Hivi watawala wetu kweli "zimo"... (Angalia video) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi watawala wetu kweli "zimo"... (Angalia video)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 28, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Silaha haramu zaidi ya 5000 zimechomwa moto kwenye uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Morogoro. Lakini kuna mambo mengine yanashangaza kama yamefanywa na watu wenye akili kichwani au la. Angala video na ujiulize maswali ambayo nimejiuliza mimi. Angalia halafu sikiliza.....

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji

  Hii nchi imejaa watu wazembe sana. Yaani wanakamata silaha halafu hawazikagui kama zina risasi au la. Huwezi kuchoma moto bunduki zenye risasi ndani unaweza kusababisha maafa makubwa. Yaleyale ya mabomu ya mbagala.
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Moja ya mambo ya ajabu nililoona ni bango, linalosema kwamba "uzagaaji wa silaha haramu unakwamisha maendeleo"!

  Pili hii haikupaswa kuwa ni moja ya "news headlines" ila ingewekwa kwenye "the rest of the news".

  Tatu nina wasiwasi kama zimo kwa kuzingatia kwamba watu wameenda "Japanese Embassy" kuomba pesa au ushauri wa jinsi ya kuteketeza silaha.

  Ila nafikiri kwamba kuna mtu anatafuta umaarufu kwa nguvu sana.
   
 4. A

  Audax JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  c hao ma rpc? ina maana na usalama wetu upo mikononi mwa nchi za nje? ,aana wamewapa uhuru wa kuchoma silaha.ina maana sisi hatuna uwezo wa kuziteketeza wenyewe?
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mmmh, sifahamu hasa ni nini ambacho mwanakijiji umekiona, lakini kilichonikera mimi hapo ni ile kwamba mpango wa kuteketeza hizo slaha umewezeshwa na serikali ya Japan. Its too funny to hear it. Hivi kumwagia mafuta na kuchoma moto kulihitaji hadi Japan itoe msaada? Imetoa msaada wa mafuta ya kuchomea, kiberiti au ukamataji wa hizo silaha? Just curious!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi mojawapo ya risasi ingeruka kumuumiza mtu hapo uwanjani wangempeleka Hospitali?
   
 7. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Moja ya mambo yanayosumbua Polisi wa nchi zilizoendelea ni matumizi ya silaha kwa vijana wadogo ambazo hupelekea upoteaji wa maisha kwa raia wasio na hatia.

  UK kwa mfano wana operesheni ambayo wanaiita Trident yaani inahusu "black on black crime". Hivyo huwa wanatoa "Amnesty" watu wasalimishe silaha hizo katika vituo mbalimbali vya polisi na baada ya hapo silaha hizo zikiwemo bunduki, pistol na vingine vinakusanywa na kupelekwa maabara.

  Pale huangaliwa moja baada ya ingine huku risasi zikitolewa na kila kitu kuwa "well documented". Pia kila silaha itajulikana inapotoka kwa kuangalia serial number, kama ni Russia, Afghanstan au Balkan states au hata kwa arms dealers.

  Silaha zingine zisizo za kawaida huwezwa kutumika kwa mambo kama mafunzo, kuwekwa makumbusho na hata kuwa "recycled".

  Zingine kama zitakuwa haziitajiki basi zitateketezwa kwa usalama na bila ya risasi ndani.

  Jambo la kuchoma silaha mchana kweupe tena zikiwa na silaha ndani ni jambo lisilo na mpangilio kabisa.
   
 8. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh...hizi silaha zimechomwa na risasi ndani?!! Hii inaonyesha polisi wamezipokea [hawakuzikagua na kutoa risasi], walizihifadhi [bila kutoa risasi] na wazisafirisha kufika hapo uwanjani [bila kutoa risasi], hatimaye zimechomwa moto [bila kutoa risasi.]??!!!

  Halafu tunakaa humu bodini kumlaumu JK kila kukicha..!!!
   
 9. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MM nimesikia kuwa hii ni mara ya 10 silaha haramu zinatekezwa. Je unafahamu mara tisa waliziteketezaje? Huenda wamefanya vilevile mara tisa zilizopia. Inawezekana tafsiri yao katika uteketezaji risasi nazo ni silaha haramu. Kwa hiyo silaha zinateketezwa pamoja na risasi zake. Labda ITV watafuatilia suala hilo kujua kwa nini imefanyika namna ile. Kinachonishangaza zaidi ni kwa nini tunahitaji msaada wa kuteketeza silaha wakati kuna jeshi la wananchi ambalo linauwezo wa kutegua hata mabomu?. Wanashindwaje kuwatumia wanajeshi hata kama polisi hawana uwezo wa kuteketeza?
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sioni kama hilo ni tatizo kubwa? Kwani kulikuwa na sababu gani ya silaha zote kugeuziwa juu? Unataka kusema kwamba wamefanya hivyo kwa bahati mbaya? Kama wamefanya kusudi unafikiri hawakuchukua tahadhari? Ukumbuke palikuwa na balozi pale. Halafu kulikuwa na sababu gani ya kutengeneza kile kijukwaa cha kuzipanga zile silaha? Naamini kulikuwa na namna ya kuzishikiza. Hapa shida kubwa ni kwanini japani watusaidie kuchoma silaha?
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii Nchi bwana, kila sehemu kuna uzembe, na uzembe huu wa kuacha risasi ni sawa na kusudio la kuua, rejea mafunzo yetu yale yale ya JKT wakati ule, kumwelekezea mwenzio mtutu hata kama hakuna risasi ni kosa kubwa sana, sembuse hili la kuchoma silaha na risasi zake. mkuu wa kitengo hiki anahitajika kujiuzulu/kuchukuliwa hatua za kijeshi.
  Halafu hivi kweli kuangamiza silaha tunahitaji utaalamu wa Japan? na umetusaidia nini kama bado risasi zimeachwa ndani
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndo inayoitwa accountability and responsibility
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  una uhakika gani kuwa wakati zinaungua zisingeweza kujiachia na kuangukia upande wowote na risasi? ila unaweza kuwa sahihi.. as long as wamegeuzia juu hawana haja ya kuzitoa risasi ndani.
   
 14. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Kwanini JK asilaumiwe? yeye ni lazima alaumiwe kwani ndiye anayemteua mkuu wa jeshi hilo (IGP). Na kwa kushindwa kumuadabisha yule aliyemteua yeye na kumpa dhamana kubwa ya kuongoza jeshi la polisi ni lazima watz tumshangae na kumlaumu daima, and one day he will pay for his negligence.
   
 15. DaMie

  DaMie JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 686
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je silaha hizo zilikuwa hazifai kwa matumizi katika jeshi letu?
   
 16. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimefaidika na clips za ziada kama ya kina Joti. inakuwaje nikitaka kuhamishia kwenye DVD kutoka YouTube?
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji umeenda US zamani sana. Ungekuwepo hapa nyumbani nadhani ungekuwa unalia kila siku, kuna mambo mengi yanafanyika hapa Tanzania ambayo ni typical style of episodes likes those in Gods must be crazy. Ukifikiria sana kuhusu Tanzania unaweza kufa, you are better ukiwa na mentality ya "ndivyo tulivyo". This says it all.
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Wakuu,

  Tunaweza vipi kumlaumu Rais wakati ambapo kama Taifa tumejijengea utamaduni wa kutokutumia akili na maarifa kwenye utendaji wa kazi zetu??!!

  Hivi kweli tuna amini hizi nchi za wenzetu ziliendelea kwa sababu walimpata Rais "Super Human"?

  Maendeleo na mabadiliko ya kweli yanakuja kutoka chini kwenda juu; kamwe sio vinginevyo. Angalia historia, kuanzia wakina Mkwawa, Churchil mpaka leo kina Obama.

  Tumekubali wenyewe mfumo mbovu...wala tusitegemee miujiza.
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  viongozi mbumbumbu hawana muda wa kufikiri hayo..we unashangaa kuomba mafuta ya taa hawa wameenda kuomba mkopo stanbic kuendesha budget sasa hii ni serikali au takataka
   
Loading...