Hivi vijana wamekataa kujiajiri?

Oct 7, 2019
51
150
Binafsi naelewa hakuna Serikali yoyote duniani ambayo haitaki kuajiri vijana wake Kama fursa zipo. Kwa Tanzania ya Sasa budget zake toka 2016 asilimia nyingi ya fedha zinapelekwa kwenye miradi ya Maendeleo. Ndio maana tunaona miradi mingi mikubwa ikitelelezeka nchini. Tunachopaswa kukifanya Sasa ni Viongozi wetu kufikiria vyanzo vingine vya mapato ili kuijengea Serikali uwezo na Fursa ya kuajiri. Sipendi Sana kusikiliza Viongozi wanaosema vijana wajiajiri maana najua Kama fursa ya KUJIAJIRI ipo na mtaji wa KUJIAJIRI upo hakuna kijana atakayeweza kukataa kufanya hivyo.

Niliwahi kusema:
Kiongozi anayepokea Mshahara kila Mwezi, Posho kila Siku, anawekewa mafuta ya gari, analipiwa malazi na marupurupu mengine. Akishakula akashiba anapanda jukwaani anamwambia kijana wa mlalahoi, aliyeifilisi familia yake ili apate ada ya kusoma, hana hata cent mfukoni baba yake na mama yake wanakomaa na wadogo zake ambao bado wapo shule KAJIAJIRI hili kwa Kifupi ni Tusi.

Mtaala wetu unahitaji marekebisho makubwa sana cha kushangaza hakuna kiongozi anayejali. Vyuo vingi vya Ufundi tumevifanya kuwa vyuo vikuu. Kwenye Soko la ajira wanaoteseka zaidi ni wahitimu wa vyuo vikuu.

Tunatoa mabilioni ya Shilingi kama mikopo ya vyuo vikuu kwa vijana ambao hatuna uwezo wa kuwaajiri. Huu ni upotevu wa fedha.... Yaani ni fedha tunachimbia chini.

Tukiendelea kudharau masomo ya Ufundi, fani mbalimbali, Kilimo na Ufugaji tutakuja kupigana Siku za Usoni. Mtaala wetu utambue fursa zilizopo nchini.... Tunapoteza muda mwingi sana kujifunza mambo yasiyokuwa na msaada kwenye maisha yetu.

Hawa viongozi wanataka watu wajiajiri watuambie watoto wao wamejiajiri wapi ili wakajifunze wengine. Huo mtaji wa kujiajiri wameupatia wapi ili nao wakajiandikishe kuchukua...

Shule zetu hazifundishi Kilimo wala Ufugaji, wanafundisha matundu ya Panzi na ukuaji wa chura. Shule zetu hazifundishi Uvuvi zinafundisha mkoloni alituuzaje utumwani, shule zetu hazifundishi Ufundi (Uchomeleaji, uchoraji, Ususi, Upishi, Ujenzi nk.) Zenyewe zimokomaa kuelezea Mzungu alivyotupora ardhi yenye Rutuba.

Kuwa na watu wengi nchini bila ajira au watu wasioweza kujikimu ni Tatizo kubwa. Vijana wanajenga chuki na viongozi wao sana kutokana na tatizo hili.

Miaka Saba msingi, Miaka Sita Sekondari, miaka Mitatu chuo kikuu jumla miaka 16 huko kote hukufundishwa kujiajiri unamaliza chuo wanataka mtende miujiza kwa kujiajiri. Tuache kutaniana na hawa vijana viongozi wanapaswa kuwaomba msamaha.

NIMEWAZA KIPUUZI ILA IDEA YANGU HII INAWEZA KUBORESHWA
Hivi tuna waalimu wangapi waliohitimu shahada ya kwanza, Stashahada na Astashahada? Hawa ni wengi Sana ni karibia Nusu ya wahitimu wote waliopo huko mtaani ambao wanatafuta ajira na bahasha kila siku.

Nikawaza hatuwezi kuishi kijamaa na kugawana hiki kidogo tulichonacho kuwapunguzia msononeko Hawa vijana? Unajua nimewazaje; twende sawa lengo letu Ni kugawana hiki kidogo kwa sisi ambao tulibahatisha kukutana na ajira pindi tulipohitimu.

Chukua kikokotoleo:
Kwa kutumia Data za mwaka 2018 toka katika jarida la Trading economics world Bank ilisema Tanzania ina idadi ya waalimu wa shule za msingi 199,705 huku wa Sekondari wakiwa 102,982 Jumla ya waalimu wote Sekondari na Msingi watakuwa 302,687.

