aliisaac1000
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 407
- 272
Nilikua naangalia taarifa ya mkulu wa Air Tanzania aliyokua akiitoa juu ya wafanyakazi wa ATC. Kinachonihuzunisha si hatua zilizochukuliwa bali ni kauli ambazo zimeonekana kama kuwadhalilisha wafanyakazi ambao inakusudia kuwapumzisha. Hawa watumishi hawana kosa na waliajiriwa kwa kufuata taratibu zote hivyo wanastahili heshima hata kama ni kuwapumzisha basi lugha za kiungwana zitumike, lugha kama ' 'BODI IMEAMUA KUWAONDOA MARA MOJA' kama vile wanafukuza mwizi, ni lugha isiyo na staha na imejawa na chuki hata kama ilikua na nia nzuri. Ikumbukwe mara nyingi katika taasisi nyingi kama si zote zilizotumbuliwa si watumishi wa chini ambao wamehujumu, mara zote ni viongozi wakuu wateule wa Serikali yenyewe!, kwahiyo si vizuri kuwadhalilisha, walipeni haki zao waondoke kwa heshima.