MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,239
- 22,318
Tukiachana na labda kushindwa kugharamia mambo yale ya lazima ili uweze kuishi, au kutokuwa na nyumba wala usafiri, basi hizi hapa dalili zingine ambazo hazitajwi sana ila zinamtafsiri kuwa huyu mtu ni maskini na anapaswa apambane sana.
1. Kuweza kuhesabu hela zako zote kwa mkono bila msaada wa mashine.
2. Hela zako zote kuenea kwenye wallet na wallet kukaa vizuri kwenye mfuko wa suruali bila kushtukiwa na yeyote.
3. Kutakiwa kujitambulisha kila sehemu utakayoenda. Waliofanikiwa wote huwa wanatambulishwa au MC husema "natambua uwepo wa Mr Mrangi hapa".
4. Kutowahi kutumia milango ya JNIA ile ya wanaoondoka na wanaowasili. Ina maana kutowahi kupanda ndege. Wenye mafanikio hujali muda.
5. Kuwa na pato la chini ya USD 10000 kwa mwaka. Yaani kama Tsh 23m kwa mwaka. Pambana sana.
6. Kuwaona wanaonunua magari ya kifahari kama vile wanatapanya pesa. Unaona mtu katumia labda Tsh 70m kununua ndinga kali halafu wewe unadai bora angenunua kiwanja. Huo ni umaskini.
7. Kuulizia bei kwanza kila ukiingia hotelini au mgahawani.
8. Kuwa na mashaka na kila tajiri kwa kudhani katumia mbinu chafu kupata utajiri.
9. Kuonyesha chuki kali kwa kina dada wanaoomba hela kwa wapenzi wao na kudhani wapenzi wao ni wajinga kutoa hela zao.
10. Kuomba punguzo la bei hata kwa kina mama wauza mboga mboga na vitu vingine vya nyumbani.
Kama una dalili zingine mzitaje.