Hizi ni baadhi tu ya faida za kusoma vitabu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,907
FAIDA KUMI (10) ZA KUSOMA VITABU.

1. Ni chakula cha ubongo. Bila kusoma ubongo unadumaa. Hivyo inakupasa kusoma ili kukuza ubongo/akili yako.

2. Vitabu vinakufikisha mahali popote duniani. Utapata kufahamu mazingira na maisha ya watu wengine waishio mbali. Ninaye rafiki, anafahamu miji na mitaa ya Uingereza utadhani ameishi huko. La hasha! Anasoma sana vitabu.

3. Unataka kuwa mzungumzaji mzuri?. Soma sana vitabu. Maana vinakuza stadi ya lugha, ambayo itakusaidia kukuza ulumbi wako. Mlumbi ni mtu mwenye uwezo wa kuzungumza kwenye hadhara.

4. Vitabu ni chanzo cha Hekima. Fanya utafiti, mtu anayesoma sana vitabu huwa na uwezo mkubwa wa kutafakari na kufanya maamuzi sahihi. Maneno na matendo yake ni yenye kujenga na kupendezwa na jamii. Mwenye hekima hazungumzi visivyo na maana, haropoki hovyo, hajivuni. Hushauri mema, huleta suluhisho la migogoro, huleta mawazo chanya katika jamii.

5. Hupunguza msongo wa mawazo. Soma sana vitabu ili kupata utulivu wa fikra. Ondokana na 'stress' kwa kusoma vitabu.

6. Unataka kuwa mwandishi mzuri? Soma sana vitabu. Hii inakuwezesha kuona na kujifunza kutoka kwa waandishi wengine, jinsi wanavyotumia lugha na kujenga mtiririko wa fikra,

7. Vitabu vinakupa maono. Kwanini? Vinatujuza mambo yaliyopita na yanayoendelea kufanyika. Kupitia hayo, tunaweza kujua nini kinaweza kufanyika huko mbeleni. Kuna usemi unaosema "experience leads" yani uzoefu huongoza. Kiongozi mzuri ni yule mwenye uzoefu. Uzoefu humuwezesha mtu 'kunusa' 'detect' mambo yanayoweza kutokea mbeleni.

8. Vitabu vinakukutanisha na watu na kukuza urafiki. Mfano mzuri ni mimi na wewe hapo. Tumeweza kufahamiana kupitia kitabu ulichoandika. Pia wewe na yule mmeweza kufahamiana kipitia vitabu. Pia vitabu vimenikutanisha na wasomaji wa kitabu chako.

9. Hazina kwa vizazi vijavyo. Kusoma kuna faida kuliko kusikiliza. Maana fasihi andishi inadumu kuliko fasihi simulizi. Vitabu ulivyohifadhi kwenye shubaka (shelf) lako sasa hivi, vitasomwa na vitukuu vyako miaka 100 ijayo. Tofauti na hadithi unayosimuliwa sasa, itapotea siku msimuliaji akifa. Teknolojia ya kuhifadhia sauti leo, inaweza isiwepo miaka 100 ijayo.

10. Kiingiacho ubongoni, ndicho kitokacho mdomoni. Hivyo, ukisoma visivyo na maana utazungumza visivyofaa. Lakini, ukisoma vitu vyenye maana, utaongea vitu vya busara. Jenga utamaduni wa kusoma, ubongo wako ni kama 'elastic' kadri unavyojaza vitu ndivyo hutanuka. Afya ya ubongo huletwa na kusoma. Kuna siri nyingi zimejificha kwenye vitabu. "Ukitaka kumficha mtu, weka ujumbe kwenye maandishi".

Wakatabahu
©KichwaKikuu.
 
Kazi njema
81gXf0Y5lsL.jpg
 
Back
Top Bottom