Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Mpenzi wangu amekuwa na hali inayonichanganya sana. Nashindwa kuelewa kama ni hasira za kawaida au kuna jambo zaidi. Kila mnapokuwa katika maongezi chochote atakacho-comment mara zote ni katika tone ya ukali..Mwanzoni nilidhani huenda kuna mambo yanayomtinga akilini hadi kumfanya awe hivyo lakini ni zaidi ya mwaka sasa hata mazungumzo ya kawaida tu huwa katika hali ya ukali usiokuwa na sababu. Rafiki yangu mmoja akanishauri kuwa nitafute mtaalamu wa ushauri nasaha ili aweze kupata kitu wanaita wenyewe " anger management class". Hivi wataalamu wa aina hii wapo hapa Tanzania kwa anayefahamu anijulishe maana sipendi kwa kweli kumpoteza huyu honey wangu lakini hili tatizo laweza kunifanya ni-act differently!!!.