Waalimu Hawa Kama kila mmoja atalipia leseni Kama fani nyingine za udaktari, wahandisi, manesi nk wanavyolipa waalimu Hawa wakalipa ada ya shilingi elfu kumi (10,000) tu kwa mwaka tunaweza kukusanya shilingi bilion tatu, milioni Ishirini na sita , Laki nane na Sabini elfu kwa mwaka (3,026,870,000). Mataifa Mengine waalimu wana Leseni na wanazilipia.

Kutokana na data za hivi Sasa inaonekana kuwa kwa Tanzania Kuna wanafunzi wa shule za msingi 11,051,537 milioni Kumi na Moja hamsini na Moja elfu Mia tano na thelathini na Saba. Pamoja na nia nzuri ya Serikali katika kutoa Elimu bure tukiamua kuboresha Elimu yetu zaidi kwa kuendeleza pale ambapo Serikali ilipofikia wanafunzi Hawa wa msingi tu wakiamua kulipa ada ya shilingi elfu kumi tu (10,000) kwa mwaka tunaweza kukusanya shilingi Bilioni Mia moja na kumi, Milioni Mia tano kumi na tano, laki tatu na Sabini elfu (110,515,370,000). Hapa ni Kama tutasema tu kuwa kila mwanafunzi alipe elfu kumi Kama ada na nchi nyingi hazitoi Moja kwa Moja Elimu bure kinakuwa na kuchangia gharama hapa watoe tu elfu kumi tutapata hizo Bilioni.

Wanafunzi wa Sekondari kwa kutumia Data za 2018 toka kwenye jarida Hilo Hilo la Trading economics World bank iliripoti kuwa Tanzania Kuna wanafunzi 2,140,442 milioni mbili laki moja na arobaini elfu Mia nne na arobaini na mbili. Hawa Kama watalipa ada ya shilingi elfu kumi tu (10,000) kwa mwaka tunaweza kukusanya shilingi 21,404,420,000 ambazo ni bilioni Ishirini na Moja milioni Mia nne na nne, laki nne na ishirini elfu.

Jumla ya fedha zote kwa mwaka tutakuwa tumekusanya 134,946,660,000 (Bilioni Mia moja thelathini na nne, milioni Mia tisa arobaini na sita, laki sita na sitini elfu.

Tuzifanyie Nini hizi fedha? Nikasema tuangalie upungufu wa waalimu upo wapi nikasema kwa mfano tukihitaji kuajiri waalimu wa shahada ya kwanza kwa kutumia kiasi hicho Cha fedha tunaweza kuajiri waalimu zaidi ya elfu kumi na sita kwa mkupuo na tukawa na uhakika wa mishahara yao ya mwaka Mzima bila kugusa chanzo kingine chochote Cha mapato.

Hii ni fursa Moja na tumegusa tu wanufaika wa sector ya Elimu. Bado sijafikiria maeneo Mengine hii ni Elfu kumi tu kwa mwaka ya haya makundi. Ukigusa vijana elfu kumi na sita umegusa karibia kila familia nchini, umegusa mapato ya PAYE ya Serikali mamilioni, umeongeza purchasing power kubwa Sana huko mtaani, utakuwa umefungua na fursa kwa watu wengine ambao Wana vinasaba na Hawa watu elfu kumi na sita.

Nadhani badala ya Waziri kupaka makeup na kuenjoy tu kiyoyozi Cha V8 miaka nenda miaka Rudi no impact waje na mawazo yanayoumiza tujadili kwa pamoja tunaweza kupata hapo kitu.
 
October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,694
2,000
Andiko zuri, ila uyo kijana wa mtaani anahitaji immediately solution pesa ya kujikimu inampiga chenga ukimuonesha mpango mkakati huo ataona bule.

Ulianza vizuri kule juu kuelekea kuokoa vijana leoleo chini umeshusha namba nyingi ambazo mpaka kutekelezeka vikao kadhaa, natamko kadhaa, bajeti kadhaa zipite kijana kashakufa njaa.
 
Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
3,227
2,000
Hili wazo mpelekee jiwe,

Ndio ambaye kashikilia mpini

Hakuna wa kumpinga akiamua

Akilikubali hili wazo, basi vijana watafaidi
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
8,411
2,000
Hivi nchi hii ilivyo tajiri mnashindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato na sio kukata watumishi mishahara Yao midogo.

Unapendekeza walimu wakatwe hela zao wakati Ni mwaka wa tano huu watu hawajapandishiwa mshahara hata shilingi 100 na mfumuko wa bei unaendelea kukua.

Tatizo la hii nchi ni kukosa planners wazuri kama mleta mada... Akili ni zile zile zinawaza kuongeza Kodi kwa watumishi na makato kwenye mishahara ya watumishi.
 
Stamina

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
964
500
Binafsi naelewa hakuna Serikali yoyote duniani ambayo haitaki kuajiri vijana wake Kama fursa zipo. Kwa Tanzania ya Sasa budget zake toka 2016 asilimia nyingi ya fedha zinapelekwa kwenye miradi ya Maendeleo. Ndio maana tunaona miradi mingi mikubwa ikitelelezeka nchini. Tunachopaswa kukifanya Sasa ni Viongozi wetu kufikiria vyanzo vingine vya mapato ili kuijengea Serikali uwezo na Fursa ya kuajiri. Sipendi Sana kusikiliza Viongozi wanaosema vijana wajiajiri maana najua Kama fursa ya KUJIAJIRI ipo na mtaji wa KUJIAJIRI upo hakuna kijana atakayeweza kukataa kufanya hivyo.

Niliwahi kusema:
Kiongozi anayepokea Mshahara kila Mwezi, Posho kila Siku, anawekewa mafuta ya gari, analipiwa malazi na marupurupu mengine. Akishakula akashiba anapanda jukwaani anamwambia kijana wa mlalahoi, aliyeifilisi familia yake ili apate ada ya kusoma, hana hata cent mfukoni baba yake na mama yake wanakomaa na wadogo zake ambao bado wapo shule KAJIAJIRI hili kwa Kifupi ni Tusi.

Mtaala wetu unahitaji marekebisho makubwa sana cha kushangaza hakuna kiongozi anayejali. Vyuo vingi vya Ufundi tumevifanya kuwa vyuo vikuu. Kwenye Soko la ajira wanaoteseka zaidi ni wahitimu wa vyuo vikuu.

Tunatoa mabilioni ya Shilingi kama mikopo ya vyuo vikuu kwa vijana ambao hatuna uwezo wa kuwaajiri. Huu ni upotevu wa fedha.... Yaani ni fedha tunachimbia chini.

Tukiendelea kudharau masomo ya Ufundi, fani mbalimbali, Kilimo na Ufugaji tutakuja kupigana Siku za Usoni. Mtaala wetu utambue fursa zilizopo nchini.... Tunapoteza muda mwingi sana kujifunza mambo yasiyokuwa na msaada kwenye maisha yetu.

Hawa viongozi wanataka watu wajiajiri watuambie watoto wao wamejiajiri wapi ili wakajifunze wengine. Huo mtaji wa kujiajiri wameupatia wapi ili nao wakajiandikishe kuchukua...

Shule zetu hazifundishi Kilimo wala Ufugaji, wanafundisha matundu ya Panzi na ukuaji wa chura. Shule zetu hazifundishi Uvuvi zinafundisha mkoloni alituuzaje utumwani, shule zetu hazifundishi Ufundi (Uchomeleaji, uchoraji, Ususi, Upishi, Ujenzi nk.) Zenyewe zimokomaa kuelezea Mzungu alivyotupora ardhi yenye Rutuba.

Kuwa na watu wengi nchini bila ajira au watu wasioweza kujikimu ni Tatizo kubwa. Vijana wanajenga chuki na viongozi wao sana kutokana na tatizo hili.

Miaka Saba msingi, Miaka Sita Sekondari, miaka Mitatu chuo kikuu jumla miaka 16 huko kote hukufundishwa kujiajiri unamaliza chuo wanataka mtende miujiza kwa kujiajiri. Tuache kutaniana na hawa vijana viongozi wanapaswa kuwaomba msamaha.

NIMEWAZA KIPUUZI ILA IDEA YANGU HII INAWEZA KUBORESHWA
Hivi tuna waalimu wangapi waliohitimu shahada ya kwanza, Stashahada na Astashahada? Hawa ni wengi Sana ni karibia Nusu ya wahitimu wote waliopo huko mtaani ambao wanatafuta ajira na bahasha kila siku.

Nikawaza hatuwezi kuishi kijamaa na kugawana hiki kidogo tulichonacho kuwapunguzia msononeko Hawa vijana? Unajua nimewazaje; twende sawa lengo letu Ni kugawana hiki kidogo kwa sisi ambao tulibahatisha kukutana na ajira pindi tulipohitimu.

Chukua kikokotoleo:
Kwa kutumia Data za mwaka 2018 toka katika jarida la Trading economics world Bank ilisema Tanzania ina idadi ya waalimu wa shule za msingi 199,705 huku wa Sekondari wakiwa 102,982 Jumla ya waalimu wote Sekondari na Msingi watakuwa 302,687.

