Hivi viongozi waliofukuzwa chuo Bugando wanalala kweli?

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
Kwa sauti ya magufuli pale UDSM alisema mwanafunzi atakaye leta mgomo chuoni ajue hataendelea na shule.... shule ita isha siku hiyo hiyo....

Roma wametekeleza.... pale bugando.... muda mwingine Rais akisema neno huwa ni sheria...
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,574
2,000
hakuna ada elekezi toka TCU... kama kuna hiyo document tafadhari share ya ada elekezi... shukrani
Kwenye suala la ada ,kabla mfumo wa serikali kubadilika kutoka kwenye utaratibu wa wanafunzi kupangiwa na serikali kwenda Vyuoni kupitia TCU kwenda utaratibu wa kuomba wenyewe chuoni, TCU ilitoa ada elekezi ambayo kwa mwaka mara ya mwisho ada elekezi ya Bugando inaonesha kuwa ni shilingi 3,700,000/= lakini chuo kimekuwa kikitoza kati ya shilingi 4,150,000/= hadi 4,300,000/= . Kwa ujumla chuo kimejiongezea pesa taslimu shilingi 600,000 ambayo ni karibia na nusu ya ada ya chuo cha muhimbili.

Hiyo ni quote ya member aliyeleta habari hizi humu, ebu fuatilia mkasa zaidi uone ulivyo
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
Hiyo ni quote ya member aliyeleta habari hizi humu, ebu fuatilia mkasa zaidi uone ulivyo
hakuna ada elekezi... kama kuna ada elekezi aje na documents... maana watu wamelalamika sana kuhusu hili lakini hakuna mpyaa
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
Ada elekezi sasa kupangwa vyuoni

SERIKALI imeanza kufanya utafiti wa kina kwa kushirikisha wadau mbalimbali ili kuweza kupanga ada elekezi kwa programu zote zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini.

Jenister Mhagama - Naibu Waziri, Elimu na Ufundi Imesema mwongozo wa ada elekezi ulizinduliwa rasmi Machi 13, mwaka huu, na kwamba ada mpya zitaanza kutumika baada ya utaratibu wa mfumo huo mpya kukamilika.


Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama, alipokuwa akijibu swali la Ismail Rage (Tabora Mjini-CCM), aliyetaka kujua gharama za ada za masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vikuu vingine nchini.


Jenister alisema kwa sasa Tanzania inavyo jumla ya Vyuo Vikuu 53 na taasisi 21 zinazotoa shahada.


Alisema sera ya elimu ya juu ya mwaka 1999 kifungu cha 6.4.3 kinaruhusu taasisi za elimu ya juu kupanga na kusimamia vyanzo vya mapato, ikiwa ni pamoja na kutoza ada za masomo.


Naibu Waziri alisema gharama za ada ya masomo katika vyuo vikuu hutegemea chuo na programu ambayo mwanafunzi anasomea.


Akitoa mfano wa ada za kozi, Jenister alisema katika programu za uhandisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatoza sh. milioni 1.3 kwa mwaka wakati Chuo Kikuu cha Dodoma kinatoza sh. milioni 1.5.


Alisema katika programu za sayansi na elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatoza sh. milioni 1.3 wakati Chuo Kikuu cha Dodoma kinatoza sh. milioni 1.2.


Aidha, alisema katika programu za elimu kwa masomo ya sayansi ya jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kinatoza ada ya sh. milioni moja wakati Chuo Kikuu cha Dodoma kinatoza sh. 800,000.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,574
2,000
hakuna ada elekezi... kama kuna ada elekezi aje na documents... maana watu wamelalamika sana kuhusu hili lakini hakuna mpyaa
Nalifuatilia maana TCU ndio inayocontrol ubora wa vyuo mbali mbali humu nchini kama tulivyoona baadhi ya vyuo huwavinafungiwa, suala la Ada sidhani kama linaweza kuachwa kila Chuo kijipangie kwa matakwa yake, lazima pawepo na namna ya kuendesha hili jambo
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
ada elekezi zilitoka kwa ajiri ya udaili au kufanyia maombi ya wanachuo kwa chuo anacho taka mtu kusoma... kuwa elfu 20, 40, 50, 100 nk
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,574
2,000
ada elekezi zilitoka kwa ajiri ya udaili au kufanyia maombi ya wanachuo kwa chuo anacho taka mtu kusoma... kuwa elfu 20, 40, 50, 100 nk
Kwa hiyo ina maana wakiweka kiwango cha chini wakati wa kudahili lakini ukianza kusoma wanakugeuziwa wanakulipisha kiasi kikubwa, unadhani hiyo ni haki?

Kwa nini wadanganye wakati wa udahili?.

Endapo wangekuwa wa kweli tangu mwanzo wa udahili juu ya Ada zao, haya mambo ya kuhoji yangetokea?

