu wana mawazo ya kichawi chawi unakuta wanaongea vitu ambavyo havipo
 
Back
Top Bottom