Waalimu Hawa Kama kila mmoja atalipia leseni Kama fani nyingine za udaktari, wahandisi, manesi nk wanavyolipa waalimu Hawa wakalipa ada ya shilingi elfu kumi (10,000) tu kwa mwaka tunaweza kukusanya shilingi bilion tatu, milioni Ishirini na sita , Laki nane na Sabini elfu kwa mwaka (3,026,870,000). Mataifa Mengine waalimu wana Leseni na wanazilipia.

Kutokana na data za hivi Sasa inaonekana kuwa kwa Tanzania Kuna wanafunzi wa shule za msingi 11,051,537 milioni Kumi na Moja hamsini na Moja elfu Mia tano na thelathini na Saba. Pamoja na nia nzuri ya Serikali katika kutoa Elimu bure tukiamua kuboresha Elimu yetu zaidi kwa kuendeleza pale ambapo Serikali ilipofikia wanafunzi Hawa wa msingi tu wakiamua kulipa ada ya shilingi elfu kumi tu (10,000) kwa mwaka tunaweza kukusanya shilingi Bilioni Mia moja na kumi, Milioni Mia tano kumi na tano, laki tatu na Sabini elfu (110,515,370,000). Hapa ni Kama tutasema tu kuwa kila mwanafunzi alipe elfu kumi Kama ada na nchi nyingi hazitoi Moja kwa Moja Elimu bure kinakuwa na kuchangia gharama hapa watoe tu elfu kumi tutapata hizo Bilioni.

Wanafunzi wa Sekondari kwa kutumia Data za 2018 toka kwenye jarida Hilo Hilo la Trading economics World bank iliripoti kuwa Tanzania Kuna wanafunzi 2,140,442 milioni mbili laki moja na arobaini elfu Mia nne na arobaini na mbili. Hawa Kama watalipa ada ya shilingi elfu kumi tu (10,000) kwa mwaka tunaweza kukusanya shilingi 21,404,420,000 ambazo ni bilioni Ishirini na Moja milioni Mia nne na nne, laki nne na ishirini elfu.

Jumla ya fedha zote kwa mwaka tutakuwa tumekusanya 134,946,660,000 (Bilioni Mia moja thelathini na nne, milioni Mia tisa arobaini na sita, laki sita na sitini elfu.

Tuzifanyie Nini hizi fedha? Nikasema tuangalie upungufu wa waalimu upo wapi nikasema kwa mfano tukihitaji kuajiri waalimu wa shahada ya kwanza kwa kutumia kiasi hicho Cha fedha tunaweza kuajiri waalimu zaidi ya elfu kumi na sita kwa mkupuo na tukawa na uhakika wa mishahara yao ya mwaka Mzima bila kugusa chanzo kingine chochote Cha mapato.

Hii ni fursa Moja na tumegusa tu wanufaika wa sector ya Elimu. Bado sijafikiria maeneo Mengine hii ni Elfu kumi tu kwa mwaka ya haya makundi. Ukigusa vijana elfu kumi na sita umegusa karibia kila familia nchini, umegusa mapato ya PAYE ya Serikali mamilioni, umeongeza purchasing power kubwa Sana huko mtaani, utakuwa umefungua na fursa kwa watu wengine ambao Wana vinasaba na Hawa watu elfu kumi na sita.

Nadhani badala ya Waziri kupaka makeup na kuenjoy tu kiyoyozi Cha V8 miaka nenda miaka Rudi no impact waje na mawazo yanayoumiza tujadili kwa pamoja tunaweza kupata hapo kitu.
Safi sana,
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,267
2,000
Nakuunga mkono hapo kwenye uwezekano wa kubadili Mitaala yetu kwa kuwekeza zaidi kwenye Elimu inayo endana na mazingira yetu pia ya vitendo zaidi kuliko ile ya nadharia na historia! Tuwekeze kwenye teknolojia na kuvumbua vipaji mbalimbali, nk.

Haiwezekani miaka karibia 60 sasa tangu tupate Uhuru, mfumo wetu wa Elimu ufanane kwa kila kitu na ule wa wakati wa Ukoloni wa kuwaandaa wahitimu kwa kazi za kuajiriwa (White Collar Jobs) na pia kukaririshwa mavitu mengi, na yasiyo na tija wala faida yoyote ile kwenye maisha halisi mtaani.

Ifikie wakati Viongozi wetu walione hili, ili tubadilike na hivyo tuweze kuyafikia maendeleo ya kweli kama Taifa siku za usoni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom