- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Hivi karibuni kumekuwa na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha mtu akifungua kapsuli na kutoa vitu vinavyofanana na misumari midogo.
Kutokana na maudhui hayo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) nchini imeeleza kuwa Video hiyo imeandaliwa kwa lengo la kupotosha na kuzua hofu. Kufungua kapsuli na kuweka vitu vya kigeni ni mbinu inayotumiwa na watu wasio waaminifu kutengeneza maudhui ya kushtusha.
Dawa zote zinazoingia nchini hukaguliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA). Aidha, viwanda vya dawa vina mifumo ya mashine inayozalisha maelfu ya vidonge kwa dakika, na haiwezekani kitaalamu kwa msumali mmoja mmoja kuingizwa ndani ya kapsuli moja.
Iwapo kungekuwa na kitu kigumu kama msumali ndani ya kapsuli, mashine za kufunga dawa (blister packing) zingeharibika au kushindwa kufunga kidonge hicho vizuri.
TMDA inashauri Jamii kuendelea kutumia dawa kama tunayoelekezwa na wataalam wa afya na kuhakikisha kuwa tunanunua dawa kwenye sehemu za kutolea huduma ya dawa (Famasi au Duka la Dawa Muhimu) au sehemu za kutolea huduma ya tiba kama zahanati, kituo cha afya au hospitali iliyosajiliwa.