Hivi tumeshindwa kushawishi TOYOTA ilete kiwanda Tanzania?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,591
4,277
Kwa takwimu zisizo Rasmi 75% ya magari yote Tanzania ni aina ya TOYOTA. Suala lililobaki ni kuchukua takwimu kutoka TRA ndani ya miaka 10 ni magari mangapi aina ya TOYOTA yaliingia Tanzania (mapya na yaliyotumika) jumlisha na mengine yalikuwepo ambayo bado yapo barabarani + yale yaliyoagizwa kupitia TZ kwa sababu nalo ni soko.

Twende kuongea nao tukiwa na DATA na sio maneno matupu. Toyota na viwanda vingine vipo kiashara hivyo visababu vya kujibia mitihani haviwashawishi kwani vipo hata kwenye Nchi nyingine.

Tukikosa kiwanda rasmi tunaweza kupata hata centre kubwa ya spea OG za TOYOTA kwa bei poa. Tukiendelea Kulala Usingizi, hiyo fursa itaenda kwa wenzetu walio aggressive kwenye fursa.
 
Kwa takwimu zisizo Rasmi 75% ya magari yote Tanzania ni aina ya TOYOTA. Suala lililobaki ni kuchukua takwimu kutoka TRA ndani ya miaka ...
Kwa umeme huu usiotabirika? hivyo viwanda vitafungwa na kwenda kufunguliwa Kenya.

Wenzetu kabla ya kuwekeza wanafanya tafiti kujiridhisha na aina ya nchi wanayotaka kuwekeza.
 
hzo zinazoagizwa baba ni used,mpya hakuna mtanzania wa kawaida anaweza nunua.....unaweza ukaambiwa vits mpya ni mil 80 unayo?!😀🤣😂
 
Wacha tusome comments ila kwa gar izi za mwaka 2002 haitawezekana sabu gar tunazonunua ata kwenye mzunguko wa toyota ziloshatoka
 
Akili za watawala hawa wa CCM ni kuiba na kuchoma documents tu hawana creativity yoyote. Upigaji, upigaji, upigaji mpaka mwisho.
 
Toyota Vitz 2020 model ni $ 11,000 FOB. Sijui model ya 2022 ni bei gani, watanzania wangapi wana purchasing power ya kununua gari ndogo brand new kwa around 30m?
 
Toyota Vitz 2020 model ni $ 11,000 FOB. Sijui model ya 2022 ni bei gani, watanzania wangapi wana purchasing power ya kununua gari ndogo brand new kwa around 30m?
Pricing ni somo tofauti kabisa; Unatakiwa ujue ni nini kina panga bei ya bidhaa.

Mfano, unajua kwa nini marekani ikizalisha suruali ya gens bei yake inakuwa kwenye $250 hadi $450 hivi ila ikizalisha suruali hiyo hiyo nchini china bei ni $45 hadi $120 (kulingana na ubora). Ndio sababu wamehamishia viwanda vingi tu China.

Ninachomaanisha ni kuwa, hiyo Vitz ikizalishwa Tanzania bei yake inaweza kuwa nusu kwenda chini; pia ujue hayo ma gharama ya FOB hayatakuwepo labda TRA wachangamkie fursa kwa kuweka kodi ya juu
 
Kwa takwimu zisizo Rasmi 75% ya magari yote Tanzania ni aina ya TOYOTA. Suala lililobaki ni kuchukua takwimu kutoka TRA ndani ya miaka 10 ni magari mangapi aina ya TOYOTA yaliingia Tanzania (mapya na yaliyotumika) jumlisha na mengine yalikuwepo ambayo bado yapo barabarani + yale yaliyoagizwa kupitia TZ kwa sababu nalo ni soko.

Twende kuongea nao tukiwa na DATA na sio maneno matupu. Toyota na viwanda vingine vipo kiashara hivyo visababu vya kujibia mitihani haviwashawishi kwani vipo hata kwenye Nchi nyingine.

Tukikosa kiwanda rasmi tunaweza kupata hata centre kubwa ya spea OG za TOYOTA kwa bei poa. Tukiendelea Kulala Usingizi, hiyo fursa itaenda kwa wenzetu walio aggressive kwenye fursa.
Magari yapi? Sikiliza TOYOTA wateja wake inao watambua ni wale wa Magari mapya ambako kwa Africa ni.kama.nchi tatu tu South, Kenya na Nigeria,
 
Kwa gharama zile za ushuru wa forodha zilivyo juu kama mwanaukome hakika itakuwa wana -discourage watu wasinunue magari .
 
Uwezo wetu wa kununua gari jipya ni mdogo sana. magari mengi tunayoendesha ni used na Toyota haina records za Tanzania kununu Toyota. Ingekuwa magari yote tunayoendesha yangenunuliwa yakiwa mapya hicho kiwanda kingekuwa hapa siku nyingi.
 
Mleta uzi tambua hili kwanza Tanzania sio sehemu salama ya uwekezaji maana miundombinu yetu ipo local Sana hivyo kufanya uwekezaji mkubwa kuwa kitendawili kisicho na majibu.

*Nani atawekeza kwenye shida ya umeme na maji (mgao)

*Nani atawekeza kwenye nchi iliyo na mifumo ya hovyo ya Kodi (tozo)

*Nani atawekeza kwenye mifumo ya kiutawala ya rad tape

*Nani atawekeza kwenye taifa ambalo viongozi wake hawa heshima sheria na kanuni za nchi yao wenyewe

"Hakuna mwekezaji mwenye akili timamu atakuja kuwekeza kwenye taifa la mazuzu na mazwazwa"
 
Serikali ya ccm inajiona yenyewe ndiyo ina haki ya kununua na kuendesha magari mapya! Halafu wananchi wanatakiwa kununua used from Japan!
 
Back
Top Bottom