Hizi Ikulu ndogo zilizopo kila mkoa kazi yake ni nini?

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,344
2,000
Habari wakuu, kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na mweshimiwa kujichimbia Wilayani Chato Kwa muda sasa, maneno ni mengi, wengine wanadai kakimbia Corona wengine wanadai mzee kaenda kupumzika home kwao baada ya purukushani za kampeni n.k..

Naamini kila mkoa kuna Ikulu ndogo, sijajua kama kila wilaya ina Ikulu ndogo Ila naamini ipo, mheshimiwa amekuwa akipokea ugeni mzito huko Wilayani Chato, wengi wamepinga hatua hii kwa kile kinachodaiwa ugeni huu ulitakiwa ufanyike Ikulu ya DSM au Dodoma.

Sio mara ya Kwanza mheshimiwa kufanya jambo hili, nakumbuka wakati fulani Ikulu ndogo ya Kigoma ilitumika kumpokea Rais wa Burundi , na wakati fulani kule Tunduma kama sikosei Rais alifanya hivi pia kwa kiongozi mkubwa wa Zambia sijui wa Malawi sikumbuki vyema.

Kwa wenye uelewa watujuze, Kisheria hizi Ikulu ndogo zina mipaka ya kiutendaji kazi, au zinaweza zika-perfom kazi sawa na Ikulu Kubwa kutokana na maamuzi ya Rais.
 

donbeny

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
3,538
2,000
Ikulu ni nyumbani kwa Rais aliye madarakani,karibu mikoa yote kuna Ikulu ndogo na kama hakuna huwa analala nyumbani kwa mkuu wa mkoa.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,344
2,000
Katiba haimzuii kufanya hivyo, wakifika Dar es Salaam, Dodoma au Tanga yote sawa tu. Hoja ya msingi ni majukumu yanatekelezeka kitaifa na aliapa kulitumikia taifa pasipo kubagua itikadi yoyote. YEYE NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Si huko huko chato ndo analitumikia taifa
 

Abigail Nabal

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
483
1,000
Mkiona watu wanakufa mfululizo halafu na yeye anakimbilia kijijini kwake unganisheni dot
corona is back

Lissu aliwaambia watz nchagueni ntakuwa faraja yenu kipindi kigumu.corona ikija sitawakimbia niende kujificha kijijini kwetu chato Bali ntabaki nanyi.
Si mnaukumbuka huu waraka wa lissu wakati anatangaza nia mkaanza kumtukana?

Yeye kikubwa yuko salama na kazi mnafanya kodi mnalipa amalize miradi yake basi.jiulizeni kwanini hata misiba haudhurii
Na siku ikija mpata itakuwa aibu kuu ya taifa.
 

MzeeMpya

JF-Expert Member
Dec 19, 2019
360
500
Tatizo la wengi wetu wanapenda kuwapangia viongozi wetu majukumu. Raisi anao mamlaka kamili kisheria na kikanuni kuwapokea wageni wake yote popote pale ndani ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

Mengine mabaya tunajitakia sisi wenyew. Tuache viongozi wetu wafanye majukumu yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom