Hivi unajua M4C ni nini?

Hivi unajua M4C ni nini?

Ltm

Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
13
Reaction score
1
Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa inahamasisha washabiki/wapenzi wake kujiunga na M4C, au Movement For Change (kwa kiingereza). Wakati mwingine wanaona kwamba jambo lao fulani limefanikiwa, basi ni kutokana na nguvu ya M4C, na kadhalika, na kadhalika......... Baada ya kuambiwa kuwa huko Uingereza (UK) kuna chama kinachoitwa Movement for Change ambacho pia kinatumia kifupisho cha M4C nikashawishika kuona kama kuna uhusiano wowote na CHADEMA.

Baada ya kusoma tovuti yao (Movement for Change | Home), sioni uhusiano wa moja kwa moja zaidi ya ku-copy jina la chama cha wazungu hao. Swali langu, je CHADEMA wameanzisha M4C yao wakiwa wanajua haya? Kama ndivyo, najua kuwa CHADEMA ina uhusiano fulani na chama cha Conservertive cha Uingereza, lakini M4C hiyo ya Waingereza ina mahusiano na chama cha Labour cha Uingereza! Hapa pana nini? Jina la jinsi hii si sawa na Athmani au Jane ambalo mtu unaweza kujiita pamoja na kujua kuwa wapo wengine wenye jina hilo. CHADEMA watufafanulie hili!
 
ikiwa ni kweli au si kweli unataka kusema nini????hebu funguka tusikie.
 
Mkuu kama wewe ni mdau wa Siasa na ni hodari wa kusoma mambo ya mabadiliko ya utawala hasa in the lines za Siasa, ni wazi kuwa the term "Movement for Change" sio ngeni. Toka huko nyuma katika mataifa na bara mbali mbali (Africa ikiwemo) walikuwa na harakati za kubadilisha mfumo wa siasa katika maeneo husika kuwa bora zaidi ya hapo ilipo kwa harakati zilizo lenga mabadiliko.

Sasa unaposema kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja, hivi kweli ilitakiwa pawe na uhusiano ndio uelewe wana CDM wana maana ipi kusema M4C? Au tu ni jitihada zako za kuonesha kuwa wamechemka kuita hizi harakati M4C? Kwa nini usiichukulie hivo hivo ilivo kuwa ni harakati za kuboresha, ongeza, kuza harakati za ufahamu wa yaendeleayo na yanayofanywa katika jamii tokana na serkali iliyopo madarakani?
 
Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa inahamasisha washabiki/wapenzi wake kujiunga na M4C, au Movement For Change (kwa kiingereza). Wakati mwingine wanaona kwamba jambo lao fulani limefanikiwa, basi ni kutokana na nguvu ya M4C, na kadhalika, na kadhalika......... Baada ya kuambiwa kuwa huko Uingereza (UK) kuna chama kinachoitwa Movement for Change ambacho pia kinatumia kifupisho cha M4C nikashawishika kuona kama kuna uhusiano wowote na CHADEMA.

Baada ya kusoma tovuti yao (Movement for Change | Home), sioni uhusiano wa moja kwa moja zaidi ya ku-copy jina la chama cha wazungu hao. Swali langu, je CHADEMA wameanzisha M4C yao wakiwa wanajua haya? Kama ndivyo, najua kuwa CHADEMA ina uhusiano fulani na chama cha Conservertive cha Uingereza, lakini M4C hiyo ya Waingereza ina mahusiano na chama cha Labour cha Uingereza! Hapa pana nini? Jina la jinsi hii si sawa na Athmani au Jane ambalo mtu unaweza kujiita pamoja na kujua kuwa wapo wengine wenye jina hilo. CHADEMA watufafanulie hili!
Movement for Change ni sentensi. ambayo inaweza kutumiwa na mtu yeyote
 
angelia nia na lengo, itakusaida zaidi ya kutafuta uhuwiano wa maneno, lengo kuu ni kuleta mapinduzi ya kisiasa, bila kujali itatumika lugha gani
 
nenda kaatamie yai lako la CCM ulilotaga maana umeliacha muda mrefu na sasa linaelekea kuharibika!
 
Huyo mwalimu wenu kweli kimeo! Kama ndio yule jamaa ameonekana kwenye media akiilalamikia michango ya M4C kweli mmeliwa. Naanza kuamini baadhi yenu mmetumwa; haiwezekani yule jamaa aongee vile halafu thread za "kukebehi" M4C zianze kufurika namna hii. Jana nilimjibu mwenzio "zomba" kama ifuatavyo. Daka hiyo, itakusaidia:

Ndio maana nakuambia use your common sense. You are a very senior JF member lakini sometimes kwa sababu unazozijua wewe unajaribu kujenga hoja za kipuuzi. Always unajaribu kuungaunga vijimambo ili kuilekeza CHADEMA kwenye udini, ukabila, au dhana yoyote mbaya! Hata kama una chuki kiasi gani wakati mwingine kuwa mkweli bro.

Well, ni kweli CHADEMA wana kitu kinaitwa "Movement for Change. Naona umejaribu kupekuapekua kwenye mitandao kutafuta ni wapi wakristo waliwahi kutumia hiyo slogan ukaibuka na "movement OF change" ya kanisa moja huko Tampa, Florida - Marekani na kuwarushia CHADEMA.

Mbona hata waisamu wana "Movement FOR Change" (link niliyokupa); lakini hiyo kwako hainogi kuihusisha na CHADEMA; of course wala hukupaswa kufanya hivyo. Mbona "Movement for Change" ziko nyingi tu duniani tena za taasisi mbali mbali iwe za kiraia, kijamii, n.k. lakini wewe umeona "Movement OF Change" ya kikristo ndio itanogesha hila zako.

Mifano ya M4Cs hii hapa:

Ya Waarabu: Arab Movement for Renewal (Ta'al)

Ya Kiislamu: MoCS | Movement for Change Sarawak

Ya wanafunzi: Movement for Change | Home

Huko Facebook: Movement for Change in Education | Facebook

n.k. n.k. n.k. ziko nyingi mno na unajua vizuri sana kuhusu hilo.

Use your common sense although common sense is not common to all.
 
Mie ninavyojua M4C ya CDM inasimama badala ya 'Millions for Commons'!
 
Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa inahamasisha washabiki/wapenzi wake kujiunga na M4C, au Movement For Change (kwa kiingereza). Wakati mwingine wanaona kwamba jambo lao fulani limefanikiwa, basi ni kutokana na nguvu ya M4C, na kadhalika, na kadhalika......... Baada ya kuambiwa kuwa huko Uingereza (UK) kuna chama kinachoitwa Movement for Change ambacho pia kinatumia kifupisho cha M4C nikashawishika kuona kama kuna uhusiano wowote na CHADEMA.....

Umetumwa?
 
Huyo mwalimu wenu kweli kimeo! Kama ndio yule jamaa ameonekana kwenye media akiilalamikia michango ya M4C kweli mmeliwa. Naanza kuamini baadhi yenu mmetumwa; haiwezekani yule jamaa aongee vile halafu thread za "kukebehi" M4C zianze kufurika namna hii. Jana nilimjibu mwenzio "zomba" kama ifuatavyo. Daka hiyo, itakusaidia:

Achana na vilaza hao watakuumiza kichwa bure.
 
angelia nia na lengo, itakusaida zaidi ya kutafuta uhuwiano wa maneno, lengo kuu ni kuleta mapinduzi ya kisiasa, bila kujali itatumika lugha gani

Muulize mtoa mada ni neno gani ambalo halijawahi kutumika popote ambalo anataka CHADEMA walitumie badala ya M4c? Hakuna neno jipya dunia hii ndugu yangu. Muulize Nape kwanini aliiga VUA GAMBA?
 
Mkuu kama wewe ni mdau wa Siasa na ni hodari wa kusoma mambo ya mabadiliko ya utawala hasa in the lines za Siasa, ni wazi kuwa the term "Movement for Change" sio ngeni. Toka huko nyuma katika mataifa na bara mbali mbali (Africa ikiwemo) walikuwa na harakati za kubadilisha mfumo wa siasa katika maeneo husika kuwa bora zaidi ya hapo ilipo kwa harakati zilizo lenga mabadiliko.....
Kwa akili za kawaida tu ambazo haziitaji kwenda kujisomea saaana neno "MOVEMENT FOR CHANGE" Linabeba maana gani? Au ni jina la chama au itikadi?

Jaribu kuwa mtu anaeweza kuchambua hata haya mambo madogo madogo acha kukalia umagamba magamba au ndio yale ya yule ndugu yenu LUSINDE?
 
CCM= CHAMA CHA MAPINDUZI ( REVOLUTIONAL PARTY) Mmeiga wapi na nyinyi?
 
Ametokea dampo gani? Mwambie arudi dampo mapema, inzi safari zao mchana.

M4C itawavuruga sana CCM.
 
Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa inahamasisha washabiki/wapenzi wake kujiunga na M4C, au Movement For Change (kwa kiingereza). Wakati mwingine wanaona kwamba jambo lao fulani limefanikiwa, basi ni kutokana na nguvu ya M4C, na kadhalika, na kadhalika......... Baada ya kuambiwa kuwa huko Uingereza (UK) kuna chama kinachoitwa Movement for Change ambacho pia kinatumia kifupisho cha M4C nikashawishika kuona kama kuna uhusiano wowote na CHADEMA.

Baada ya kusoma tovuti yao (Movement for Change | Home), sioni uhusiano wa moja kwa moja zaidi ya ku-copy jina la chama cha wazungu hao. Swali langu, je CHADEMA wameanzisha M4C yao wakiwa wanajua haya? Kama ndivyo, najua kuwa CHADEMA ina uhusiano fulani na chama cha Conservertive cha Uingereza, lakini M4C hiyo ya Waingereza ina mahusiano na chama cha Labour cha Uingereza! Hapa pana nini? Jina la jinsi hii si sawa na Athmani au Jane ambalo mtu unaweza kujiita pamoja na kujua kuwa wapo wengine wenye jina hilo. CHADEMA watufafanulie hili!

This is none issue really, instead of looking on the pixels,we should focus on the big picture
 
Back
Top Bottom