Hizi tabia zinakera sana

Hizi tabia zinakera sana

1) unakuta bodaboda iko mwendo wa kasi ajabu!!!!
kisha inapiga mziki mkuuubwa nakereka saaana

2)unamkuta mtu na mswaki mdomoni
anakatiza mitaani domo limechafuka
naweza kutapika

3) kwenye daladala unakuta watu wawili wanaongea kilugha
cha kwao kwa kelele mpaka inakuwa kero kwa wengine
haaa tena wengine wanakulaga na miwa juu
asee nakasirika sana lool af ukute upo dirishani sasa yeye anafanya jitihada
za kutupa maganda yake hayo ya miwa
mara yakurukie aaaghhhhrrrr naweza kumkata vibao asee!!!!!!


NB:hao wamachinga wanaouza sumu
za mende.....asee af unakuta hizo supika zao
zina mgogoro wa battery hahaha
zinakoroma balaa khaaaa


1. Utakuta mtu anatembea barabarani huku anavuta sigara hajali kuwa moshi wa hiyo sigara yake unakera watu
2. Mtu anatembea barabarani anatema mate au anapenga kamasi hovyo hovyo kila mahali bila ustaarabu
3. Mtu anakupa business card siku unamtafuta ukipiga namba za simu zilizoko kwenye card hapatikani
4. Hawa wamachinga wanaouza vitu wakitumia kispika saa zote kikisema 'dawa ya mende, mchwa, mba na mapunye inapatikana hapa' kinarudiarudia kwa kweli kinaleta kero
Na mengine mengi yenye kero katika jamii yetu, Hii inakera sana
 
5. Inakera sana msomi anakula kwenye basi na kutupa mifuko na chupa dirishani!
6. Inakera sana mtu anaongea na simu kwa sauti ya juu kwenye public!
7. Inakera sana dada mrembo anatupa ovyo maganda ya chocolate!
8. Inakera sana mtu ameomba simu ya mtu apige anaanza kuangalia salio!


hapo pekundu tena kwa kiluga loool.
 
12. Inakeresha sana kwa mara yakwanza unapomwambia demu achague sehemu ya date na anakupeleka kwenye kiota cha bei chafu ambacho yeye na familia yake mzima hawajawahi kukanyaga
13. Inakeresha sana mbu, paka, mbwa, na nzi wanapovamia kituo cha raha chini ya mti nyakati za jioni
14. Inakeresha na kutapisha wauza samaki, mchicha, DVD, sidiria, vinyago n.k wanapovamia meza ya makulaji kwenye bar za chini ya mti


asee wanaweza kukukata moto vibaya hawa wamachinga
kuna na yale mapaka ya bar kila
ukimega tonge lenyewe nyaaaaau
nakerekaga saaana

 
aseee full mziki kama sabufa limefungwa hapo bank
kelele mtindo mmja hahahah
 
asee inaweza kukuuwa kwa presha ikipigwa bila wewe
kuitarajia, hebu fikilia unawaza ugumu wa
life ,wattoto hujawaachia kitu cha kueleweka
home mara honi mgongoni
tena na hilo boda lina mziki wa kichina
kero saaaana



15.bodaboda inapowekewa honi ya lori na kupigwa hovyohovyo inakerasana.
 
na weweeee.kutunza mazingira ni kila mtu
awe kilaza au msomi inakera tuu mtu
kutupa matakataka hovyo period
 
9. Dereva anaona mko mnasota kwenye foleni anatoka nyuma anataka aje akae mbele yako kama vile ana haraka kuliko watu wengine
10. Mtu anakujia ana shida anaomba umkopeshe pesa kwa ahadi ya kukurudishia kesho, hiyo kesho unasubiri haifiki mpaka unajuta kumkopesha
11. Mtu anakuahidi kitu na kukuomba umpigi baadae, hiyo baadae kila unapopiga hapokei simu wala hajibu meseji
Hiyo namba 10 imenikuta, kwa mama mwenye nyumba wangu, ni mwezi wa 3 sasa na mbaya zaidi anaingia mpaka chumbani ninakolala, si ndo mwanzo wa kutonilipa huo jamani maana duh!!!!!
 
Wale wa uswazi jirani akiskia unaangalia movie akugongea eti nae aingie mtazame wote,unakuta upo ma mpenzio mnajiachia hata bila nguo kupata hewa et jiran nae anataka loool
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom