Kama una miaka 30 na zaidi na bado unaishi maisha haya, basi wewe ni kubwa jinga

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
1. Hela ya vocha, kunyoa na kumpa demu wako bado unategemea upewe na baba au shemeji

2. Kula yako ni ya shikamoo baba au shemeji unasubiri msosi wa kengele

3. Huna mpango wa kupanga wala kujitegemea kwa kisingizio huna ajira

4. Ukiamka asubuhi break yako ya kwanza kijiweni kuzungumza habari za siasa au mpira mchana unarudi nyumbani unakula chakula cha kengele jioni unarudi tena kijiweni kwa washikaji unarudi nyumbani msosi wa kengele

5. Kurudi nyumbani unapangiwa muda wa kurudi ukichelewa zaidi unachapwa bakora au fimbo na baba na umri huoo

Haya aendeleeni wana JF DALILI ZINGINE
 
Kwanza, pamoja na kutuita kubwa jinga Mkuu. Tambua kwamba maisha ni kuchagua siyo lazima wote tuishi kama unavyotaka wewe. Hayo ndiyo maisha tuliyoyachagua.

Pili, kama kila kitu kipo nyumbani kwanini mtu akateseke kwenda kupanga? Mateso ya kupanga ni makubwa sana wakati maisha ni haya haya. Kwanini ujitese? Au kujitesa ndiyo kunakufanya uonekane kidume?

Tatu, angalia maisha yako mkuu. Achana na maisha ya watu kabisa.
 
Wengine kwao hakuna nafasi hivyo lazima waondoke waachie nafasi, lakini wengine wazazi wao walijipanga kuishi na watoto wao maisha yote hivyo wakaandaa nafasi na mazingira ya kutosha kufanikisha hilo.

Usiongee vitu kwa ufinyu wa ujuzi.

Kawatafute wahindi na waarabu uone wanavyoishi.
 
Wengine kwao hakuna nafasi hivyo lazima waondoke waache nafasi, lakini wengine wazazi wao walijipanga kuishi na watoto wao maisha yote hivyo wakaandaa nafasi na mazingira ya kutosha kufanikisha hilo...
Umeongea point sana, Mimi niliondoka nyumbani mapema sababu hakuna nafasi, sahivi na familia(mke na mtoto mmoja) sijajenga kwangu ila nimejenga nyumbani nyumba ndogo naimalizia kuezeka ili nipate nafasi nyumbani hata mke wangu akienda kusalimia awe comfortable baada ya hapo ndio ntadili na familia yangu.
 
Wengine kwao hakuna nafasi hivyo lazima waondoke waachie nafasi, lakini wengine wazazi wao walijipanga kuishi na watoto wao maisha yote hivyo wakaandaa nafasi na mazingira ya kutosha kufanikisha hilo.
Usiongee vitu kwa ufinyu wa ujuzi.
Kawatafute wahindi na waarabu uone wanavyoishi.
Na wasomali mkuu!

Nyumba baba, babu, bibi, shangazi, bamdogo, watoto wote wameoa wapo pamoja!

Everyday is Saturday.:cool:
 
Back
Top Bottom