Hivi Ulaya pia kuna wanga? Mlioishi ughaibuni mpite hapa

Masangutu

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
748
540
Habari zenu wananzengo, natumai mnaendelea kupambana na mfumko wa bei?!

Nisiwachoshe sana, nataka kujua hivi Ulaya pia kuna wanga kama huku kwetu? Hawa wanaorukia mabati na kukaba watu usiku, kifupi wanga nawachukia sana.

Mlioishi ughaibuni naomba mpite hapa kutupa experience yenu juu ya vitimbi vya wanga na wachawi kama mlikutana navyo.

Imeisha hiyoo.
 
Wanga waliopo afrika waliletwa na na wakoloni wa kiarabu na kizungu.

Huko ughaibuni ndio makao makuu ya Wanga, wapo wengi mno.
 
Nasubiri..
Hata wazungu wana uchawi wao sema sio wa kimaskini kama sisi waafrika.
Wenzetu wameipa kipaumbele elimu na maarifa ndo mana ni ngumu kukuta wanashikana mashati eti mzee wattson na mkewe wanamroga mzee Floyd ili asipate kazi serikalini

Wanalima mashamba kwa teknolojia za kisasa,wanazingatia mbolea,madawa,majira nk!
Hata akikosea atafanyanutafiti atagundua dawa alizouziwa hazikua sahihi ndo mana mazao hayajastawi yamedumaa...ila sasa itokee tz hapo mzee mwaipopo kashaanza kuzipanga na mzee tuntufye anadai anamroga viazi vyake visiote,kaambiwa na mganga kumbe kauziwa mbegu mbaya

Mtu una insomnia unadai wanga wanakuchezea usilale.
Una typhoid unatapika na kuharisha,hospital wanakwambia una Uti na malaria.unatumia dawa hazisaidii unakimbilia kwa mganga nimerogwaa!

Mifano ni mingi tu.ila ushirikina umekua mkubwa africa sababu ya elimu duni na ukosefu wa maarifa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom