Hizi bia zenye jina la hifadhi zimechakachuliwa

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,274
Kiukweli Huwa nna machaguo 3 ya bia popote pale kwenye stuli ndefu ntakapokua, nikiiikosa bia namba moja,
basi ntaomba nipatiwe namba mbili, nikiiikosa namba mbili basi ntaomba nipatiwe bia namba 3. Cha muhimu moyo umwagiliwe, uelee, ufurahi na nifurahi na marafiki

Sasa Hii bia namba 3 ambayo jina lake ndo Lile la hifadhi yetu pendwa kivutio cha watalii, imenipa changamoto sana. Ijumaa kuna party nilienda na chaguo namba 3 ndiyo bia zilizokuepo kwa wingi(namba 1 na namba 2 hazikuepo kabisa), ikabd ninywe hivyo hivyo. Cha kushangaza ilikua na ladha ya uchungu sana, halafu ile hali ya upombe pombe(kulewa) nikawa naihisi kwa mbali sana tofauti na zamani. Nikahisi labda ni kwasababu muda mrefu sijainywa.

Kiukweli nilikunywa nyingi sana ila hata stimu la ulevi hamna kabisa. Ikabd niagize kitu kikali angalau nimix nijiskie nafuu na uchangamfu fulani mpaka mwisho wa party. Sasa Jumamosi tulikua tunavunja kamati, bia namba 3 ndo ilikuepo tena, nilivokunywa ladha ya uchungu ikaendelea kuwepo na kilevi kikawa kiko kwa mbali mno.

Nilivyo mshirikisha jamaa yangu wa karibu akanambia inawezekana uchungu ule unaletwa kwasababu nilikua nakunywa kwa pozi sana(bia ilikaa wazi sana), sababu ya zile ongea ongea na majukum kadhaa ya majadiliano ya kikao, ikapotezea.

Baada ya kuvunja kamati, kuna bia zilibaki, ikabidi tugawane kila mmoja abebe anazoweza akanywee nyumbani. Nikabeba bia 28 nikampelekea mwanamke wangu(mama J) jana Jumapili maana ndiyo bia zake zile anazokunywaga. Nilimkuta na shoga yake, wakasema bia zile hazitoshi, basi nikawaongezea kreti moja na kiti moto kilo 3.

Cha kushangaza,lLeo asubuhi nampitia kwake nakuta hata zile bia 28 watu wawili wameshindwa kuzimaliza(zimebaki bia 3) na kreti jipya liko vile vile. Nimewauliza tatizo nini, wanasema hizi bia hata hawazielewi,
zina ladha ya ajabu ya ajabu na hazichangamki mdomoni.

Wakuu, hii imekaaje? Hawa wenye kiwanda ndo wamelewa sifa wameamua kutuchakachua kupunguza ubora wake ili wapige faida kubwa? Au Kuna wahuni mitaani washaanza kuzifyatua? Au kuna hujuma zinafanyika huko wanakozalisha.

Kiukweli wanaohusika na hili wanapaswa waliangalie sana, vinginevyo hali Hii ikiendelea kwa bia hii itakuja kujifia kibudu kama ile bia yetu ya zamani yenye muungurumo wa simba ilivokua inatikisa miaka ile. Walipoichakachua tu, wanywaji wengi tukaisusa. Sasahivi naona imerud tena na wamejaribu kushusha bei siku hizi inauzwa 1,200 na wanywaji bado wamekua ni changamoto. Wanaohusika na hili waliangalie tafadhali.

Nawasilisha.
 
Itakuwa nyepesi tu, maana ndio inakimbiza sana sokoni sasa hivi

Ila nje ya mada. Mkuu saluti kwa shemeji, yaani mtu mbili shemeji na mwenzie ni beer 28 + 25 = 53 plus mdudu kilo 3!

Hiyo 'kapo' yenu si mchezo
Zile nyepesi kwasababu ni chupa ndogo zinaenda kirahisi.
 
Kumbe ni lite hapo sawa nikajua hizi lager ningeshangaa

Hivyo vilite wengine tunavionaga vichungu tangu mwanzo na hatujawahi kabisa kuvielewa

Beer ni lager tu yani safari, balimi, kilimanjaro, serengeti, and the likes hizo lite ni maji yaliyotiwa povu tu
 
Itakuwa nyepesi tu, maana ndio inakimbiza sana sokoni sasa hivi

Ila nje ya mada. Mkuu saluti kwa shemeji, yaani mtu mbili shemeji na mwenzie ni beer 28 + 25 = 53 plus mdudu kilo 3!

Hiyo 'kapo' yenu si mchezo
Kiwanda Cha kisukari kinatengenezwa hapo.
 
Huo ni ukwel kabisa..
Izi bia zenye jina la mbuga fulani ivi zimekua chungu sana,ilikua ndio bia yangu ila kwa sasa hapana..
Nmehamia kwenye zile zina jina la pembe za tembo, ila zile lite... asee ziko poa saana
 
Kiukweli Huwa nna machaguo 3 ya bia popote pale kwenye stuli ndefu ntakapokua, nikiiikosa bia namba moja,
basi ntaomba nipatiwe namba mbili, nikiiikosa namba mbili basi ntaomba nipatiwe bia namba 3. Cha muhimu moyo umwagiliwe, uelee, ufurahi na nifurahi na marafiki

Sasa Hii bia namba 3 ambayo jina lake ndo Lile la hifadhi yetu pendwa kivutio cha watalii, imenipa changamoto sana. Ijumaa kuna party nilienda na chaguo namba 3 ndiyo bia zilizokuepo kwa wingi(namba 1 na namba 2 hazikuepo kabisa), ikabd ninywe hivyo hivyo. Cha kushangaza ilikua na ladha ya uchungu sana, halafu ile hali ya upombe pombe(kulewa) nikawa naihisi kwa mbali sana tofauti na zamani. Nikahisi labda ni kwasababu muda mrefu sijainywa.

Kiukweli nilikunywa nyingi sana ila hata stimu la ulevi hamna kabisa. Ikabd niagize kitu kikali angalau nimix nijiskie nafuu na uchangamfu fulani mpaka mwisho wa party. Sasa Jumamosi tulikua tunavunja kamati, bia namba 3 ndo ilikuepo tena, nilivokunywa ladha ya uchungu ikaendelea kuwepo na kilevi kikawa kiko kwa mbali mno.

Nilivyo mshirikisha jamaa yangu wa karibu akanambia inawezekana uchungu ule unaletwa kwasababu nilikua nakunywa kwa pozi sana(bia ilikaa wazi sana), sababu ya zile ongea ongea na majukum kadhaa ya majadiliano ya kikao, ikapotezea.

Baada ya kuvunja kamati, kuna bia zilibaki, ikabidi tugawane kila mmoja abebe anazoweza akanywee nyumbani. Nikabeba bia 28 nikampelekea mwanamke wangu(mama J) jana Jumapili maana ndiyo bia zake zile anazokunywaga. Nilimkuta na shoga yake, wakasema bia zile hazitoshi, basi nikawaongezea kreti moja na kiti moto kilo 3.

Cha kushangaza,lLeo asubuhi nampitia kwake nakuta hata zile bia 28 watu wawili wameshindwa kuzimaliza(zimebaki bia 3) na kreti jipya liko vile vile. Nimewauliza tatizo nini, wanasema hizi bia hata hawazielewi,
zina ladha ya ajabu ya ajabu na hazichangamki mdomoni.

Wakuu, hii imekaaje? Hawa wenye kiwanda ndo wamelewa sifa wameamua kutuchakachua kupunguza ubora wake ili wapige faida kubwa? Au Kuna wahuni mitaani washaanza kuzifyatua? Au kuna hujuma zinafanyika huko wanakozalisha.

Kiukweli wanaohusika na hili wanapaswa waliangalie sana, vinginevyo hali Hii ikiendelea kwa bia hii itakuja kujifia kibudu kama ile bia yetu ya zamani yenye muungurumo wa simba ilivokua inatikisa miaka ile. Walipoichakachua tu, wanywaji wengi tukaisusa. Sasahivi naona imerud tena na wamejaribu kushusha bei siku hizi inauzwa 1,200 na wanywaji bado wamekua ni changamoto. Wanaohusika na hili waliangalie tafadhali.

Nawasilisha.
Hivi ndugu zangu walevi,hamjiulizi kwanini bia hazipandi bei !! Kila kitu kila mwaka,mwezi kinapanda bei. Hata hizo Heineken winhoek zote fake. Mnakunywa takataka . Hakuna bia yenyeladha ya bia saiv.
 
Back
Top Bottom