Hivi wenzangu mnaishi vipi hapa mjini?

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,003
2,000
Wakuu habarini.

Mambo yanaendaje..

Wakuu awali ya yote natambua/mnatambua kuwa maisha ya mjini haswa ukiwa umepanga + ukiwa na watoto ni changamoto nzito.Hivyo inahitaji uchapakazi/utafutaji maisha yaende.

Wakuu jana asubuhi nikiwa naelekea kwenye harakati za utafutaji nikiangaza angaza macho huku na kule kuna wazee flani + vijana wamekaa kwenye kijiwe...nahisi walikuwa wakipata kahawa kama sio chai huku wakiendelea kuchambua hotuba ya juzi ya Mh Raisi.


Kilichonifanya mpaka nikaleta hii thread hapa niliporudi mida ya mchana... kwa sabbu nilipata emergence kidogo kuna kitu nilisahau....sasa ile kuangaza macho formation ni ile ile niliyoiacha asubuhi(wazee flani na kofia zao) huku wakicheza draft.


Ilinipa tafakari kidogo nikajiuliza hivi hawa jamaa hadi jioni watakuwepo?...Cha ajabu Ile niliporudi mida ya kumi na mbili hivi na alama formation ni ile ile,Ila nahisi kuna baadhi ambao ni wachache nahisi walipungua( japo formation ni ile ile) niliowakumbuka kuna wazee wanne hivi waliokuwa wamevalia kofia,rasi,big na wengine kama sita hiv.


Hao wazee wanne niliwamark toka asubuhi kwa sabbu ya kofia zao,ila hao wengine niliwamark mchana japo nahsi tangu asubuhi walikuwepo.


Ok.sasa wakuu lengo langu sio kutangaza life style ya mtu humu/kufuatilia na pia sitarajii kwa sabbu sipendi majungu + umbeya ila kwa sabbu humu ni jamii pana na hatutambuani nina imani may be kuna jinsi wenzetu wanarelax na maisha ilihali wengine tunasota.


Sasa Jee wanayaendesha vipi maisha ya hapa mjini? au wamewekeza? Na hata kama wamewekeza nahisi sio kwa idadi ile niliyo iona.
Wana nyumba zao+ za urithi wamepangisha.

Vile vile wengine madalali, na pia wake zao ndio wanaopambana kuuuza chakula usiku, na vitafunwa kama maandazi, mihogo, kalimati n.k
 

RtSleooz001z5ckjdNDt

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,862
2,000
Wana nyumba zao+ za urithi wamepangisha.

Vile vile wengine madalali, na pia wake zao ndio wanaopambana kuuuza chakula usiku, na vitafunwa kama maandazi, mihogo, kalimati n.k
Oooh sawa sawa..ndio maana asubuhi mpaka jioni wamejiachia.
Ok,Ahsante Mkuu ila kuna watu wanarizika mapema sana.

Ila Mkuu kwa upande wa pili kwa idadi niliyoiona nina wasiwasi sio wote wana nyumba za urithi kama unavyodai. Au unasemaje Chief
 

RtSleooz001z5ckjdNDt

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,862
2,000
Hata hapa jukwaani tuna soma, comments na ku-like 24/7...

Sasa sijui tunapataje bando na mambo mengine... Vipi hao wazee hapo mtaani walishakuja kuhemea kwako kwa kibaba cha Unga?
kiukweli hawajawahi.. na sitarajii

Ila Mkuu huo mkwanja wanautoa wapi? Isije ikawa nguvu za giza zinahusika.

Mtu anatoka asubuhi kwenda kijiweni jioni anarudi na mahitaji yote ya familia + mkate juu.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,003
2,000
Oooh sawa sawa..ndio maana asubuhi mpaka jioni wamejiachia.
Ok,Ahsante Mkuu ila kuna watu wanarizika mapema sana.

Ila Mkuu kwa upande wa pili kwa idadi niliyoiona nina wasiwasi sio wote wana nyumba za urithi kama unavyodai. Au unasemaje Chief
Mjini hapa mzee,

Wengine wana miamvuli yao ile mikubwa wanakodisha kwa siku 1,000 wengine wenye nyumba hata mbovu tu hapo Kariakoo wamazigeuza Godown, ukiuza mzigo wako ukibaki unaenda kuweka kwa siku buku.

Wengine wana maeneo, ukiwa na kieneo chako kikubwa kidogo unalaza magari na pikipiki.

Wengine walinzi, mchana stori nyingi usiku wanapotea.

Wengine ni wazee wa kuunganishia machinga wenye mabanda barabarani umeme. Ukiwa machinga na banda lako la mazaga akikuwekea taa, kwa siku buku.

Wengine wana utaalamu wao, labda kupaka rangi, ujenzi, umeme hivyo mara nyingi labda deal zinatiki mara moja wiki.

So, mishe ni nyingi huku town mzee🤣
 

RtSleooz001z5ckjdNDt

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,862
2,000
Maisha ya mjini ni rahisi sana. Ukishamiliki nyumba zako kadhaa, wewe ni kula tu mafao. Kodi miezi 3-6! Unapiga zako dili za udalali! Unakula cha juu, maisha yanaendelea.

Ole wako uwaige hao Maalwatan! Utalala na njaa.

Hahaha kweli kweli..au wapiga debe wa vituoni.

Ila Mkuu kwa idadi niliyoiona nahisi sio wote wenye hizo nyumba changanya na vijana juu niliowashuhudia.

yaan jamaa hana mishe yoyote anapiga patrol tuu ikifika jioni anarudi na mahitaji ya home..bado haingii akilini
 

RtSleooz001z5ckjdNDt

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,862
2,000
Mjini hapa mzee,

Wengine wana miamvuli yao ile mikubwa wanakodisha kwa siju 1,000

Wengine walinzi, mchana stori nyingi usiku wanapotea.

Wengine ni wazee wa kuunganishia machinga wenye mabanda barabarani umeme. Ukiwa machinga na banda lako la mazaga akikuwekea taa, kwa buku.

So, mishe ni nyingi huku town mzee

kwamba wengine ni walinzi mchana stori nyingi usiku wanapotea basi nimeanza kukuelewa Mkuu,kumbe kila mtu ana mishe zake.

Kumbe kila mtu ana muda wake wa kuteseka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom