Hivi vibwengo kweli vipo?

Hivi vibwengo kweli vipo?

Nyamuleha jr

Senior Member
Joined
Feb 20, 2013
Posts
185
Reaction score
65
Niliwahi kusikia wanafunzi huko masekondari zamani walikuwa wanaonaga wanyama flani kama binaadamu kama mashetani sasa naomba mwnye kuwafahamu au mwenye picha ya hao vibwengu aitupie eti hata wengine walipo lala walikabwa usingizi na hao vibwengu je hii ni myth au ni jambo la kweli

Tangu nipo mdogo nilikua naskia watu wanasema habari za vibwengo kua wana tabia ya kuwatokea wanadamu na kuwaletea mauza uza hasa baharini,sasa najiuliza huyo kiumbe ana umbo gani la mnyama au binadamu? au vibwengo ndio majini?

MziziMkavu et.al karibuni hapa mtoe darasa.
 
Nenda mkwakwani Tanga Tech. School shule aliyesoma Dhaifu utasikia au kuona story hehehe nakumbuka sekese la shule kuchomwa baada ya moto wa shauri Tanga kulipita kimondo angani nusura tuuane mlangoni
 
Vipo, Tuliosoma Rungwe sec. enzi za Mzee B.C Mgeni ni mashahidi...
 
Kibwengo kina kitu kama king'ora cha polisi au ambulance pale juu ya utosi...
Kasheshe huwa inakuja pale akikuuliza swali umeanza kuniona wapi wakati nakuja?

Kwa kuwa kinajijua ni kijeba "mfupi kwa kimo", basi huuliza hilo swali kama mtego...

Salama yako ni pale tu utakapojibu kuwa nimekuonea kuleee, hapo utaachiwa na kitapotea ghafla.

Lakini ukijichanganya tu ukajibu kuwa nimekuonea hapa, utakula bonge la kerebu halafu hata hutajua limetokea wapi.
 
Kibwengo kina kitu kama king'ora cha polisi au ambulance pale juu ya utosi...
Kasheshe huwa inakuja pale akikuuliza swali umeanza kuniona wapi wakati nakuja?
Kwa kuwa kinajijua ni kijeba "mfupi kwa kimo", basi huuliza hilo swali kama mtego...
Salama yako ni pale tu utakapojibu kuwa nimekuonea kuleee, hapo autaachiwa na kitapotea ghafla.
Lakini ukijichanganya tu ukajibu kuwa nimekuonea hap, utakula bonge la kerebu halafu hata hutajua limetokea wapi.

Ha haa haaa
 
ha ha ha ha hizi fiksi zimenivunja mbavu asante sana
 
Hata milambo sec wanasema vipo vingi pale ila tabora boys na umoja sec shwari tu
 
Sometime hivi vidude vinaweza kukuibukia usingizini ukashangaa umepigwa kabali mtu humuoni unabakia kuugulia tu,mara ingine unaota watu wa ajabu ajabu wanakutoa baruti na mapanga na visu halafu unakimbia huendi.mpaka ukatwe panga ndo unashtukia unaamka.bongo tunalogana sana aisee au sijui sababu ya kulakula ugali ndo unapata ndoto mbaya mbaya🙄
 
Tangu nipo mdogo nilikua naskia watu wanasema habari za vibwengo kua wana tabia ya kuwatokea wanadamu na kuwaletea mauza uza hasa baharini,sasa najiuliza huyo kiumbe ana umbo gani la mnyama au binadamu? au vibwengo ndio majini?

MziziMkavu et.al karibuni hapa mtoe darasa.
 
Last edited by a moderator:
Kibwengo + chunusi = nami naomba nijuzwe
 
Mimi najua wasichana waliokua na sura mbaya shuleni ndio tuliwaita vibwengo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom