Sikilizeni hii ya CCM:
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema kiasi cha asilimia 30 na 45 ya mapato ya madini ya dhahabu yanayochimbwa kwenye migodi mikubwa hubaki hapa nchini na si asilimia 3 kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa wanaosaka kuingia Ikulu kwa kuwahadaa wananchi.
Aliyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema, wawekezaji huchukua kati ya asilimia 55 na 70, na hiyo asilimia 97 inayodaiwa na upinzani ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kupotosha jamii.
Alisema kutokana na mfumo wa uendeshaji wa migodi uliopo, serikali imekuwa ikipata faida ya madini kutoka katika vyanzo vitano tofauti vya mapato na siyo aina moja ya asilimia tatu ya mrahaba ambayo hata hivyo imeongezeka kuanzia mwezi huu.
Alifafanua kuwa mrahaba huo ni moja ya vyanzo hivyo vya mapato vilivyomo katika mfumo wa kodi inayotozwa kwenye migodi ya dhahabu wakati madini ya vito kama almasi na tanzanite, hutozwa mrahaba wa asilimia 5.
Alivitaja vyanzo vingine vya mapato vinavyolipwa na migodi mikubwa ya madini kuwa ni pamoja na kodi ya mapato kwa asilimia 30, mapato kutokana na kodi ya zuio asilimia 10 na kodi ya zuio kwenye huduma za kitaalamu ambayo ni asilimia 5 kwa makampuni ya ndani na ya kigeni asilimia 15.
Aidha Ngeleja alisema michango ya hisani imekuwa ikitolewa na migodi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa maeneo yanayozunguka migodi ambayo sasa baada ya sheria mpya kuanza kutumika, ni asilimia 0.03 ya pato la uzalishaji wa mgodi ambapo awali walikuwa wakitoa dola 200,000 kwa halmashauri.
Waziri Ngeleja alisema migodi ya Geita (GGM) na Resolute wa Luthu wilayani Nzega, imekuwa ikilipa kodi hizo tangu mwaka 2008 huku mingine ikifanyiwa tathmini ili ianze kulipa kodi husika baada ya kuwa imerejesha mitaji.
Migodi itakayoanza kulipa kodi zote hivi karibuni baada ya tathmini ni pamoja na ile ya Buzwagi, Tulawaka, North Mara na Bulyankhulu inayomilikiwa na kampuni ya Barrick African Gold.
Source:Habari Leo
My take:Huo mrahaba wa 3% anaousemea WN unatosha?