Hizi tabia zinakera sana

16.Inaboa sana wahitimu wa wanapokuja kuanza kazi kwenye gate wakati procedure zinafutwa kuweza kuingia wanaanza kutukana walinzi kuwa hawajui kazi zao...na wakiingia watakuwa maboss wao.

17.Inakela sana wanafunzi wa Practical training wanapokuwa wajuaji wakati wanahitaji msaada na mwisho wa siku wanaandika jina lako kama umewasaidia.
 
1.0 Mtu anatumia choo, harafu anaachaa kuflashi.
2.0 Mijitu inasimama kati kati ya bara bara harafu inapiga stori bila kukaa kando.
3.0 Jitu kubwa kutongoza vitoto vya shule, vidogo vidogo.
 
Inakera sana maboss kuwa na upendeleo ofisini, utakuta kwa kuwa anampenda aisha basi safari zote za ofisi ni aisha tu, training zote ataenda aisha tu, madeal ya pesa yote anapewa aisha tu
 
11. Inakera zaidi pale unapopita mitaani mida ya asubuhi unakuta takataka zimerundika zaidi na kuchafua hali ya mitaa
12. Inakera zaidi demu unapokuwa naye katika date bila ridhaa yako anapomwita Waiter alete msosi na vinywaji na kukuachia bill na bila hata shukrani mnaishia kama vile mmegombana!

sasa jamani akam ana njaa acle?...lol
 
Inakera sana wanao pandisha bei ya bia ovyo ovyo wkt kwenye kizibo pameandikwa 1400/=
 
pale mtu anapokuuliza...zain yako (au voda) ina hela...kuna mtu nataka nimpigie....wewe wakati unanunua simu ulikuwa unategemea kuombaomba....inaboa sana
 
inakera mtu anapojitokeza kutafuta mwenza hapa jf halafu wengine wanamfanya kama mzaha wa siku...............!
inakera kuona mtu akichokonoa pua yake kutoa uchafu..............!
wanakera watu wanaojiona wako bora kuliko wenzao.................!
inakera taarabu zinazopigwa uswahili usiku kucha......................!
inakera kuona mbongo akijifanya kasahau kiswahili baada ya kuishi ng'ambo muda mchache..................!
wanakera raia wanaodhani ni lazima uwape lift sbb tu wewe ni jirani yao...............!
 
inanikera zaidi wabongo wanaoenda kusoma nje wana decide kuchukua urai huko, wanajenga nchi za wenzao wanasahau kuja kujenga yao. no uzalendo at all!
 
Wananikera sana watu wanaopenda kuchanganya lugha za Kiingereza na Kiswahili. Nashawishika kuamini kuwa watu wa aina hiyo hawawezi kuongea kwa ufasaha kwa kutumia moja ya lugha hizo na hivyo kulazimika kuzichanganya.
 
  • Ni upuuzi kuanza kumchukia Msichana / Mwanamke anapokuwa amekutolea nje andiko mradi la penzi

  • Ni ukosefu wa hekima kufikiri kuwa umri mkubwa na nyota zako ndani ya JF ndio tiketi ya wewe kuwa bora katika kuchangia hoja kuliko yule mgeni au aitwaye junior

  • Ni kituko kuendelea kumchunguza mwenzako kwa siri wakati tayari yeye anajua wazi kazi hiyo unayoifanya
  • Ni mparaganyiko wa viungo vya fahamu kuamini katika jambo fulani lakini hulitendi (ingawa una fursa na uwezo wa kufanya hivyo)
  • Ni ufisadi kukaribisha maoni ya watu katika blogu yako lakini ukaamua kuwa unaminya yale yote yanayo tofautiana na mapendeleo yako hata kama si matusi.
  • Inakera sana watu wanaoendelea kuweka uzito uliokithiri juu ya kuwa na Diwani, Mbuge na Rais fulani katika kuleta maendeleo nchini Tanzania bila kufikiria pia na kuweka uzito juu ya uwajibikaji wa Wananchi wenyewe mmoja mmoja au kama jamii
  • Mwalimu kuanza kuuza mitihani (au majibu yake) kwa Wanafunzi wake si tu kuwa ni uvunjaji wa maadili ya taaluma bali pia ni zoezi la kudhoofisha kiwango cha elimu katika nchi
  • Kuwazuia wanaume wafiwa kuomboleza kwa kulia waziwazi na au kuwalazimisha Wanawake kuomboleza kwa kulia (kwa nguvu) hata kama hawana hizo hisia ni ubinywaji wa uhuru wa kuonyesha au kutoonyesha hisia.
  • Ni ulimbukeni Msanii na Mapromota wake kuendelea kulandalanda bila maelezo wala kuomba radhi wakati muda uliowawekea wateja kuanzaa show umepita.
  • Ni uchafuzi wa hewa mabasi kuungurumishwa na kupiga honi nyingi sana za mwendelezo alfajiri bila kuondoka toka vituoni
  • Ni kudharau utu na haki ya Mwanaume kudhani kuwa kila anapotegwa au kupendwa na mwanamke yeyote lazima ajilegeze au amkubalie.
  • Ni kinyaa Sheikh, Maalim au Mchungaji au Askofu n.k kuwa muongo, mfitini, mwizi au mzinzi
 
hapo kwenye swala la kungurumisha mabasi stendi asubuhi limenigusa sana, utakuta kila basi linaburuza resi hapo stendi mengine ndio piston zimekufa ndo basi tena, hali ya hewa inazidi kuchafuka, lakini wahuisika wala hawalitambui hilo
 
Inakera sana pale baba/mama mwenye nyumba pale anapsema kama mmeshindwa kukaa hapa hameni kisa mwanae kagombana na wa mpangaji wake.
 
Inanikera sana pale siku ya public holiday kwenda kazini bila malipo
 
inanikera zaidi wabongo wanaoenda kusoma nje wana decide kuchukua urai huko, wanajenga nchi za wenzao wanasahau kuja kujenga yao. no uzalendo at all!

Uzalendo uanze kuonyeshwa na serikali kwanza kuwajali wananchi wake halafu watu binafsi ndio watafuata, tatizo siku hizi kila mtu amekuwa mbinafsi kwahiyo hata hao wanapotelea huku nje usiwalaumu, wanapigania tu nafsi zao kama vile tu wanasiasa wetu wanavyoweka mbele maslahi yao kwanza.
 
Inanikera sana pale boss wako wa kitengo unapomplekea matatizo yako ayapeleke ngazi za juu anakuambia mbona safi nshamaliza kumbe hajafanya lolote ni unafiki na woga.
 
1.Wananikera sana watu wanao sema ntaku dipu baadae badala ya ntaku beep baadae.
2. Wananikera sana watu wanooongea kwa sauti wakipokea simu kwenye daladala tena jitu lipo ubungo linadanganya nipo magomeni hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom