Hivi ushawahi kukaa chini ukajiuliza hivi!

Hivi ushawahi kukaa chini ukajiuliza hivi!

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,107
Maisha ni mipango na mipango ni maisha ya kila siku!,ushawahi kujiuliza ukifanikiwa kuowa na ukapata watoto je?ungependa watoto wako waishi maisha yapi?maisha bora ama bora maisha?
Umepanga kuwa na watoto wangapi na utawasaidia vipi kutimiza ndoto zao!?
Mtoto mmoja ili aishi vizuri bila chenga anahitaji laki mbili kwa mwezi[200,000tsh]
Ambayo kwa mwaka ni sawa na 2400000tsh!
Hadi mtoto mmoja akue vizuri hadi atimize miaka 18 unahitaji milioni 43 na laki mbili!
Wanaume tutafute pesa tuache ujingaujinga
 
mkuu tutaishi kibabe maisha lazima yaendeleee ukipanga saiv hutofika tutaunga unga kisela mpka tunafika hakuna namna
 
Hayo mkuu yanapangwa huko mbele kwa wenzetu walioanza kuelimika,ila kiuhalisia lazima tuishi kiafrica zaidi hamna namna
 
Maisha ya mtoto hutegemeana na uchumi ulivyo. Mipango si matumizi.

Ila sipendi maisha niliyoishi au shule nilipopitia mwanangu apitie.
 
Ndio maana majengo yanapata Ufa na kudondoka, uchumi haukuwi, wanasiasa wanayumba yumba hawana kipawa cha kuongoza sababu ya wazazi kama ninyi.....!
Ndio nimepanga kuwa na watoto 4,moja napenda awe mwanasiasa,2 wanafizikia,na 2 wana uchumi.
Tayari nina 2 bado 2 na nina muda wa kuwa shape katika mazingirs hayo.
 
Kila mtoto anakuja.na riziki yake, zaa ujitume maisha yanakwenda....
 
Nimepanga kuwa na watoto watano
Nitapenda wanangu waishi maisha bora sana ambayo sikuwahi kuyaishi
Katika kutimiza ndoto zao nitahakikisha ninadedicate kipindi changu cha kuishi kilichobakia hapa dunia kupigania wao watimize ndoto zao watakazokuwa nazo na sio kutimiza ndoto ambazo mimi baba yao nilishindwa kuzifikia!

Naomba kuwasilisha!!
 
mtoto akisha fikisha 18 mpaka 30
ni miaka 12(nimeweka 30 kwasababu ya uhaba waajira na mtoto mpaka amalize chuo ni miaka 24.
300,000×12miez=3,600,000
3,600,000×12miaka=43,200,000

jumlishia hapo hii.

hapo uombe Mungu asiwe amezalia nyumbani.
 
Ukifanya mahesabu hayo kama hujaoa hutokaa uoe tena
 
Back
Top Bottom