Hivi wazungu wanajua au kushiriki Uchawi?

Hivi wazungu wanajua au kushiriki Uchawi?

Mzee wa kurekebisha

Senior Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
178
Reaction score
170
Nimejiuliza sana hii kitu, naona kama wenzetu hawajui kabisa mambo ya Ulozi kwa sababu nayaona tu katika bara la Afrika na Asia. Wakuu naomba kufahamishwa ukweli bila kuhusisha Movie zao ambazo zimejaa uongo uongo tu.
 
Yes wanayajua lakini hayawapi tabu wao wamechukua yale mazuri yenye kujenga wanachukua idea za kichawi then wanazigeuza tija.Sisi tunachukua uchawi mbaya wa kutudhuru,wa kutukwamisha.All in all uchawi ni umasikini, hata watoto wa wachawi huwa wakishasoma na kuelimika ni nadra sana kuurithi.
 
Wazungu waliufuta uchawi zamani sana enzi za ukristu umeshika dola ulaya iliwekwa sheria ya kusaka na kuua Familia Zima ya mchawi
 
E84EDAD6-FA88-4352-A3CF-A600B7394721.jpeg
 
Duh, hii sijaipata mkuu.
We Google witch hunt or hammer of the witch papa alitoa order wachawi wote wauliwe kwa sababu ni anti-christ. Sasa njia za kumgundua mchawi ni zipi. Walikua wanaangalia chale yani kama hizi za kibongo wachawi wakizungu nazo walikua wanajichanja. Kingine wanakuzamisha majini usipozama wewe ni mchawi si unajua watu wametambika kuzuia kifo so uchawi wako unakufanya usizame na njia nyingine. Ukishagundulika mchawi ni wewe na Familia yako wote mnauliwa ili asitokee mrithi au mtu wa kulipa kisasi
 
Nimejiuliza sana hii kitu, naona kama wenzetu hawajui kabisa mambo ya Ulozi kwa sababu nayaona tu katika bara la Afrika na Asia. Wakuu naomba kufahamishwa ukweli bila kuhusisha Movie zao ambazo zimejaa uongo uongo tu.


Wazungu nao wana uchawi ila kuendelea kwao kumewasaidia kuutupa kando japo kuna wengine (wachache) bado wanafanya sana.
 
Ngoja nikujibu kwa mtindo huu wa enzi za utoto.

Tulikubaliana kua ugali haupo ulaya kwa sababu hakuna jina la kizungu kuutambulisha.

Hoja yetu ilikua kwamba kama ungekuepo lazima wangekua na jina la ugali.

Mashahidi wa Yehova ilikua ngumu kusambaza injili nchi fulani ya ndani ndani Amerika kusini kwakua walikua hawana ule mti aliotandikiwa Yesu akapita na punda hivyo hakukua na msamiati wa mti ule.

Kwa hoja hiyo ni kwamba, kwakua wana maneno ya kiingereza ya uchawi, ulozi, majini, nyumba kutembelewa na wafu naamini hivi vitu wanavyo.

Ngoja nile kwanza
 
Wazungu waliufuta uchawi zamani sana enzi za ukristu umeshika dola ulaya iliwekwa sheria ya kusaka na kuua Familia Zima ya mchawi
Sisi leo tukiwakata mapanga vile vibibi vya shinyanga wanasema haki za binadamu wazungu watu wa ajabu sana.
 
Sisi leo tukiwakata mapanga vile vibibi vya shinyanga wanasema haki za binadamu wazungu watu wa ajabu sana.
Msimu ulishapita Enzi hizo kulikua hakuna haki za binadamu now zipo kwahiyo kitu pekee cha kuondoa uchawi ni technologie maana kama hakuna wateja nani qtafanya uchawi
 
Kama mpaka wanatunga movie that means wanaamini uchawi upo
 
Kaangalie Series hizi,
Secret circle,
Witch hunter,
Salem,
The Originals,
Pia ask bwana google utapata jibu kamili tena uchawi wetu huu ni cha mtoto ndio maana hauna maendeleo yoyote wao ndio vigagula ila technology inawabeba.
 
1-Mzungu ni Nani au ni
Mtu anaetoka/tokea wapi hasa?

2-Uchawi ni kitu gani/Upi hasa?

3-Je, Tunaweza kusema kwa hakika kuwa 'WaTanzania' Ni wachawi au 'Si Wachawi'?

Tukiwekana Sawa katika hayo tutapata pakuanzia pazuri zaidi nadhani,
Maana Hoja yako ni ya Msingi na ina mapana yake pia.
 
Last edited:
Back
Top Bottom