Hivi wengine wanapata wapi ujasiri wa namna hii?

"Hiyo ndoa haiwezi kudumu"
Umekuwa Mungu ww?
Kudumu kwa ndoa hakutokani na aina ya harusi mnayofanyika.
Harusi ni sherehe ya siku moja. Ndoa ni mshikamano wa muda mrefu.
So wether watadumu au lah ,thats up to them na Mungu wao. Lakin harus na msiba havitohusika na ndoa huko mbeleni
 
Naamini hujawahi fiwa na mzazi ndiyo maana unasema hayo ngoja afe mzazi wako yeyote ndiyo utajua kuwa kifo siyo cha kufanyia dhihaka lakini pia kijamii haueleweki MSIBA NA NDOA NI MAJI NA MAFUTA HAVIKAI PAMOJA KWA NAMNA YEYOTE ILE TOKA KUUMBWA KWA DUNIA HAYO MAMBO YANAFANYIKA HATA SHETANI HAWEZI FANYA UPUMBAVU HUO SOMA BIBLIA, MSAHAFU NA HATA WAPAGANI HAWAJAWAHIFANYA UJINGA HUO NDOA NI JAMBO LA KUPANGA KIFO HAKIPANGIWI TAREHE LABDA NI MAIGIZO LAKI KAMA NI HALISI HAPO KUNA MAJANGA TUPU WALA HAKUNA NDOA TUSUBIRI TUKIJALIWA KUWEPO NA WATU WAKAANDIKA MTANISNIMULIA HUMU JF. INGIA YOU TUBE KUNA BI HARUSI ALITEKWA NA KUBAKWA SIKU YA NDOA YAKE NA BAADA YA KUPONA BWANA HARUSI ALIAMBIWA ASIMUOE YULE MAMA KWAKUWA NI ISHARA MBAYA AKALAZIMISHA ALIKAA NAYE KWA SIKU 27 TU AKAFA GHAFLA. KILA JAMBO LINALOTOKEA KWENYE MAISHA LINA UJUMBE MAALUMU
 
Unafunga ndoa, mwili wa mama yako uko nyuma ya jeneza, unasema dedication?
MKUU HUYO BHANGI ZINAMSUMBUA KAMA NI MKE WAKO MUNGU KAKUPA UKIAHIRISHA KUFUNGA NDOA NA HIVYO VYAKULA VIKATUMIKA MSIBANI NA UKAMZIKA MAMA YAKO KWA HESHIMA ZOTE UTAPUNGUKIWA NINI HATA HIVYO MSIBA NA NDOA HAVICHANGANYWI KAMWE.
 
Wange mourn kwanza msiba,hapo wameshaziniana wee
 
Huyu jamaa ni bonge la bahili.........maana alishapiga hesabu akaona maandalizi na vitu vyote alivyoandaa angekula hasara kubwa sana..........akaona bora iwe ivyo ivyo tu......maana msibani watu wanakula bure na kulewa pia........na harusini ni hivyo hivyo...... ndio maana gharama ingekuwa kubwa zaidi harusi ibume na watu washachanga na wabongo balaa hawana dogo ........nadhani ndicho alichokifanya
 
Jinsi Mama anavyouma, narudia tena Jinsi Mama anavyouma ....

Sitaki kuwahukumu, ila kwa upande wangu nisingeweza kabisa, Its a No Brainer ... hiyo takataka ya Ndoa naweza kufanya siku yeyote ila heshima na mazishi kwa Mama yanafanyika mara moja tuu maishani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bw harusi alisema hivi;

Najua kuna watu watanishangaa na wengine kuniona ni mpumbafu ninaepaswa kulaaniwa kwa tukio hili, lakini nataka kuwafafanulia kwamba nimefunga ndoa huku mwili wa marehemu mama yangu nao ukiwa humo humo kanisani ili mama yangu ashuhudie ndoa yangu ki roho, alinisisitiza kwa muda mrefu sana nifunge ndoa, pia nilipanga kwa siri siku hiyo ya ndoa yangu nimfanyie birthday yake bahati mbaya zaidi inakuwa death day..... Kwa nitakaokuwa nimewakwaza wanisamehe lakini mimi nimefanya lile nililoona sahihi.

Asanteni wote mliohudhuria.

Hayo ndio maneno ya bw harusi msimuhukumu bila kujua, Mc aliyeongoza sherehe ya Send off ni rafiki yangu na alinieleza yote yaliyojiri siku hiyo ukumbini
 
Sijaona Tatizo hapo,wameamua mama ashuhudie kile alichokuwa akikitamani kwa mwanae kabla hajaingia Kaburini.
Huo Upuuzi wa kusema laana nk ni upungufu wa fikra tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…