Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,128
- 8,058
"Hiyo hela itume kwenye namba hii mpya: +252 799 80090011, jina litakuja: Chaelmi Majuu. Simu yangu ya kawaida inadaiwa."
Ukipokea meseji zenye ujumbe kama huo, usikasirike, usimtukane aliyekutumia, wala usifanye haraka kum-block. Mhubiri Injili. Mwambie: "Je, kuna faida gani ukiyapata mapesa yote ya ulimwengu huu kisha uyapoteze maisha yako na kutupwa motoni milele?" (Rum 8:36-37). Au mwambie: "Waongo hawataurithi ufalme wa Mungu (Ufu 21:8). Tubu leo huo udanganyifu, uokoke halafu umuombe Mungu akupe kazi itakayokuingizia pesa halali." Au mwambie: "Mshahara wa dhambi ni mauti."(Warumi 6:23). Mkaribishe pia aje kanisani Jumapili.
Kuna Mkuu alisema: "Binadamu wote ni ndugu zangu..."
Kama tunakubaliana na kauli hiyo, kwanini tusiwape habari njema ndugu zetu tunaoona wazi kabisa kwamba watapotea milele?