Hizi sio Tabia za Watanzania Ninaowajua.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Kuna matukio Yanatokea nchini Mwetu ambayo kwa haraka haraka sio Tabia za Mtanzania/Kitanzania kipindi cha nyuma hata kama yalikuwepo ni kwa uchache sana ila kwa sasa hapana too much.

Isifike Mahali Watanzania tukaanza kuingia hofu eti kesho yangu itakuaje tukaanza kunyimana Amani ndani ya nchi yetu sitaki kuamini kama hilo litakuja kutokea kwenye kisiwa hiki cha Amani.

Kuna matukio Yanatokea hapana kwa kweli sikuwahi kuyaona,Mtu kushikiwa bastola kwenye Umati wa watu,watu kupotea kimazingaombwe,,,nk

Kwa kweli sio matukio mazuri kwa nchi yetu hata kidogo mtu kukushikia bastola kwa hesabu za haraka ni kutaka kukutoa uhai wako na sio kingine kwa hapa nipo kinyume kabisa

Hizi hazijawahi kuwa tabia za Mtanzania ninayemjua mimi kama tumeiga mahali HAPANA tuwarudishie tu tabia zao hazitufahi Watanzania.
 
Kuna watu Uki Dili na Mitazamo yao Utajipa mastress Nasemaje Kesho yangu haijui Magu wala siro Kesho yangu Anaijua Mungu tu Amen
 
Angetupa na mifano hai kuonyesha huo ukawaida sana kuanzia lini!? Watanzania wangapi hutekwa kila mwaka!? Mbona hatujawahi kusikia hili la Watanzania kutekwa nchini pamoja na yeye kudai ni la kawaida sana!?
Ni la kawaida sana... Sema ni kwavile wanaotekwa sio watu popular. Njoo polisi uone kesi zilivyo nyingi
 
Sasa anaposema ni kawaida sana sisi hatujui huo ukawaida ndiyo nikasema angeweka na ushahidi husika ili Watanzania tuufahamu huo ukawaida sana.

Ni la kawaida sana... Sema ni kwavile wanaotekwa sio watu popular. Njoo polisi uone kesi zilivyo nyingi
 
Hongera kwa kuliona hili,hizo ndiyo gt zinazotafutwa humu.Hii siyo tabia ya kitanzania,kutekana nyara,kutukanana kama walevi,kupinga kila kitu,siyo utanzania huu. Kama muziki ulikuwepo,kama siasa zilikuwepo tu na tulipingana kwa kuheshimiana.
 
Kuna matukio Yanatokea nchini Mwetu ambayo kwa haraka haraka sio Tabia za Mtanzania/Kitanzania kipindi cha nyuma hata kama yalikuwepo ni kwa uchache sana ila kwa sasa hapana too much.

Isifike Mahali Watanzania tukaanza kuingia hofu eti kesho yangu itakuaje tukaanza kunyimana Amani ndani ya nchi yetu sitaki kuamini kama hilo litakuja kutokea kwenye kisiwa hiki cha Amani.

Kuna matukio Yanatokea hapana kwa kweli sikuwahi kuyaona,Mtu kushikiwa bastola kwenye Umati wa watu,watu kupotea kimazingaombwe,,,nk

Kwa kweli sio matukio mazuri kwa nchi yetu hata kidogo mtu kukushikia bastola kwa hesabu za haraka ni kutaka kukutoa uhai wako na sio kingine kwa hapa nipo kinyume kabisa

Hizi hazijawahi kuwa tabia za Mtanzania ninayemjua mimi kama tumeiga mahali HAPANA tuwarudishie tu tabia zao hazitufahi Watanzania.
Watu wapo tayari kufanya baya lolote ili waendelee kutawala.
 
Anafuata ushauri wa Kagame..Muhima mwenziwe kwa ufupi yule mtu ni Mnyarwanda
 
Ni la kawaida sana... Sema ni kwavile wanaotekwa sio watu popular. Njoo polisi uone kesi zilivyo nyingi
Kama unayosema ni kweli basi Tanzania tumefika kubaya sana, na ingebidi Sirro ajiuzuru mara moja kwa kushindwa kuyazuia matukio hayo na pia kushindwa kuyaweka wazi hayo matukio ya kutekwa kipindi chote hicho.

Nini maana ya kuwa na jeshi la Polisi nchini, kama matukio ya utekaji nyara ni mambo ya kawaida. Kidunia tukio lolote la utekaji Nyara ni 'Biggest Evil' na nchi yoyote yenye kesi nyingi za namna hiyo inapaswa kutangazwa kama Eneo hatari zaidi katika dunia, na mara zote wageni na watalii huonywa vikali wasifike kabisa maeneo hayo. Ni sawa sawa na kutangaza mlipuko wa Ebola katika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom