Hivi walimu tumemkosea nini Mungu?

Hivi walimu tumemkosea nini Mungu?

Mamy K

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
3,166
Reaction score
11,160
Yani hadi najuta kusomea hii kazi, kila mtu bosi wako. Akija mzazi anataka akupige, Mkuu wa shule akupige mikwara, Afisa Elimu akutishe, Mkuu wa Mkoa akuogopeshe, jamani hadi lini.

Yani hadi unaweza kukufuru kuzaliwa katika familia masikini, bila umasikini wa familia yangu nisingesomea huu upumbavu.

That time nilivutika kusomea kwa sababu ya mkopo na jinsi Al habiby Jakaya M Kikwete alivyokuwa anawatreat walimu, ila kwa sasa najuta, najuta.

Mungu, sisi binadamu tunakosea, hatujakamilika, usituadhibu kwa mateso haya, nakuomba tuondolee haya mateso, wewe Mungu unajua utayaondoaje, kwako hakuna linaloshindikana.
 
Mkuu yule aliepoteza fahamu kwenye mkutano kule (mbinguni) kwani alikuw mwalimu?
 
Andika barua yako ya malalamiko uipeleke kwa mwalimu wa kemia pale getini magogoni.

Nasikia na mkewe pia alikuwa mwalimu kabla ya kuingia jumba jeupe.

Huenda wakakusikia, maama wanajua machungu ya waalimu.
 
Mada yako ina gusa sana, ningekuwa mtu mwenye mamlaka sector hiyo basi, leo ingekuwa mwisho wa vilio vya walimu
 
Mamy K,ukitaka kuifurahia kazi hii jiamini,tekeleza majukumu yako kwa wakati pia
Ukija huku kanda ya ziwa kuna sehemu panaitwa Bulima,huwezi fanya kazi kama ukiwa na roho nyepesi,majungu kutoka kwenye kamati ya shule,staff,mwenyekiti wa kijiji,vitongoji,Veo,Diwani na mwenyekiti wa chama cha...!
 
Ningekuomba usimlaumu Mwenyezi Mungu katika hizi fujo zetu tufanyazo duniani.Haya ni matokeo ya matendo ya mikono yetu.Mwanadamu kaonyeshwa na Mola wake njia ya kupita lakini kaikataa na kwenda anakotaka,sasa hapa Mwenyezi Mungu alaumiwe kwa lipi?
 
Unakosea sana Mamy K!!!! Mungu gani unayemzungumzia hapa? Mana umemtaja Jakaya Kikwete kisha mwanzo aliwa treat vizuri Kama binadamu halafu unahama unaleta lawama kwa Mungu tena bila kutambua kwamba kama JK aliweza kuwa treat vizuri kama binadamu basi kunabinadamu ambaye kwasasa hafanyi nafasi yake sawa na silawama kwa Mungu... Lawama ni kwa kiongozi mkuu wa Malaika ajaye aka Jiwe
 
Pole sana.
Thread yako unanikumbusha yule mwanasheria wa Kenya alichosema juzi. Hakukosea hata kidogo
26/4
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom