Hizbulah wabomoa kamera za Israel huku washirika wake wakizidi kukasirika

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,186
10,922
Israel imezidi kuonesha unyama wake na kibri kilichopitiliza ada kwa kukataa kufungua mpaka wa Rafah ili raia wa nchi rafiki zake waweze kuondoka Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri amesema malori mengi ya misaada ya kibinadamu yapo mpakani tayari kuingia Gaza na upande wao uko wazi kwa misaada hiyo kuendelea na safari,tatizo upande wa pili ndani ya Gaza ambako Israel ndiyo yenye mamlaka wamekataa kufungua mpaka.

Sambamba na hilo raia waliokushanyika kwa msongamano mkubwa wa kibinadamu upande huo wa kusini ya Gaza wameendelea kupigwa kwa mabomu ya kutoka angani huku wakiwa hawana maji ya kutosha,chakula wala umeme.

Upande wa kaskazini ya Israel kwenye mpaka na Lebanon wanamgambo wa Hizbulah wameziharibu kamera kadhaa za vituo vya kijeshi vya Israel ambazo kazi zao ni kuangalia harakati zote za kuvuka mpaka kutoka kusini ya Lebanon kuingia nchini humo.

Inavyoonekana kwa sasa Marekani imetishika sana na kiburi cha Israel ikiona kama kwamba itawaharibia maslahi yao pia.Hilo linaonekana katika nenda rudi ya wanadiplomasia wa Marekani kuzungumza na Israel kuhusiana na kiburi chake cha kujifanya hataki kumsikiliza yeyote.

Mshirika mwengine muhimu wa Marekani ambayo ni mlinzi wa Israel ni Saudi Arabia. Kuonesha kukasirika kwa mwanamfalme Mohammed Suleiman, alimuacha Antony Blinken kwenye ukumbi kwa masaa akimsubiri bila kutokea mpaka pale Blinken alipochoka na wala hakujitokeza kuzungumza naye ikabidi aondoke tu.
 
Tulieni mnachezewa mchezo mchafu na Israel, Hezbollah kundi dogo haliwezi kufanya chochote kwa Israel. Hata kipindi cha Entebe operation Israel wallijifanya kama wanashindwa kumbe ndo mbinu za kuovamia Uganda. Air supremacy ya Israel ni bira mara 10 kuliko ya Iran.
 
Iran kwanini asimfanye Israel, kama Japan alivyofanywa na USA. Huyu Israel mbona anaonyesha kibri cha hovyo sana. Ingekuwa ni uwezo wangu ningemfuta kabisa kwenye uso huu.
Iran Hana uwezo wa kumpiga Israel, level ya Israel katika medali za vita ni USA, Rusia, China, England kutokana na air supremacy take, level ya Iran ni Egypt, South Africa, Ukraine, Saudia Arabia
 
Tulieni mnachezewa mchezo mchafu na Israel, Hezbollah kundi dogo haliwezi kufanya chochote kwa Israel, . Hata kipindi Cha Entebe operation Israel wallijifanya kama wanashindwa kumbe ndo mbinu za kuovamia Uganda. Air supremacy ya Israel ni bira mara 10 kuliko ya Iran
Inaonekana hujapata habari za wapanda pikipiki 10 wa Hamas walivyozima technology supremacy ya Israel.

Baada ya hapo wenzao wakaanza kazi krusha makombora na matrekta kubomoa kuta za zege ndipo vigari vyao vidogo vikaingia nchi nzima walipotaka na huko juu mvua ya makombora ikazizidi nguvu Iron dome. Hakuna mwenye nguvu na supremacy ya kweli dunia hii ukiamuacha muumba mwenyewe.
 
Hezbollah kundi dogo haliwezi kufanya chochote kwa Israel,
Hezbollah is a proper match to IDF compared to Hamas.
Air supremacy ya Israel ni bira mara 10 kuliko ya Iran
Sema support ya US kwa Israel ni kubwa hata Tanzania ipewe trillion 10 kila mwaka za kununua silaha tungekua miles ahead.
Hata kipindi Cha Entebe operation Israel wallijifanya kama wanashindwa kumbe ndo mbinu za kuovamia Uganda
Vipi wakashindwa rescue mateka wa Munich? Na walikua wamestage mpaka Airport feki? Why utolee mfano wa inferior country kama Uganda unaacha superior kama Germany? Au unashindwa kuhoji kivpi Iron Dome waliodai inazuia mabomu iliruhusu rocket za Hamas zaidi ya elfu 5 kutua ndani ya Israel?

All in all tuombee amani tu kuonyeshana ubabe hakumsaidii yoyote. Walimtunishia misuli Hitler wakaishia kufa million 6!!
 
Hezbollah is a proper match to IDF compared to Hamas.

Sema support ya US kwa Israel ni kubwa hata Tanzania ipewe trillion 10 kila mwaka za kununua silaha tungekua miles ahead...
Jeuri ikizidi inafaa ukumbushwe kidogo kwmba duniani kuna jamii nyngi zenye haki sawa na ww tu....nchi za waarabu ilifaa wamstue kidogo tu Ili akae akijua hata kama una nguvu vp unaweza kutikiswa vilevile....na wakati ndio huu wa sasa
 
Sikulaum
Iran kwanini asimfanye Israel, kama Japan alivyofanywa na USA. Huyu Israel mbona anaonyesha kibri cha hovyo sana. Ingekuwa ni uwezo wangu ningemfuta kabisa kwenye uso huu.
Sikulaumu,ndo kipimo cha akili zako. Unaposema kufuta, ni miti unakata, ni maji unamwaga, au ni roho za watu unatoa uhai?
 
Haaahaaa ndio mnavyodanganyana vijiweni? Subiri siku US apunguze misaada uone kitakachotokea.
Hollywood imechota akili ya vijana wengi sana...plus na media za kimagharibi....na ukiangalia na elimu tunayopata hapa kwetu nayo kwa asilimia kubwa haitufanyi tuwe wadadisi wa mambo Bali ni kupokea vitu kama tunavyoambiwa na kuendelea na maisha...no room for inquisitivity kabisa
 
Jeuri ikizidi inafaa ukumbushwe kidogo kwmba duniani kuna jamii nyngi zenye haki sawa na ww tu....nchi za waarabu ilifaa wamstue kidogo tu Ili akae akijua hata kama una nguvu vp unaweza kutikiswa vilevile....na wakati ndio huu wa sasa
Musa a.s alimshinda Firauni kwa kupewa miujiza iliyoushinda uchawi mbele ya wafuasi wake aliowakushanya kwa fakhari.

Habari za teknolojia kubwa ya ulinzi ya Israel kila mtu aliiogopa japo haioni.Watoto wadogo wa Hamas wakaisoma na kuidukua halafu wakaizima yote kusini nzima ya Israel.
 
Back
Top Bottom