Hivi wazungu huwa wanachangiana harusi?

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,542
Waafrika hatuwezi kuendelea hata iweje. Mtu akiwa na shida hachangiwi kabisa, hata akikosa ada ya shule hachangiwi,

Tangaza harusi uone watu wanavyoibuka kutaka sifa, mimi nitatoa mil moja, mimi laki 9, sisi ni watu wa ajabu kabisa.

Acheni tuteswe na umaskini.
 
Mazee usiwapangie watu jinsi ya kutumia fedha ambayo hujashirikiana nao kuipata.

Unajivunjia heshima wewe na kuwavunjia heshima wao.

Unajivunjia heshima wewe kwa sababu unakuwa mtu unayetaka kuweka maamuzi kwa kitu kisicho chako.

Unawavunjia heshima wao kwa sababu hujawapa heshima ya kuwaruhusu watumie hela zao wanavyotaka.
 
Did U hit ur head somewhere today? Uchangiwe kusomesha majukumu yako yatakuwa nini? Kupiga paipu tuu? Kwani unadhan Mungu aliposema Mwanaume utakula kwa jasho ulizani alimaanisha nini? Am ashamed of u! Change ur name yaani hapo ndio wisdom imekufikisha? After All kila watu na utamaduni wao! We are African braza kaka!
 
Miafrika hatuwezi kuendelea hata iweje.
Ujinga mtu umetujaa kichwani, na laana kubwa ,mtu akiwa na shida hachangiwi kabisa, hata akikosa Ada ya Shule hachangiwi, tangaza harusi uone mijitu inavyoibuka kutaka sifa, Mimi nitatoa mil moja ,Mimi laki 9,sisi na mijitu ya hovyo kabisa.
acheni tuteswe na umaskini shenzi zetu.
Hama nenda ulaya usilaumu watu kwa kukosa kwako pambana!
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia 100+. Haya ni mambo ya kizamani sana na hayana tija kabisa.
Leo hii kwenye familia hiyo hiyo kuna vijana wanamawazo ya biashara yanayohitaji 1 M lakini hawapati na ajira hawana lakini zainachangishwa hela kwajili ya jambo la hovyo tu halafu watu wanatetea tena kwa kummandi mleta hoja, kweli watanzania.....

Mbaya zaidi mtu usipomchangia unaona kabisa urafiki,undugu na ukaribu unavoyeyuka kana kwamba hilo lilikuwa jambo la maana sana kwake.

Harusi kwangu haziniumizi kichwa nilishaamua sichangi isipokuwa kwa mashart magumu sana. Niwe na taarifa miezi 6 kabla, awe mtu ambaye kisheria ni ngumu kumkwepa kwenye hilo jambo na mchango hautazidi 30k, vinginevyo sifa nyingi hizo habari za kulisha na kunywesha watu kwa siku moja huku nikiacha mambo ya msingi kabisa.

Serikali sijui inalala wapi hizi zinapaswa zitozwe kodi kabisa.
 
Mazee usiwapangie watu jinsi ya kutumia fedha ambayo hujashirikiana nao kuipata.

Unajivunjia heshima wewe na kuwavunjia heshima wao.

Unajivunjia heshima wewe kwa sababu unakuwa mtu unayetaka kuweka maamuzi kwa kitu kisicho chako.

Unawavunjia heshima wao kwa sababu hujawapa heshima ya kuwaruhusu watumie hela zao wanavyotaka.
Nilitarajia tu kujibiwa hivyo , haya kila la heri mweka hazina wa harusi ya Fikiri.
 
Gharama kubwa ya kwanza kwa wazungu ni mwanaume kununua engagement ring, baada ya hapo mwanamke akikubali ni kwenda kumwomba ridhaa baba wa bibi harusi kuwa unamoa mwanae. Upande wa mke na mume wote wanaweka budget ya harusi, wengine hii ni maharusi wenyewe.
 
Nilitarajia tu kujibiwa hivyo , haya kila la heri mweka hazina wa harusi ya Fikiri.

Fikiri ni nani?

Umeelewa nilichokuambia?

Usitolee macho hela za wenzako na jinsi wanavyozitumia, tafuta zako na amua unavyotaka kuzitumia.

Pilipili iko shamba inakuwashia nini?

Watu wakiamua kutupa pesa zao wewe tatizo lako nini? Kinachokuuma nini?

Ukiniambia hutaki watu wakuombe michango ya harusi nitakuelewa, una haki ya kukataa michango.

Ukilalamika watu wanachangiana harusi unaonekana unatolea macho hela za watu bila sababu.

Tafuta zako uzipangie matumizi, usiwapangie wenzako jinsi ya kutumia zao.
 
Sawa mweka hazina Nimekuelewa vizuri Sana, vp mmefikisha mil ngapi hadi sasa kwenye kamati? Na je kutakuwa na bia?
 
Sawa mweka hazina Nimekuelewa vizuri Sana, vp mmefikisha mil ngapi hadi sasa kwenye kamati? Na je kutakuwa na bia?
Hujajibu swali langu. Fikiri ni nani?

Unakandia kuchangishana harusi halafu unaulizia kama kutakuwa na bia? Unataka kudoea?

Sipendi kuchangishana harusi, hususan kwa watu wasio na uhusiano wa karibu sana, lakini sipendi kuwapangia watu jinsi ya kutumia hela zao zaidi.

Sijawahi kuwa mweka hazina wa harusi yeyote maishani yangu.

Naona unanichanganya na mtu mwingine.

Fikiri ni nani?
 
Mmh, kwaupandewangu naona sivbaya kuchangiana ktk sherehe za harusi, naningelipenda tuhamasishane kuchangiana kweneshida na matatzo mbalimbali pia niushikiano kiujumla mzuli xana,
 
Back
Top Bottom