Jana nilileta uzi hapa nadhani luga niliyoitumia ilikuwa ya high pitch nami naona ni toe tafsiri kwa luga nyingine ambayo pia inaweza kuwa ya juu lakini yenye kukubalika na mfumo wa ulimwengu wa walio wengi.
Ni nini basi maana halisi ya M4C na nini chanzo chake kwa tafsiri sahihi yangu mwenyewe!
Huu ni uamsho wa kukataa kuendelea kuishi maisha ya ufukara na umasikini ulitopea katika nchi yenye utajiri usiotamkika (Nukuu isiyo rasmi kutoka kwa Dr. Slaa). Uamsho una malengo ya kumfanya kila raia katika nchi ya Tanzania kutambua wajibu na sehemu yake katika kujiletea maendeleo kama ilivyokuwa kwa malengo ya kupigania uhuru wanchi. Hii inamaana fisadi yeyote bila kujali itikadi yake ya kichama ama kiroho hata pata nafasi ya kukanyaga Ikulu ya Tanzania. Hii haihitaji demokrasia na kila aliye fisadi na anadhani anaweza kufanya hivyo na athubutu basi kusonga mbele tuone kati ya hii kauli nay eye nani ni mwenye mamlaka na nguvu kubwa kumzidi mwenzake.
Nini chanzo cha huu uamsho wa M4C
Wengine watasema ni CHADEMA ni vyema na haki lakini naomba hapa nisimame mwenyewe nakuisimamia kauli yangu hii! Chanzo ni asili yenyewe ya uumbaji (ambayo mm naiita nguvu ya roho mtakatifu wewe waweza kuipa jina lako sahihi) Na kama hivyo ndivyo CHADEMA imetumika tu kama chombo sahihi ambacho kilijiweka tayari kupitishia mapenzi mema ya Mungu kwa watu wa taifa la Tanzania. Hii inamaana yakuwa hata kama kutakuwa na fisadi yeyote atakaye tokea ndani ya CHADEMA kutaka kuingia hilo jumba ufalme hataweza kwenda kinyume na amri hii halali ya Mwenye enzi mwenyewe! Nakama yupo anayebisha basi naye anaruhusa ya kusonga mbele ili adhihirishe nguvu yake kinyume na haya ninayo yasema.
Inawezekanaje haya kutokea...Sina maneno mengi ila katika tafakari yangu ili kufikisha ujumbe huu wa vipi hii nguvu ina fanya kazi basi kwa ufupi sana ni kama chembe chembe ziitwazo Solitons. Hizi zinatabia yakujikusanya japo zikiwa na nguvu ndogo lakini zinapokutana zinajiunga na kutengeneza nguvu moja kubwa inayoweza kusafiri katika hali hiyo hiyo bila kujichanganya na chembe nyingine zenye tabia isiyo fanana na zenyewe na kwa kasi ile ile hadi kubomoa miamba mikubwa....Inasemekana ndizo hasa zinazo sababisha vitu kama tsunami etc. Kwa jinsi hiyo hiyo ndivyo wazalendo wengi watanzania ambao kwa uweza wa Mungu mwenyewe wameweza kuunganishwa huku wengine wakijijua na wengine wasijue kuwa wanasaidia kupigana dhidi ya ufisadi.....(Kwa ufasaha wa jinsi solitons zinavyofanya kazi soma hapa; wale wana science
Soliton -- from Wolfram MathWorld and ;
Chaos, Solitons & Fractals - Elsevier. Kwa wale ambao luga ya science ni ngumu Wikipedia imewarahisishia nao wanaweza jisomea hapa
Soliton - Wikipedia, the free encyclopedia.
Nafasi ya Ame katika hili......
Baada ya kuzisoma hizi chembechembe darasani niliamua kufanya utafiti wangu mwenyewe na kwa imani yangu nikaamua kumlilia Mungu a lete nguvu ya solitons Tanzania nami nilipoweza kuichora ramani nzima nilimwelezea muumba mbingu na nchi nini ninataka. Ikawa jioni ikawa asubuhi hatimaye imetokea.......Naijua ramani yote ndiyo maana na uhakika na ninachokisema....Haina haja ya kuumiza watu wasio na hatia mwenye blue print ni Mungu mwenyewe na kazi ilisha malizika.......Ukombozi ni lazima anayebisha afanye atakalo!