Hizi Radio ni za CCM?

Hizi Radio ni za CCM?

Nadhani muadhama askofu mstaafu ana uhuru wa kutoa mawazo yake.Kumbuka vyama havina dini na dini haina chama yawezekana hayo mawazo ni ya kwake binafsi siyo ya dini yake
 
Dah mkuu mimi nilikuwa namheshimu sana huyu mtumishi wa Mungu ila alichokifanya leo kimempotezea heshima yake yote kabisaa.Sikusikia kabisa kama amegusia ibara ya kwanza au ya sita zaidi ya vijembe kwa UKAWA.Halafu hapa eti tutegemee katiba kama hata viongozi wa dini wanashindwa kujitofautisha na ma.poyoyo ya CCM!!
 
Waacheni wafu wazikane,UKAWA MBEEELE

Askofu anajua anachotakiwa kufanya.ni kada wa ccm kwa kupitia kivuli cha dini.anaaibisha kanisa.nilitegemea angetoka jana kumbe yupo.ndio maana tulisikia kundi la 201 ni makada wa ccm leo imejidhihirisha kwa huyu askofu
 
Mahali sasa viongozi wa dini wanapo potea ni wakati unaamriwa kuicheza ngoma usio ijua. Mtetemela na Utakatifu wa Julius! Ama kweli, kabla hatujafa tutaona mengi. Mzee huyu na heshima zake anaamriwa asifie maiti. Haya mzee nawe tumekusikia. Njaa mbaya saana ndiyo imemweka pale mjengoni leo. Avute za bunge na hizo za Ikulu.
Kama umemtumikia Mungu miaka yoote mpaka ukastaafu kazi yake haku kukumbuka hizi za siku 90 hazitakutosha. Tuwe wa kweli tu

cc mtetemela
 
Ni li kada la CCM kama alivyo PENGO, maaskofu wa ukweli ni RWAICHI, MALASUSA, MOKIWA na yule RAIS wa TEC hawa wengine wanashiba kama viongozi wa CCM
 
Anajiosha tu huyo hana lolote anajipendekeza kwa ccm kama wanaweza kumfikiria kwa lolote,njaa hizi mbaya sana,, na ccm wamemtumia makusudi kwa kigezo cha uchungaji.

Mzee huyu wa watu amekuwa mnafiki Kwa kuonyesha dhahiri yuko Chama gani. Huu ni usaliti Mkubwa na udhaifu Mkubwa wa kifikra kwani alipaswa kuwa neutral. Kwa staili hii pia amegawanya Kanisa vipande viwili
 
Mtemelwa ameagizwa kusema aliyoyasema. Tumbo kwanza utaifa baadae
 
Anajiita askofu mstaafu,anawakilisha vikundi vya dini,.
Lakini porojo zake ni kuisifia ccm badala ya kuwa neutral.
Kamaliza kwa kusema kwamba wanaobeza kwamba ccm kwamba hawajaleta maendeleo hawana macho

Ndugu zangu naona mumeshasahau kuwa Asikofu mtetemela kuwa ni kada wa CCM na aligombea ubunge jimbo la Dodoma mjini kupitia CCM na akashindwa kwenye kura za maoni.
 
Kanisa la huyu askofu linaongozwa na mashoga na yeye alikua ni miongoni mwa watu saba wanalolishauri kanisa la agilkan ambalo linaongozwa na mashoga kwa hiyo tuwe makini anaweza kupendekeza katiba yetu iwe na mashoga
 
Kiongozi wa kidini anapaswa kuonya, kukemea ama kushauri pande zote mbili za majadiliano pasipo kuonesha msimamo wake kisiasa kwani yeye sio mwanasiasa. Kwa kweli askofu yule amefanya makosa makubwa ambayo yatamfanya hata muumini wake asimuelewe kwa kutoa msimamo wake hadharani.
 
Baada ya Ukawa kutoka bungeni jana leo ndio nimejua matawi ya Radio Uhuru. Nikianza na Clouda fm,RFA, yaani wamekuwa mawakala wa kuisemea CCM Leo.

tAARIFA YA KUTOKA NJE WABUNGE WA UKAWA NILIIPATA JANA JIONI MUDA MFUPI KUPITIA CLOUDS FM KAMA BREAKING NEWS. BWANA SIMALENGA AMBAYE NADHANI NI MWAKILISHI WA CLOUDS MEDIA HUKO BUNGENI DODOMA AKATOA SABABU ZA WAJUMBE KUTOKA NJE. KWANZA NIKAWA NA MASHAKA KAMA ILIKUWA NI KWELI KWANI NIMEWAHI KUMSIKIA LIVE KATIKA KIPINDI CHA JENERALI ON MONDAY AKITOA MAWAZO YAKE KUHUSU RASIMU YA KATIBA NA MAWAZO YAKE HAYANA TOFAUTI NA WAJUMBE WANAOJIITA WENGI. NIKAFANYA KILA JITIHADA NIKAMSIKIA KWA MASIKIO YANGU PROF LIPUMBA BBC JIONI ILEILE NIKASHANGAA SANA HUYU SIMALENGA KAZITOA WAPI SABABU ALIZOZITOA. KATIKA MASUALA YA KISIASA MARA NYINGI CLOUDS NAPONA WANABASE UPANDE WA CCM NA SERIKALI KWA UJUMLA. ANYWAY WANAWEZA KUWA NA SABABU ZAO
 
Back
Top Bottom