Hizi St. Makafyondo nazo! Kisa cha Mwalimu wa field...

Hizi St. Makafyondo nazo! Kisa cha Mwalimu wa field...

sakapal

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
1,804
Reaction score
1,425
Jamani kuwa mzazi nako shuhuli kama huna general knowlegde au baadhi ya vitu huvijui nouma.
Kisa hiki kimenitokea jana usiku niliporudi nyumbani mida ya saa 2 usiku nikamkuta mtoto wa wifi yangu yuko standard 5 ni wa kiume(huyu nakaa nae for family reasons) huwa wanalala mapema sasa nikamuuliza why hujalala? Akaniambia shangazi kuna mwalimu amekuja shuleni kwao ni wa field hivo atawafundisha kwa muda wa miezi miwili somo la sayansi na kurudi masomoni. Sasa jana baada ya kuwafundisha akawaachia kazi za makundi na yeye ndio kiongozi wa kundi lao. Wameambiawa waandike paragraph moja kueleza kuhusu kujamba. Waeleze kawaida mtu anajamba mara ngapi kwa siku na kama si kawaida atakuwa anajamba mara ngapi kwa siku yaani kama ikionekana huyu anamatatizo ya kujambajamba. Na je kuna ambao hawajambi kabisa? na wasiojamba kabisa ni wagonjwa? Kazi hiyo inatakiwa jumatatu sasa aliponiuliza hivyo anaomba msaada maan mara nyingi huwa namsaidia kumuelewesha na yeye kukamilisha homework yake. Hajui chochote kuhusu hilo na huyo mwalimu amewaambia kundi likija halijafanya watapata adhabu akanisihi sana nimsaidie..........
Daah nikawa kwanza puzzled na maswali kibao ambayo sikuwa na majibu yake..... hivi huyu mwalimu anachofundisha ni sahihi? ni sayansi au ni topic mpya? maana mie sikufundishwa hivyo. Au huyu mwalimu anakusanya dodoso ya paper anayofanya shuleni? Hakuwa na cha kufundisha hivyo kuvutamuda uende darasani? Au mie ndo sijui niko nyuma ya wakati?
Kwakweli sijui hata swali moja na nilimwambia mtoto wa wifi yangu akalale nitamsaidia jumamosi kwani nimechoka, ila nilimjibu hivyo ili kuokoa jahazi maana hata sikutegemea kuulizwa swali kama hilo. Kwenu wana jamvi msaada kwa hayo maswali tafadhali sio utani wala sio kichekesho, asante kwa msaada utakaonipa.
 
Itabidi wakifeli awape karatasi ya majibu
 
hiyo nayo kali kuliko,mi mwenyewe sijawai fundishwa hyo kitu,tuwasubiri wajuzi wa mambo waje huenda wana jibu!
 
mmh imenishangaza kwa kweli.ufundishaji gani huo?ni kuwapotosha wanafunzi tu
 
ingekuwa mimi ni mzazi wa huyo mtoto,ningeenda kuyauliza shule.na hiyo assignment mwanangu asingeifanya,maana mtu yoyote utakayemuuliza kuomba msaada kidogo atashangaa
 
ingekuwa mimi ni mzazi wa huyo mtoto,ningeenda kuyauliza shule.na hiyo assignment mwanangu asingeifanya,maana mtu yoyote utakayemuuliza kuomba msaada kidogo atashangaa
sakapal nisamehe kwa kuwa nimecheka! (pengine ni kicheko cha kusikitika) embu nenda naye kwa mwalimu wake wa darasa am yoyote kuwauliza hiyo kitu kama kisukari alivyosema. utapata kujua mengi huko. Tujulishe pia.
 
Last edited by a moderator:
Ila kuna facts kuhusu kujamba (au kufart, ili kupunguza makali) , kuwa normal human being anatakiwa a-fart 14 kwa siku, na ikizidi hapo ni kwamba umekula chakula ambacho hakiendani na mwili wako (yaani kina gas sana), na mambo mengine mengi yapo utayaona kama uki-google. So sidhani kama mwalimu alikuwa na nia mbaya, japo sidhani hiyo toipic nayo ipo kwenye silabasi, kama ulivyosema huenda anafanya papers.
 
Dero siku hz hakuna silabasi kila mlm anafundisha anachojiskia . Hujaona hoja ya Mbatia kule Jukwaa la siasa
 
owiwiiiiiiiiiiiiii, yaani hii nayo kazi kweli kweli mie sijawahi sikia hii kitu, may be ndo mtaala mpya mbona anawapa watoto hawa adhabu ya kufikiria kwa kiwango ambacho hakiendani na umri wao? loh.
 
Walimu wengi wa miaka ya karibuni ni JANGA LA TAIFA(BOMU LINALOSUBIRI KULIPUKA)...na hii yote ni kutokana na sera mbovu za "sirikali" kutaka tu kujiridhisha kuwa walau kila mtu kasoma hadi elimu ya chuo.
Nadharia ya kujamba ni elimu kubwa sana kwa watoto wa shule ya msingi...hebu hakikisha huyo mwalimu unaonana naye maana nahisi "akili zake hazina akili nzuri"

::Samahani kwa waalimu mliopo hapa jamvini, ila nisiposema mimi ukweli basi kuna mwingine atasema tu utofauti ni kwamba pengine nimekuwa wa kwanza.
 
Tenga mda cku ya jumamosi au juma pili ambayo huendi kwa kazi ushnde nae then umwambie awe anahesabu kila utakavokuwa unajamba, tena jitahd utoe ushuzi kwa sauti usimuonee aibu. Well done mwl wa digital.
 
Ndala ndefuuuu Khaaa!!!!
 
KWani si mmeona kule mjengoni serikali imedhihirisha hakuna mtaala? kwa hiyo kila mtu anajifundishia tuu ili mradi
 
my wee!pole ndo mabadiliko ya mtaala hayo ngoja nimwite gfsonwin atwambie au Baba V au Madame B

jamani mwl mwenzangu snowhite kwani tunapowafundisha wanafunzi digestion system tunategemea kumfunza mtoto?? hii ni kama eneo la kutilia mkazo kwa mwanafunzi na mwl mzuri huwa swali kama hili amelenga kumfanya mtoto ajue mechanism yote ya jambo husika.

farting ni biological process na ina mechanism yake kabisaa tena kitaalam na huwa ikikosewa baasi huwa ni tatizo. na mtu asipojamba basi tutegemee awe na tatizo kwenye mfumo wake wa umenng'enyaji chakula.

kwa kumsaidia mwl anategema mwanafunzi aje na generala knowledge ya farting nikiwa na maana mechanism behind it.

nashangaa sana kuona hata hapa jf watu wanaona kama mwl kakosea nachelea kusema kwamba tujifunze kuwaacha watoto wasome yaani wapate elimu na tusiwaekee limitations katika kusoma. hivi utajiskiaje mwanao anamaliza shule hajui kwikwi inatokana na nini ama kujamba ama kupiga chafya ama kupiga miayo?? je utasema kaelimika kama vitu basic kama hivi havijui??
 
Bibie ungekuwa karibu ungeona jinsi nilivyofurahishwa na jinsi ulivyoliona hili suala; sidhani kama mwalimu alikosea hata kidogo kama wengi wetu humu tunavyojitahidi kuonyesha-inawezekana mwalimu alitaka kupima uelewa na umakini wa wanafunzi wake.
Mleta mada ulifanya busara sana kuahirisha kujibu swali hilo hadi ujipange bila kutoa negative comments kwa hiyo assignment kwani moja ya makosa makubwa tuyafanyayo kama wazazi ni ku undermine kazi na uelewa wa walimu wanaofundisha watoto wetu matokeo yake watoto huwa sio wasikivu tena kwa walimu hao kwa sababu tayari wanawaona ni 'vihiyo' kama ambavyo uliwahi kusema siku moja!!
 
thanks. mm kama mwl wa biolojia jambo la kwanza mwanafunzi wangu wa form two analotakiwa kulijua ni MECHANISM BEHIND THESE BIOLOGICAL PROCESSES KWIKWI, CHAFYA MIAYO NA KUJAMBA. kwangu mm ni basics za kujua body systems vizuri zaid kuliko njia nyingine.

ningependa kuwashauri wanajamvi kuhusu elimu ya watoto wenu hebu oneni umuhimu wa kumwamini mwl na kazi yake. oneni kwamba waalim wako committed na wanachokifanya, jueni kwamba hatupendi watoto wenu wafeli manake kufeli kwao ama kufaulu kwao hakautusaidii sisi hata kidogo. pia wapeni watoto muda wa kujifunza wakaelimika na sio wakahitimu jamani. mkitaka tuwafunze ili wahitimu tu inawezekana kabisa lkn hakuna maana manake elimu kusudia inakuwa hajaipata mtoto.

imagine wewe ni mzazi una mtoto wa form 4 ukimuuliza kwikwi inatokana na nini hawez kukuelezea ama hajui hata kujamba kunaitwaje kiingereza halafu unajisifia mwanagu yuko kidato cha nne kweli tunataka waelimike??

nchi za wenztu jamani nimetembelea germany wakati fulan wanafunzi wa huko primary school unamkuta anajua kuelezea vitu utafikiri ni mwl wa huku kwetu nilishangaa sana nikaona sisi bado tuko nyuma sana. leo hii mwanafunzi wa darasa la 3 ukimuuliza organ5 za faham hajui wala ukimuuliza seli zikijumuika huunda nini hajui. halafu bado mzazi unasema eti hii ni kazi ya mwl kapewa anataka mwanafunzi amfanyie kweli mko fair kwa waalim?? ama mnataka tuwatengenezee taifa lenye vilaza??
sakapal uliwah kusema waalim ni vihiyo lkn hao hao vihiyo wanajitahd mwanao apate elim asiwe kihiyo bado wewe unakuwa na mashaka na wasiojua wanakusahuri eti nenda shule kamuulize mwl kama hiyo ni syllabus. Jiulize hivi nani anayehakiki scheme ya mwl?? ni academic master tena wala haakiki subject matter bali ana hakiki kama imefikiwa lengo, anayehakiki subject matter ni mwl wa somo husika tu basi na kipimo cha mwisho kwa mwl huyu ni mthani wa taifa kama mlikuwa hamjui.

ingekuwa mm ndo mwl mzazi unakuja hivyo ningekujibu hivi nenda na mwanao nyumban kamfundishe unavyofikiri ndivyo anavyotakiwa kujifunza. manake huna imani na mimi kabisa lkn jua nina teknik zote ama za kumfanya mwanao afaulu ama afeli. na FYI ingawa mtihani unasahiahishwa na baraza mwl akikusudia mwanafunzi fulan afaulu somo lake anaweza kabisa kumfanya afaulu tena kwa flying colors na akitaka asifaulu anaweza akamfelisha milele.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom