Hizi kauli zina maana gani?

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,183
3,520
Salaam wakuu......
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26, nilipokuwa o' level nilipata msichana fulani hivi ambao ni miongoni mwa wale ambao wanakuwa na marafiki wakiume tu na sio wadada wenzao lakini mimi nilimweelewa kwa kuwa nilimwamini sana, unfortunate marafiki zao hao wengi huwa wanawatongoza basi kwa hili nilisikia Kuna jamaa anatoka nae ( japo yy alisema ni urafiki tu hakuna la ziada) basi niliamua kumfuatilia nikajua muda mwingi wako wote hata mida ya usiku wanaenda wote sokoni ,kwa hili niliumia sana na nilipojalibu kumwambia akasema sijiamini na hanitaki tena, niliumia sana mpaka kutoa machozi. Tangu hapo nilisema sitakuja kuwa na msichana yeyote mpaka nitakapo pata wangu nilipangiwa na mwenye Ezi Mungu.

MIAKA MITATU BAADAE;
Baada ya kujua nipo chuo kikuu na nakaa ghorofani kariakoo ( Maana matukio hapo juu ilikuwa mbeya mjini ) akaomba msamaha kwa namna zote zilizopo duniani na kuniambia " Anahitaji mtoto na anataka kuzaa na mie yupo tayari kunipa kila kitu ili mradi tu nimzalishe kwa sharti kwamba ,kwanza nimvishe pete ya u chum ba. Nilivyomsoma ni kwamba umri unamtupa mkono na hana mtu anayefikiria kuwa nae maishani aliyokuwa kuwa nao aliponitosa washasepa baada ya kufunua na kufunika.
N:B Ningemsamehe lakin kwa sasa sina mapenzi nae kabisa naogopa kumpotezea muda wake.

BACK TO THE HEADING ABOVE.
Baada ya matukio hayo ckutaka kabisa kuwa na mwanamke ,maisha ya chuo nilihitaji sana kuwa na msichana lkn nikiwaza changamoto zao narudi nyuma hasa ikizingatiwa CPENDI KABISA STRESS MAISHANI MWANGU. Nikiwa mwaka wa tatu UDSM pacha wangu aliniambia nimemtongoza neema zaidi ya mara tano na mara zote amekuwa akinitosa kavu kavu lakini nimeshangaa leo kaniambia nanukuu ," wewe unanipenda sijui unanitaka lakini mimi ckupendi wewe nampenda pacha wako , nilikuwa nampenda tangu utotoni lakini yeye kawa domo zege, " mwisho wa kunukuu.
Who is Ney?
Ni jirani yetu kule mbeya mjini , yeye na sisi tumekuwa pamoja na kucheza pamoja.
...................................
Baada kuambiwa vile na ndugu yangu nikampandia hewani na kunieleza kila kitu jinsi alivyonipenda tangu tukiwa shule za msingi ,aliniambia nanukuu" Nilikupenda sana na nilipenda bikra yangu uiondoe wewe, lakini ukajifanya uko busy na masomo mpaka wajanja wamewahi mzigo" daaah iliniuma sana na nilijilaumu sana kwa uwoga wangu. Baadae bila kujua ana mtu ama hana tukaanzisha mahusiano na tangu tumeanza mpaka sasa ni mwaka mmoja. Sasa ivi karibuni amekuwa na kauli tata mno ambazo zinanipa mawazo na kuamua kuja kuomba ushauri kwenu. Kwa mfano jana usiku wakati nachati nae kanitumia sms hizi:

1.Mzuri bongo ?au wazuri wameisha?

2.Hacha hizo zilipendwa bana ck hizi unalove kidogo tu.

3.Wewe mtu mzima kama kusoma hujui hata picha huoni.

Hizi sms zimenipa mawazo makubwa mno na ikizingatiwa mie muda huu nipo Mwanza Mana niliamishwa kikazi na yeye yupo Mbeya. Nishaurini wadau hayo maneno yana Maana gani ? Na mie nichukue hatua gani hapa nilipo am confused.
 
Ilikuwaje kuwaje mpaka akakutumia sms hiyo?na je ukimuomba papuch anasemaje?
 
Mkuu nadhani unachosubiri wewe ni kumuona live na boy mwingine....
Maaana hapo kilakitu kipo live unless mlikuwa mnajoke wakat mnachart
 
Kabla sijatoa ushauri, naomba kufahamu kwanza kama ulishampa mimba, maana lengo la kuwa na wewe lilikuwa umpe mimba.
Hapana cjampa mimba ,nilimtosa kabisa kwa sababu cna mapenzi nae.
 
Kabla ya kukushauri ningependa kujua msg yako uliyomtumia mpaka yeye akakujibu hivyo ndio tuendelee.
zilikuwa sms za kumsifia mno na kuonesha ni jinsi gani nampenda mno ,muda mwingi nafikiria yeye. Hapa ndo akaporomosha ile ya kwanza.
 
One thing for sure is, "She is not that into you". Pia keshazunguka sana na kufikia state ya Hakuna Jipya Chini ya Jua!
U should be happy because there are no signs of commitment which makes it fine to have fun.
Ila usiweke moyo wako hapo
Thank you mkuu
 
Back
Top Bottom