Hizi tabia zinakera sana

dropingcoco

Senior Member
Jun 21, 2008
124
11
1. Utakuta mtu anatembea barabarani huku anavuta sigara hajali kuwa moshi wa hiyo sigara yake unakera watu
2. Mtu anatembea barabarani anatema mate au anapenga kamasi hovyo hovyo kila mahali bila ustaarabu
3. Mtu anakupa business card siku unamtafuta ukipiga namba za simu zilizoko kwenye card hapatikani
4. Hawa wamachinga wanaouza vitu wakitumia kispika saa zote kikisema 'dawa ya mende, mchwa, mba na mapunye inapatikana hapa' kinarudiarudia kwa kweli kinaleta kero
Na mengine mengi yenye kero katika jamii yetu, Hii inakera sana
 
1. Utakuta mtu anatembea barabarani huku anavuta sigara hajali kuwa moshi wa hiyo sigara yake unakera watu
2. Mtu anatembea barabarani anatema mate au anapenga kamasi hovyo hovyo kila mahali bila ustaarabu
3. Mtu anakupa business card siku unamtafuta ukipiga namba za simu zilizoko kwenye card hapatikani
4. Hawa wamachinga wanaouza vitu wakitumia kispika saa zote kikisema 'dawa ya mende, mchwa, mba na mapunye inapatikana hapa' kinarudiarudia kwa kweli kinaleta kero
Na mengine mengi yenye kero katika jamii yetu, Hii inakera sana

hicho huwa kinakera sana
 
Inakera zaidi hizi boda boda kupiga piga honi kila saa katika njia za wapita kwa miguu! piii piiii pii pi pi piii piiiiiiiii! Hovyo kabisa!
 
Bajaj zinavyoendeshwa bila hata kufuata sheria.Nina mashaka kama madereva wake wana leseni au hata wanajua sheria za usalama barabarani!
 
5. Inakera sana msomi anakula kwenye basi na kutupa mifuko na chupa dirishani!
6. Inakera sana mtu anaongea na simu kwa sauti ya juu kwenye public!
7. Inakera sana dada mrembo anatupa ovyo maganda ya chocolate!
8. Inakera sana mtu ameomba simu ya mtu apige anaanza kuangalia salio!
 
Watu wenye meno yaliyo na irregular allignment wanakera sana wanapocheka na kukenua....

Go get some braces
 
9. Dereva anaona mko mnasota kwenye foleni anatoka nyuma anataka aje akae mbele yako kama vile ana haraka kuliko watu wengine
10. Mtu anakujia ana shida anaomba umkopeshe pesa kwa ahadi ya kukurudishia kesho, hiyo kesho unasubiri haifiki mpaka unajuta kumkopesha
11. Mtu anakuahidi kitu na kukuomba umpigi baadae, hiyo baadae kila unapopiga hapokei simu wala hajibu meseji
 
12. Inakeresha sana kwa mara yakwanza unapomwambia demu achague sehemu ya date na anakupeleka kwenye kiota cha bei chafu ambacho yeye na familia yake mzima hawajawahi kukanyaga
13. Inakeresha sana mbu, paka, mbwa, na nzi wanapovamia kituo cha raha chini ya mti nyakati za jioni
14. Inakeresha na kutapisha wauza samaki, mchicha, DVD, sidiria, vinyago n.k wanapovamia meza ya makulaji kwenye bar za chini ya mti
 
Inakera sana unapanda kwenye basi halafu unasimama karibu na mtu ananuka jasho vibaya mno,halafu mbaya zaidi anakuwekea kwapa karibu na pua...yani kero kubwa!
 
Inakera sana kuishi na mtu mmbea, anatunga tunga tu mambo mwisho wa siku unaoneka wa ajabu katika jamii
 
inanikera sana unapojua fulani na fulani wana mahusiano na wewe unatongoza palepale
 
Inakera sana mtu unapokuwa serious kuuliza jambo JF wengine wanaleta masihara
 
Inakera sana nyie mnaoingia Benki na simu za kichina mmeweka milio ya nyimbo za ajabu ajabu na sauti za juu.
 
11. Inakera zaidi pale unapopita mitaani mida ya asubuhi unakuta takataka zimerundika zaidi na kuchafua hali ya mitaa
12. Inakera zaidi demu unapokuwa naye katika date bila ridhaa yako anapomwita Waiter alete msosi na vinywaji na kukuachia bill na bila hata shukrani mnaishia kama vile mmegombana!
 
Inakera mtu anakutumia sms yenye lugha chafu wakati humjui na unauhakika kabisa kakosea namba, unampigia kumwambia wrong number anang'ang'ania kuwa hajakosea na kuzidi kukuporomoshea lugha chafu
 
15.bodaboda inapowekewa honi ya lori na kupigwa hovyohovyo inakerasana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom