Hivi ujenzi wa Barabara Dar utaisha lini?

Hivi ujenzi wa Barabara Dar utaisha lini?

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Unajua imekua kama kero hivi, yaani miaka inaendaga inarudi ila kila siku Dar es salaam wapo kwenye ujenzi wa barabara. Hivi ni ujenzi wa miundo mbinu gani hii isiyoisha?

Ujue kuna maeneo Dar ukipita unaweza dhani upo mkoani?

Nauliza tu, kwamba Serikali imeshindwa kutenga hata mwaka mmoja au hata miwili mkaumaliza mkoa mzima? kipi kinashindakana? Maana tangu enzi za JPM hadi leo ujenzi bado unaendeleaga tu, na wala hata huoni wanapopajenga.

Wahusika litazameni hili, linasababisha foleni zisizo za msingi, njia nyingi zinafungwa fungwa kisa huo ujenzi mwisho wa siku inakua kero sasa.
 
Tatizo kuna watu wa mipango miji halafu wanabwia tu hela za bure.

Yaani barabara zinatengenezwa akija kiongozi mwingine anavunja..kwanini wasiwe na plan ya miaka 50 ijayo? Zikija Metro/subway watavunja tena ,yaani hatuna plan kabisa ,inabdi now tutenge njia za metro/subway so huko mbele tukipata fund ni kuendeleza tu pasipo kuvunja miundombinu iliyopo.
 
Unaisha siku ufisadi wa ccm utakapoisha, mtaa wa lindi kuelekea Shauri moyo umejengwa na wakandarasi wanazidi 20

Barabara ya Dar-Moro-Iringa-Mbeya inajengwa tangu nazaliwa hadi nazeeka n.a. haijaisha hadi leo
 
Kila sehemu wanajenga barabara. Mfano hawa wa Bagamoyo Rd ndio hapana aisee
 
Maendeleo ni kama bahari, haina mwisho, hivyo ujenzi utaendelea tu🐼
 
Hakua mwenye muda na maendeleo ya kweli. Ukiangalia Stop over kimara to Mbezi na Stop over to Ubungo utaona tofauti kubwa sana ya ujenzi wa barabara. JPM4R.
 
Back
Top Bottom