Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 31,139
- 88,800
Wakuu, poleni na mapambano. Leo nina swali au mjadala general.
Mara nyingi tunakimbizana na mishe za kila siku bila hata kuupa mwili na akili nafasi ya kupumzika, ukiachilia mbali vacation.
Vacation inaweza kuwa fupi tu, hata wikiendi moja nje ya mji, lakini matokeo yake yakawa makubwa sana.
Kuna tafiti nyingi zinaonyesha mapumziko husaidia kupunguza msongo wa mawazo na kurejesha nguvu mpya ukirudi mzigoni. Swali langu, je, wewe ukirudi kazini au kwenye shughuli zako baada ya vacation unahisi tofauti?
Kuna watu wanasema productivity huongezeka mara mbili kwa sababu akili inakuwa fresh, mwili umepumzika, na ubunifu unarudi kwa nguvu.
Wengine wanahisi ni kama hakuna mabadiliko makubwa, wanaendelea tu kama kawaida.
Huenda hii inategemea mtu, nature ya kazi yake na aina ya likizo aliyojipa (labda ni ya kupumzika kabisa au ni safari lakini yenye shughuli nyingine tena)!
Lakini pia kuna changamoto; mara nyingine ukirudi kutoka likizo, kazi ulizokimbia unazikuta so unaweza uone kama mapumziko hayakusaidii sana.
Ila kwa upande wangu na nature ya ajira yangu, nikitoka likizo mwili na akili vinakuaga vimepumzika sana. Especially nikitoka vacation ata ya week moja tu aisee uwa nakua fresh sana.
Je, kwa uzoefu wako binafsi, vacation imekuwa na faida gani kwako kwenye kuongeza au kubadilisha kiwango cha uzalishaji? Na mara ya mwisho lini ulienda vacation?