Hivi wazungu huwa wanachangiana harusi?

Hivi wazungu huwa wanachangiana harusi?

Wanaoana wanasave kwa ajili ya harusi hata kukopa ikibidi, wenye wazazi poa wanawapa, hivyo ndio zaidi kwao.
 
Mazee usiwapangie watu jinsi ya kutumia fedha ambayo hujashirikiana nao kuipata.

Unajivunjia heshima wewe na kuwavunjia heshima wao.

Unajivunjia heshima wewe kwa sababu unakuwa mtu unayetaka kuweka maamuzi kwa kitu kisicho chako.

Unawavunjia heshima wao kwa sababu hujawapa heshima ya kuwaruhusu watumie hela zao wanavyotaka.
Kutafuta nitafute mwenyewe matumizi unipangie ....KHA ...Muambie awe mpole ...
 
Mtoa mada kwan hizo hela zinazochangwa ni zako? Kama hupendi kuchangia harusi acha usichange sio kitu cha lazima na wanaopenda kuchanga wacha wachangiane mwisho wa cku kila mtu anaishi maisha yake jins alivyojipangia.. Kuna wengine harusi hawachangii wala shida na hivo vitu unavyosema vya muhimu hawachangii vilevile so mi naona kuchanga au kutochanga ni uamuz wa mtu
 
Sisi African cjui nan aliyetuloga....hii nikama kutoa ela kwenye msiba wakati marehemu alipo kuwa mgonjwa ukumpa ata mia!!!!!!!!!![HASHTAG]#shameonus[/HASHTAG]
 
Miafrika hatuwezi kuendelea hata iweje.
Ujinga mtu umetujaa kichwani, na laana kubwa ,mtu akiwa na shida hachangiwi kabisa, hata akikosa Ada ya Shule hachangiwi, tangaza harusi uone mijitu inavyoibuka kutaka sifa, Mimi nitatoa mil moja ,Mimi laki 9,sisi na mijitu ya hovyo kabisa.
acheni tuteswe na umaskini shenzi zetu.
Inaonekana umesha changiwa sasa hutaki kuwachangia wenzako
 
Kutafuta nitafute mwenyewe matumizi unipangie ....KHA ...Muambie awe mpole ...
Kama ni kwa pesa zako za kutafuta unaweza fanya harusi hata angani lakini hapa haziongelewa pesa za kutafuta kwa njia ya kuwasumbua watu kwa michango harafu unakwenda kufanya uwekezaji kwenye harusi.

1) kama akina mimi sina hata mkokoteni, lakini kwenye harusi tunatenga milions kwaajili ya kukodi usafiri.

2) suti na gauni la bi harusi, best man& woman + brighter ni zaidi ya 2 milioni.
3) bi harusi saluni gharama inaweza fika laki 4 mpaka 5.
4) ukumbi
5) mapambo
6)
Ukute mwengine ndio kamaliza chuo hana hata ajira lakini anawekeza hela mingi kwenye harusi. Nyumba ya kupanga huku uswazi kwetu unafanya harusi ya 15m+.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ponda Mali kifo chaja
 
Did U hit ur head somewhere today? Uchangiwe kusomesha majukumu yako yatakuwa nini? Kupiga paipu tuu? Kwani unadhan Mungu aliposema Mwanaume utakula kwa jasho ulizani alimaanisha nini? Am ashamed of u! Change ur name yaani hapo ndio wisdom imekufikisha? After All kila watu na utamaduni wao! We are African braza kaka!

Husituweke waafrika wote kwenye kapu moja ,Kenya hatuna tabia za ajabu ajabu kama zenu hizo kila siku mnakesha vikao vya harusi na mziki.
Mleta mada ana akili sana,wengi wenu mgalikuwa kama yeye leo hii na ardhi kubwa yenye rutba tele pamoja na madini na malighafi yote mlionayo mgelikua matajiri Afrika Mashariki na Kati.
Kumsomesha mtoto mmoja tu aje awe tabibu ,mhandisi ama hata kiongozi ni maendeleo makubwa sana katika jamii hususan za kimasikini .
Waweza kuishi na mkeo/mmeo kwa furaha na mafanikio siku zote za maisha yenu bila hivyo vijitamasha vyenu vya harusi sijui miziki na hafla.
Ni tabia mlioambukizwa na waarabu.
 
Fikiri ni nani?

Umeelewa nilichokuambia?

Usitolee macho hela za wenzako na jinsi wanavyozitumia, tafuta zako na amua unavyotaka kuzitumia.

Pilipili iko shamba inakuwashia nini?

Watu wakiamua kutupa pesa zao wewe tatizo lako nini? Kinachokuuma nini?

Ukiniambia hutaki watu wakuombe michango ya harusi nitakuelewa, una haki ya kukataa michango.

Ukilalamika watu wanachangiana harusi unaonekana unatolea macho hela za watu bila sababu.

Tafuta zako uzipangie matumizi, usiwapangie wenzako jinsi ya kutumia zao.

Hapangekua na haja ya kukaa vikao vya michango ikiwa wangalitumia pesa zao wenyewe kama bwana na bi harusi, ina maana wanatumia pesa za wengine/jamii kwa kuwashurutisha kuchangisha.
 
Husituweke waafrika wote kwenye kapu moja ,Kenya hatuna tabia za ajabu ajabu kama zenu hizo kila siku mnakesha vikao vya harusi na mziki.
Mleta mada ana akili sana,wengi wenu mgalikuwa kama yeye leo hii na ardhi kubwa yenye rutba tele pamoja na madini na malighafi yote mlionayo mgelikua matajiri Afrika Mashariki na Kati.
Kumsomesha mtoto mmoja tu aje awe tabibu ,mhandisi ama hata kiongozi ni maendeleo makubwa sana katika jamii hususan za kimasikini .
Waweza kuishi na mkeo/mmeo kwa furaha na mafanikio siku zote za maisha yenu bila hivyo vijitamasha vyenu vya harusi sijui miziki na hafla.
Ni tabia mlioambukizwa na waarabu.
despite of the things u have mentioned tushawahi kuwagongea kuomba msaada wa chakula au ardhi? Nyie ndio kila kukicha mwamiminika kwetu kutafuta maisha! Kuchangiana twachangiana sababu umoja & Upendo ndio hulka yetu! Nyie mnaoishi kizungu mbona mnashida kama sisi tu? Tumieni uzungu wenu na ukauzu wenu kumalizana na alshababu mkimaliza uje utu-critisize!
 
Kwenye harusi huchangiwi wewe... watu wanachangia ili waje kula na kunywa... Shida ni zako peke yako...
 
Miafrika hatuwezi kuendelea hata iweje. Ujinga mtu umetujaa kichwani, na laana kubwa, mtu akiwa na shida hachangiwi kabisa, hata akikosa ada ya shule hachangiwi, tangaza harusi uone mijitu inavyoibuka kutaka sifa, mimi nitatoa mil moja, mimi laki 9, sisi na mijitu ya hovyo kabisa.

Acheni tuteswe na umaskini shenzi zetu.
"Mtu mweusi ni kiumbe hatari sana,kuwahi kutokea..!"
 
Hapa ndipo waafrika hatuwezi kubadilika kamwe, labda mambo ya kijamaa yalituathiri ndio maana hata familia yangu ni ya mama yangu, wakwe zangu, shemeji zangu etc.

Ukitaka kulinganisha lifestyles unaweza kuwehuka, mengi tu tunafanya lakini hayana mantiki katika maisha.

Just live and let live.
 
Hapangekua na haja ya kukaa vikao vya michango ikiwa wangalitumia pesa zao wenyewe kama bwana na bi harusi, ina maana wanatumia pesa za wengine/jamii kwa kuwashurutisha kuchangisha.
Sawa.

Kwani wamekulazimisha?

Kama wanatumia pesa za wengine, na wote wanakubaliana, wanaochangiwa na wanaochanga wamekubaliana, na wewe hawajakulazimisha kuchangia, wewe tatizo lako linaanzia wapi?

Kuna mshkaji anaitwa Martin, alifanya harusi yake "kizungu", akasema hatahitaji mchango.

Watu wakaona amejikweza na kujifanya hahitaji kushirikiana na jamii katika kufanikisha mambo yake, wakanung'unika.

Akasema mkitaka kunichangia harusi, msichangie harusi, pelekeni mchango kwenye shule fulani inayohitaji msaada huko umasaini.

Wabongo bado wakamuona kawatenga kwa sababu hakuwapa nafasi ya kuchangia harusi yake.

Binafsi sifagilii michango ya harusi, hususan kama inahusisha watu wengi na wa mbali, kwa sababu inawapa mzigo mkubwa bila ya ulazima. Michango labda iwe kwa watu wa ndani kabisa wa familia kama kaka na dada.

Lakini Watanzania tatizo letu wengi ni unafiki.

Mtu anakuja hapa JF anakandia michango halafu akiombwa michango anaona haya na kutoa hela.

Mimi sioni sawa kuchangisha watu harusi, sijawahi kuchangisha na sitakuja kuchangisha, hata familia yangu. Lakini watu wakikubaliana wenyewe wachangishane, mimi sijioni kama nina haki ya kuwasema.

Kanuni ya msingi hapa ni kile Waswahili wanachosema "Cha Mtu Mavi".

Usikikodolee macho wala kukipigia kelele.

Maadam mtu kashapata hela zake kwa jitihada zake, huna haki ya kumpangia atazitumiaje, ili muradi hajavunja sharia.

Ukianza kumsema mtu kwa kuwa kachangia harusi wakati hujachuma naye hiyo hela hujamtendea haki huyo mtu wala hujajitendea haki wewe mwenyewe kama mtu anayefikiri.

Unapata wapi nguvu ya kumpangia mtu mwingine aliyepata hela yake kihalali jinsi ya kuitumia hela hiyo?
 
Husituweke waafrika wote kwenye kapu moja ,Kenya hatuna tabia za ajabu ajabu kama zenu hizo kila siku mnakesha vikao vya harusi na mziki.
Mleta mada ana akili sana,wengi wenu mgalikuwa kama yeye leo hii na ardhi kubwa yenye rutba tele pamoja na madini na malighafi yote mlionayo mgelikua matajiri Afrika Mashariki na Kati.
Kumsomesha mtoto mmoja tu aje awe tabibu ,mhandisi ama hata kiongozi ni maendeleo makubwa sana katika jamii hususan za kimasikini .
Waweza kuishi na mkeo/mmeo kwa furaha na mafanikio siku zote za maisha yenu bila hivyo vijitamasha vyenu vya harusi sijui miziki na hafla.
Ni tabia mlioambukizwa na waarabu.
Joo umesema kweli(in Kenyan voice)
 
Back
Top Bottom