mambo_safi
Senior Member
- Jul 22, 2019
- 147
- 391
Nimezaliwa na kulelewa Bukoba mpaka nilipoanza kidato cha kwanza ndo kama nilihama mkoa wangu mpaka sasa umri unasoma kula chumvi nyingi.
Tangu miaka hiyo sijawahi kukutana na vyakula hivi vya asili kwa majina ya kihaya vinaitwa:
"Amakongo"
"Ebira"
"Ebira ebilikweera"
"Amasoma"
"Enumbu"
AMAKONGO ni jamii kama mihogo vile lakini yenyewe ni mviringo na mmea wake unatambaa chini au juu kama utapata mahali pa kujishikiza. Ukiyapika yanakuwa magumu kiasi kwamba ukiwa unayatafuna yanalia kama muhogo mbichi.
EBIRA: vyenyewe ni vikubwa kama papai jamii ya mihogo na mmea wake unatambaa chini au juu kama utapata mahali pa kujishikiza. Ukiyapika yanakuwa malaini na yanakuwa na rangi rangi fulani hivi.
EBIRA Ebilikwela ni jamii moja ya Ebira isipokuwa hivi ni vyeupee na vinanukia nukia vizuri saana ukivipika mtaa wa pili lazima wanuse
AMASOMA tofauti na jamii hizo tatu juu ambazo ukulia ardhini jamii hii utokeza kwenye mmea juu ya ardhi na mmea huu utambaa ardhini au juu ya ardhi ukipata pa kujishikiza
ENUMBU ni jamii kama tangawizi mwonekano na kuzaliana kwake lakini zenyewe nyeupe na zikipikwa msosi mmoja matata.
Ebu wajuzi na wenyeji wa Bukoba tuelimishe tafadhari!