Hivi vitanda vina ubora?

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
175
618
Hakuna asiyependa kwenda na wakati,ivi vitanda ndo habari ya mjini saizi lakini je Vina ubora? kama sofa ukiinunua tu baada ya miaka mitatu minne kitambaa kinaanza kupauka na kufifia rangi yake na kama una sofa ya laiza pia kitambaa kinatoboka na kufubaa yaani mng'ao unapotea.sasa swali langu je ivi vitanda vya sofa vina ubora gani? na kama hamtojali tupia picha yenye kitanda kizuri na sofa, wengine tunataka tuanze maisha na vitu vyenye ubora sio kila siku unanunua kitu kile kile.

Screenshot_20231121-045416_1700531717022.jpg
 
Hakuna asiyependa kwenda na wakati,ivi vitanda ndo habari ya mjini saizi lakini je Vinaubora? kama sofa ukiinunua tu baada ya miaka mitatu minne kitambaa kinaanza kupauka na kufifia rangi yake na kama una sofa ya laiza pia kitambaa kinatoboka na kufubaa yaani mng'ao unapotea.sasa swali langu je ivi vitanda vina ubora gani? na kama hamtojali tupia picha yenye kitanda kizuri na sofa, wengine tunataka tuanze maisha na vitu vyenye ubora sio kila siku unanunua kitu kile kile.
Kwani wewe unacho taka ni urembo, kudumu au ubora? Vyote huwezi kuvipata kwa kitanda kimoja, Kama wataka cha kuka miaka 20 hadi 50 nunua cha chuma tena bei iko chini hivyo vya urembo achana navyo kabisa......
 
Kwani ubora kwako ni nini? Uzuri, uimara, au kudumu maana lazima ujue unchotaka ndio ujue unanunua nini, chuma ni durable ila hakitakupa muonekno nzurii, mbao kama mpingo ambayo ni ngumu na itaishi maisha marefu haifai kwasabbu hata msumeno hauwezi kukata vizuri mbao yake, miti mingine kama mninga, mtiki, mvule au mkongo na yakufanana na iyo inauzwa ghali sana kitanda chake si mchezo kununua labda uibe mbao ukampe fundi ila ukidakwa ni juyako.

Sofa na mbao laini ndo option ya kitanda cheap lakini vinapewa muonekano mzuri vinadumu kwa muda mfupi , na tafadhali usiwe mchafu na sofa bed kunguni watakuua. Kwa maelezo hayo nafikiri tafakari ubora kwako unaangalia nini then the choice is yours
 
Hakuna asiyependa kwenda na wakati,ivi vitanda ndo habari ya mjini saizi lakini je Vinaubora? kama sofa ukiinunua tu baada ya miaka mitatu minne kitambaa kinaanza kupauka na kufifia rangi yake na kama una sofa ya laiza pia kitambaa kinatoboka na kufubaa yaani mng'ao unapotea.sasa swali langu je ivi vitanda vina ubora gani? na kama hamtojali tupia picha yenye kitanda kizuri na sofa, wengine tunataka tuanze maisha na vitu vyenye ubora sio kila siku unanunua kitu kile kile.
Hakuna kitanda hapo ,ndani ya miezi 4 tu utatamani kutupa ...mbao fake ,vitambaa fake ,vijigodoro fake ,...
 
Vitanda vya kipumbavu kuliko upumbavu wenyewe. Usikubali kununua kitu cha mbongo kilichofunikwafunikwa na kufichwa material.
Kwanza hivyo vitanda havivutii kama mnavyodai, pia ni kitanda andazi yani kinalegea mara sofa kipande kibanduke mara misumali ilegee na kuchomoka. Kitanda hakitaki kuhamishwa hovyo, kisimwagiwe maji bahati mbaya. Mbao za kijinga kama njiti, godoro la ulimi yale meupe kabisa yanafungwa kwenye guta mpaka juu.

Hata kitanda cha chuma sio kizuri. Kitanda ni mbao halisi kijana
 
Hivyo vitanda jau, wanaunganisha tu papi kadhaa tena zile super cyprus kisha wanashonea hayo manguo

Ni bora hata ununue kitanda cha kawaida tu cha mbao cha laki 350 mpaka 500 kitakuwa imara

Ila hivyo ni vizuri kwa ajili ya kudozi tu, ila kama unaamsha popo na kucheza gwaride hakifai hata
 
Mimi acha watu waniite old school.
Upande wa kitanda kwangu mbao is the best
 
achana nacho kama ni cha kibongo kanunue kile chenye spring unaweza kulala bila godoro na godoro nalo lina spring
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom