Hizi ndizo mbinu za mabingwa wa kusaliti

Hizi ndizo mbinu za mabingwa wa kusaliti

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
ccouple.jpg
USALITI ni jambo baya katika uhusiano. Usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja. Wanajiona wamewini pale ambapo wanasaliti na wenzi wao kutogundua kama wanasalitiwa.

Siku zote anayesaliti huwa anajiona mjanja kwamba, yeye anasaliti wakati mwenzake hasaliti. Kwa asilimia kubwa, wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao. Wanataka wao wasaliti lakini wapenzi wao wasithubutu kusaliti.

Kwa nini hawataki wenzi wao wasaliti? Eti wanaumia. Hakuna kitu kinachomchukiza mwanaume kama kusalitiwa. Kusaliti asaliti yeye, akisaliti mwenzake ni kosa la jinai. Anaona amedhalilishwa.

Anajisikia fedheha kwamba mpenzi wake amemuonaje? Amemchukuliaje? Hajakamilika idara gani? Anawaza sana. Anajiuliza jamii yote inayojua kitendo hicho inamtazamaje? Kwamba ni boya kiasi gani hadi anaibiwa kirahisi. Hana nguvu za kiume? Hana uwezo kifedha?

Hapo ndipo unapokuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenzi wake.

Marafiki zangu, watu wanauana kwa sababu ya usaliti. Kwa mwenye penzi la dhati, kamwe hawezi kuvumilia usaliti.

Nikirudi katika mada yangu kama inavyojieleza hapo juu, kuna viashiria mbalimbali ambavyo ukiviona kwa mwenzi wako basi ujue unasalitiwa. Vifuatavyo ndivyo viashiria vyenyewe:

KUTOPENDA KUCHIMBWA
Mara nyingi anayesaliti huwa hapendi kuchimbwa mambo kwa undani. Anahofu anaweza kuchanganya madawa. Hupenda mazungumzo mafupi na moja kwa moja. Hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimuuliza anayakwepa haraka na kutaka kukupeleka kwenye mazungumzo anayoyataka yeye.

Ukimuuliza kuhusu mipango yenu, ukimuuliza kuhusu mustakabali wa penzi lenu baadaye hukuondoa kwenye mstari na kukufanya usiwe na hamu ya kumuuliza mara mbilimbili.

HAPENDI UJUE RATIBA YAKE
Mara nyingi mtu ambaye ana lake jambo huwa hapendi ujue ratiba yake. Anataka usimzoee. Iwe anafanya maamuzi yake kulingana na yeye mwenyewe anavyojua. Ikitokea unaijua ratiba yake, atakuwa ni mtu wa kutoa udhuru kila wakati.

Leo atakwambia kuna mgonjwa anakwenda kumuona. Kesho atakwambia kuna vikao na wafanyakazi wenzake. Siku nyingine atakuambia gari imepata pacha, analazimika kusubiri mafundi hadi wafike ndio aweze kuanza safari ya kurudi nyumbani.

Ukiona mtu ana visingizio vingi, jua kwamba njia zake si salama. Hataki ujue nini anafanya kwa wakati fulani. Kwa ambaye hana makando kando, anaeleza ratiba yake kwa uwazi. Hata kama inatokea dharura, anaieleza na inaeleweka.

SIMU YAKE KITUO CHA POLISI
Anayesaliti mara nyingi hapendi kuacha simu yake kiholela. Simu inakaa mfukoni kwake hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo. Mpo nyumbani, mpo kwenye mazungumzo ya kifamilia yeye simu yake ipo mfukoni.

Imetolewa mlio. Hataki uione maana inawezekana akatumiwa ujumbe, picha na mambo mengine ya kimapenzi. Anayejiamini na yupo kwenye uhusiano imara, hana sababu ya kufichaficha simu yake. Anaiweka hadharani.

Mwingine atakusetia simu yake. Ukimpigia kila wakati inaonekana iko bize. Kila ukipiga inaonekana inatumika, kumbe yeye ndio anatumika wakati huo. Anakusaliti.

ANACHATI SANA
Wanaosaliti wengi wao hupenda kutumia meseji katika mawasiliano yao. Yani amewazoesha michepuko wake wote kusaliti. Hapendi kupokea sana simu. Zaidi anapenda kuchati hivyo ni rahisi kuwasiliana na mchepuko wake.

HAKUTAMBULISHI NDUGU, MARAFIKI
Msaliti anataka usiwajue watu wake wa karibu. Anahofia wanaweza kuvujisha taarifa bila hata kujua wanauza silaha. Kuepuka hilo, anataka umjue yeye na watu wake wachache.

Zaidi sana atakutambulisha kwa rafiki yake ambaye ni mchepukaji mwenzake. Wanajua namna ya kucheza michezo ya usaliti.

Usalitiwa kunauma. Kuepuka maafa ni vyema wapendanao wakawa waaminifu. Kila mmoja aheshimu hisia za mwenzake. Amtunzie heshima, awe na hofu kwamba akifanya hivyo anamuumiza mwenzake na kama ambavyo yeye ataumia akifanyiwa
 
Ninapenda kusema karma is true
"The force acting upward is equal to a force acting Downward clockwise and anticlockwise

every One is cheating
 
Kufanyiwa kitu ambacho Ww hufanyi inauma sana,..unakuwa na imani na mwenzio lakini yeye imani inamkosa,ni basi tuu...ndio maana wengine tunakuwa wapole tukiamini Mungu hamfichi mnafiki na njia ya mwongo fupi kuna siku utajua tuu mbivu na mbichi,.hapo ndipo utajua usuke au unyoe...

Usaliti sio jambo zuri hata kidogo,japo muosha huoshwa.
 
Umeleeza kwa hisia,yamewahi kukukuta?
 
Kufanyiwa kitu ambacho Ww hufanyi inauma sana,..unakuwa na imani na mwenzio lakini yeye imani inamkosa,ni basi tuu...ndio maana wengine tunakuwa wapole tukiamini Mungu hamfichi mnafiki na njia ya mwongo fupi kuna siku utajua tuu mbivu na mbichi,.hapo ndipo utajua usuke au unyoe...

Usaliti sio jambo zuri hata kidogo,japo muosha huoshwa.
Aliekuoa kafaidi sana.
 
Wewe unahitaji maombi haraka iwezekanavyo.
Baada ya hayo maombi nipongezwe pia kwa kuwa jasiri wa kusema hili

Nyinyi wanawake watu wa ajabu sana tusipojifunza mbinu mpya mnaleta uzi huku kutusema kuwa tukishaoa tunajisahau tunafanya kama mazoea sijui mbuzi kagoma kila siku tunawachosha

Acheni tukaongeze maujuzi tukirudi ndani mfurahi
 
Kuchepuka au kusaliti haipendezi hata kidogo...

Kwanza unaishi maisha ya wasi wasi kwamba hujui muda gani utafumaniwa...

Mambo yako ni ya vificho vificho... huna uhuru wala amani...

Cc: mahondaw
Kuchepuka au kusaliti haipendezi hata kidogo...

Kwanza unaishi maisha ya wasi wasi kwamba hujui muda gani utafumaniwa...

Mambo yako ni ya vificho vificho... huna uhuru wala amani...

Cc: mahondaw

kweli kabisa
 
Dah
Kuchepuka au kusaliti haipendezi hata kidogo...

Kwanza unaishi maisha ya wasi wasi kwamba hujui muda gani utafumaniwa...

Mambo yako ni ya vificho vificho... huna uhuru wala amani...

Cc: mahondaw
Kweli kabisa unaishi maisha kama nyumbu yaani......
 
Back
Top Bottom