Nani mwenye kosa juu ya hili?

Ebu fikiria ingekuwa wewe ungesemaje?

Japo limeanza kulalamikiwa kwa muda mrefu sasa limezidi linahitaji ufumbuzi wa mamlaka za juu ikiwemo serikali, kumbuka hizi ni taasisi za mashirika binafsi na zimesajiliwa na serikali.
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
Nalifuatilia maana TCU ndio inayocontrol ubora wa vyuo mbali mbali humu nchini kama tulivyoona baadhi ya vyuo huwavinafungiwa, suala la Ada sidhani kama linaweza kuachwa kila Chuo kijipangie kwa matakwa yake, lazima pawepo na namna ya kuendesha hili jambo
act ya kuanzishwa kwa TCU ina semaje...? kwanini walipinga kipindi ambacho TCU walipewa majukumu ambayo hawakuwa nayo kisheria...

na hapo una ona kuwa sherria ina toa mwanya kwa taasisi husika kujipangia zenyewe ada... ndio maana ukienda pale NIT ada mpaka milioni 12 kwa mwaka na kuna kozi ya hiyo ada una soma kwa miaka minne au mitano...

au hivi vyuo vina enda kwa nacte...? na nacte ana semaje...? kuangalia ubora wa chuo haimaanishi ni pamoja na ada... ndio maana walishindwa kwa ada za sekondari

ni mamlak ambayo hawana kisheria...
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
TCU YATOA BEI ELEKEZI ADA YA UDAHILI VYUO VIKUU
Na Mwandishi wetu – Dar es Salaam


WAKATI wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu wakijiandaa kujiunga elimu ya juu, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), imetoa ada elekezi ya udahili kwa vyuo vyote vya elimu ya juu kuanzia mwaka wa masomo 2017/18 ambayo itakuwa Sh 10,000.

Kabla ya kutolewa ada elekezi hiyo, wanafunzi walikuwa wanaomba kujiunga na vyuo kupitia mfumo wa TCU walikuwa wanalipa ada ya Sh 50,000 kila mmoja kuomba nafasi katika vyuo vitano.

Pia kabla ya TCU kuanza kutumia mfumo huo, kila chuo kilikuwa na ada yake ya udahili ambayo ilikuwa ni kati ya Sh 30,000 mpaka Sh 50,000, hivyo mwanafunzi aliyekuwa akiomba nafasi kwenye vyuo vitano ilibidi alipe hadi Sh 250,000.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 12 ya vyuo vikuu, Mkuu wa Idara ya Ithibati TCU, Valerie Damian, alisema hakuna chuo kitakachotoza ada ya udahili zaidi ya kiwango kilichowekwa sasa.

“Tumeamua vyuo kudahili wanafunzi baada ya hapo majina yaliyodahiliwa yatapelekwa TCU, hivyo hapatakuwa na wanafunzi wasio na sifa na ukaguzi utakuwa mara kwa mara,” alisema Valerie.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Profesa Jacob Mtabaji, alisema vyuo vinapaswa kudahili wanafunzi kwa kuzingatia ada iliyotangazwa na tume hiyo.

“Naomba niwasihi viongozi wa taasisi mbalimbali za elimu zilizopo kwenye maonyesho haya, wazingatie maagizo ya tume na ada ya udahili isizidi Sh 10,000 … chuo kitakachokaidi maagizo sheria itachukua mkondo wake,” alisema.

Alisema TCU imeandaa mwongozo utakaowasaidia wanafunzi kujua ni programu zipi zimepewa uhalali wa kufundishwa kwenye kila chuo.

Profesa Mtabaji alisema mwongozo huo utawasaidia wanafunzi kujua kikomo cha kuomba udahili na kujiridhisha kama ataweza kumudu gharama za chuo alichoomba.

Alisema kila chuo kitengeneze mfumo ambao utakuwa rahisi kwa mwombaji kupata taarifa ya chuo husika ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo wa mtandao.

MAJALIWA APIGILIA MSUMARI VYUO VILIVYOFUNGIWA

Wakati huohuo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Simon Masanjila, wamevitaka vyuo vikuu vilivyozuiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2017/18, viache kutafuta njia za mkato na badala yake virekebishe kasoro zilizojitokeza.

Wametoa kauli hiyo ikiwa ni siku tatu tangu TCU ivifungie vyuo 19 kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18, huku ikifungia fani 75 kutoka vyuo 22 vikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu Mzumbe.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Majaliwa alivitaka vyuo hivyo kuhakikisha vinamaliza kasoro hizo na kuomba kuhakikiwa badala ya kulalamika katika vyombo vya habari.

“Mabadiliko haya yanalenga kuhakikisha tunaendana na matakwa ya dhati ya taaluma ili kujiingiza katika ushindani.

“Hivyo kila mmoja apokee na ajikite katika marekebisho ya mabadiliko hayo na kuacha kulumbana katika vyombo vya habari na makongamano,” alisema Majaliwa.

Naye Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Simon Masanjila, alivitaka vyuo vyote vilivyozuiwa kufanya udahili kuondoa kasoro zilizopo na kuomba kukaguliwa tena ili viruhusiwe kuendelea na udahili.

“Vyuo hivyo ni bora vikaondoa kasoro zilizobainika, maana vingine vimeanza kutafuta njia za mkato.

“Hata mimi nimepokea simu, ni vema vikamilishe taratibu vipeleke majibu TCU viombe kukaguliwa,” alisema.

Elimu ya kujiajiri

Katika hatua nyingine, Majaliwa aliagiza TCU na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha vyuo vinatoa wahitimu wenye uwezo wa kujiajiri na kumudu ushindani katika soko la ajira.

Alisema kwa sababu hiyo vinapaswa kuangalia mitaala ya vyuo inayotumika kama inaendana na mabadiliko yanayotakiwa.

Alivitaka vyuo kuongeza mikakati ya udahili na a kozi zinazohusu masuala ya gesi na mafuta ili kupata wataalamu watakaotumika katika sekta hiyo ambayo awali haikuwa na wataalamu.

“Wanafunzi watumie maonyesho haya kujifunza sifa na ubora wa vyuo mbalimbali kujua kozi wanazopenda,” alisema Majaliwa.

Alisema vijana wapya wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka ni kati ya 650, 000 hadi 750,000 hivyo lazima elimu inayotolewa iwawezeshe kujiajiri.

Waziri Mkuu alisema bado kuna matatizo katika mfumo wa elimu nchini yanayotakiwa kurekebishwa kutokana na upungufu uliopo katika mfumo wa elimu.

Naye Mkuu wa Chuo cha Aga Khan cha Dar es Salaam, Profesa Joe Lugalla, aliiomba Serikali kuondoa baadhi ya vikwazo vinavyovikabili vyuo binafsi ikiwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa vibali vya kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi.

Prosefa Lugolla alisema katika wakati huu wa kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima vyuo vyote viwe na uwezo wa kutoa wataalamu wenye ujuzi wenye kuendana na matakwa ya maendeleo.

“Ndiyo maana sisi tumeamua kuwekeza katika masuala ya afya na elimu kwa sababu hakuna nchi inaweza kuendelea kama watu wake hawana afya njema ,wala kwa kuwa na watu wajinga.

“Lazima iwe elimu yenye kuleta mabadiliko na inayowezesha wananchi kutatua changamoto na matatizo yao,” alisema Profesa Lugalla.

*Habari hii imeandaliwa na LEONARD MANG’OHA, MWANAIDI MZIRAY(TSJ) na ABDALLAH NG’ANZI (Tudarco)
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,977
2,000
Kwa hiyo ina maana wakiweka kiwango cha chini wakati wa kudahili lakini ukianza kusoma wanakugeuziwa wanakulipisha kiasi kikubwa, unadhani hiyo ni haki?

Kwa nini wadanganye wakati wa udahili?.

Endapo wangekuwa wa kweli tangu mwanzo wa udahili juu ya Ada zao, haya mambo ya kuhoji yangetokea?

Nani mwenye kosa juu ya hili?

Ebu fikiria ingekuwa wewe ungesemaje?

Japo limeanza kulalamikiwa kwa muda mrefu sasa limezidi linahitaji ufumbuzi wa mamlaka za juu ikiwemo serikali, kumbuka hizi ni taasisi za mashirika binafsi na zimesajiliwa na serikali.
Profesa Mtabaji alisema mwongozo huo utawasaidia wanafunzi kujua kikomo cha kuomba udahili na kujiridhisha kama ataweza kumudu gharama za chuo alichoomba.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,574
2,000
Profesa Mtabaji alisema mwongozo huo utawasaidia wanafunzi kujua kikomo cha kuomba udahili na kujiridhisha kama ataweza kumudu gharama za chuo alichoomba.
Alichokosea kwenye huo ufafanuzi, haueleza/hakujua kama ukianza chuo ndio unageuziwa na kulipa Ada yao ambayo hawakuitangaza wakati wa udahili.

Hilo jambo ndio linalowagharimu watu kwa sasa.

Pia suala la Bima(NHIF) kwa mwanafunzi ni Tsh 50400/= lakini waalipishwa 200000/= hili nalo kila chuo kinajipangia? Ninachojua bima ya matibabu kwa wanafunzi gharama yake ni sawa.
 

VietCong

Senior Member
May 9, 2018
133
250
Unalate harakati chuo cha warumi, hawatakagi kusikia. Pale Saut hostel ya Mikumi B tulikua tunapata maji Mara 1 kwa wiki ila jaribu kuongea dadeeq.. Kiufupi pale ni kama tulikua tunaishi South Sudan vijijini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom