Slowly
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 10,486
- 34,789
Habari wakuu, kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na mweshimiwa kujichimbia Wilayani Chato Kwa muda sasa, maneno ni mengi, wengine wanadai kakimbia Corona wengine wanadai mzee kaenda kupumzika home kwao baada ya purukushani za kampeni n.k..
Naamini kila mkoa kuna Ikulu ndogo, sijajua kama kila wilaya ina Ikulu ndogo Ila naamini ipo, mheshimiwa amekuwa akipokea ugeni mzito huko Wilayani Chato, wengi wamepinga hatua hii kwa kile kinachodaiwa ugeni huu ulitakiwa ufanyike Ikulu ya DSM au Dodoma.
Sio mara ya Kwanza mheshimiwa kufanya jambo hili, nakumbuka wakati fulani Ikulu ndogo ya Kigoma ilitumika kumpokea Rais wa Burundi , na wakati fulani kule Tunduma kama sikosei Rais alifanya hivi pia kwa kiongozi mkubwa wa Zambia sijui wa Malawi sikumbuki vyema.
Kwa wenye uelewa watujuze, Kisheria hizi Ikulu ndogo zina mipaka ya kiutendaji kazi, au zinaweza zika-perfom kazi sawa na Ikulu Kubwa kutokana na maamuzi ya Rais.