Buku 7 at workWasalaam wanaJF,
Kwa bahati nzuri nimefanikiwa kufuatilia mchakato wa kutafuta wagombea/ wawakilishi wa nafasi mbalimbali kwenye vyama mbalimbali kwaajili ya kupeperusha bendera za vyama vyao kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2020.
Kiukweli na uwazi ni dhahiri kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejitanabaisha na kujipamba sawia katika wagombea wake kuanzia ngazi za udiwani kwani katika vitu vyote walivyofanya kwenye mchakato huu kumewajengea jina watu wanaoenda kuwa wagombea wao na katika duru za siasa umaarufu ni mtaji mkubwa kwenye kutengeneza wapiga kura kitu ambacho vyama vya upinzani Tanzania havijatilia mkazo katika hili.
Kitu cha pili ni mpango mkakati, Vyama vya upinzani Kwa mfano Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) nguvu kubwa wamewekeza kwa wagombea wa nafasi za uraisi! Sasa najiuliza mgombea wa Chadema akishinda nafasi hii ya uraisi ataongoza Serikali ya namna gani? Je, atadumu kwenye kiti ya uraisi hata kwa mwaka mmoja?
Kwanini vyama vya upinzani haviwekezi nguvu kwenye kutafuta wabunge na madiwani ili kupata wawakilishi wengi kwenye mabaraza na Bunge? Leo hii asilimia kubwa ya wabunge wa upinzani ni matokeo ya M4C na movements mbalimbali Kwanini wametelekeza mkakati huu. Hivi wakiamua kusimamisha wagombea 200 wa uhakika na kuachana na Urais walau kwa kipindi kimoja na kulishika Bunge kisawasawa hawaoni watajenga zaidi nafasi yao?
Uhitaji kutumia nguvu kubwa kuona kuwa CCM itapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huu ujao na si kwasababu za kufichika hapana bali CCM wamejiandaa vizuri kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vingine vya siasa.
Naomba kuwasilisha