Hivi TFDA na Wizara ya Afya hazijui kwamba Fluoride ni hatari kwa afya ya binadamu?

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
7,981
4,166
Kemikali hiyo ya Fluoride ndio inayotumika kusafishia maji tunayokunywa na pia inapatikana kwenye dawa moja ya meno maarufu nchini.

Nchi zilizoendelea kama Marekani wamepiga marufuku matumizi ya kemikali hiyo kwa sababu ina athari hasa kwenye ubongo na kutoboa meno.

Fluoride Officially Classified as a Neurotoxin in World’s Most Prestigious Medical Journal - WAKING SCIENCE
Shirika la Afya duniani nalo lilitoa ripoti kuhusu hatari za afya ya kinywa inayosababishwa nafluoride. Risks to oral health and intervention

Fluoride in Your Drinking Water May Be Damaging Your Brain

Fluoride: Just when you thought it was safe to drink the water...

Fluoride inasababisha ugonjwa wa saratani kama ilivyobainishwa na taasisi ya saratani nchini Marekani Water Fluoridation and Cancer Risk
 
Aisee

Hii hatari
Watu wanakula na kunywa sumu halafu eti bado tunaamini tuna wizara ya afya! Afadhari tunaweza kuepuka kutumia dawa yenye fluoride na badala yake tukatumia colgate lakini kwenye maji ndio tatizo maana kila siku watu wanakunywa fluoride inayowekwa kwenye maji kutokea kwenye mabomba.
 
Angalau tunaotumia maji ya visima tumeepuka hilo....
 
Nandio maana magonjwa yasiyo na majina hayaishi kila kitu ni hatari. nimesikia hata [HASHTAG]#Apple[/HASHTAG] zinazotoka sauth zinasababisha kansa kwa dawa wanazoweka siziharibike zinaposafirishwa
 
Kemikali hiyo ya Fluoride ndio inayotumika kusafishia maji tunayokunywa na pia inapatikana kwenye dawa moja ya meno maarufu nchini.

Nchi zilizoendelea kama Marekani wamepiga marufuku matumizi ya kemikali hiyo kwa sababu ina athari hasa kwenye ubongo na kutoboa meno.

Fluoride Officially Classified as a Neurotoxin in World’s Most Prestigious Medical Journal - WAKING SCIENCE
Shirika la Afya duniani nalo lilitoa ripoti kuhusu hatari za afya ya kinywa inayosababishwa nafluoride. Risks to oral health and intervention

Fluoride in Your Drinking Water May Be Damaging Your Brain

Fluoride: Just when you thought it was safe to drink the water...

Fluoride inasababisha ugonjwa wa saratani kama ilivyobainishwa na taasisi ya saratani nchini Marekani Water Fluoridation and Cancer Risk

Ni swala gumu sana kwani haijathibitishwa kwa 100% isitoshe nchi nyingi sana bado zinatumia Fluoride kwenye maji ya kunywa ikiwemo USA yenyewe na nchi nyingine nyingi zilizoendelea!

Lengo la kuweka Fluoride siyo kusafisha Maji kama ulivyosema bali ni kuzuia ugonjwa wa Meno au wanaamini hivyo!

Usisahau pia kila Dawa ya meno uitumiayo ina Fluoride ndani yake, sasa tuache kupiga mswaki kutumia Dawa ya neno kama Colgate& Co.?
 
Imethibitishwa kwamba ni sumu, pitia link ya mwisho tena utafiti umefanyika Marekani. Na kuna nchi tatu ndani ya USA zinazopinga matumizi ya fluoride.

Kwanza fluoride inayotumika kusafishia maji kwa bongo huenda ikawa inazidi kipimo maana maji yananuka kuashiria yameharibika.
 
Sidhani kama umeelewa hasa kinachoongelewa, Fluoride haitumiki kusafisha Maji, bali ni Madini ambayo huongezwa kwenye Maji ya kunywa ili kupungiza Magonjwa ya Meno (Cavities) kama vile Fluoride itumikavyo kwenye Dawa ya meno kama Colgate, WHO yeyewe inashauri kiasi cha Fluoride kitumike kwenye Maji ya kunywa!

Ramani chini inaonyesha Nchi ambazo hutumia Fluoride kwenye Maji ya kunywa na kiasi kinachotumika, 100% -20%, Rangi nyekundu iliyoiva inaonyesha utumiaji mkubwa wa Fluoride yani 80-100%!
Nchi kama USA, Austarlia, Ireland., Japani, Brazili, New Zealand hawa wote ni wanatumia 60-80%, na sisi (TZ) tuko kwenye 40-60%!

940px-Fluoridated-water-extent-world.svg.png
 
Muwe mnauliza basi

Floride inafaa iwe (0.7-1.2)miligram per lita. hii inasaidia kuzuia meno kupata vitundu ( cavity) na kupata strong teeth.

sasa sijui tafiti zipote tanzania lakini america wakazi wao wana access na floride (kwenye dawa za meno like COLGATE) hivyo wakaja na pendekezo kuwa kwa kuwa wana asses na floriddated dent basi ipunguzwa kwenye maji kwa kuwa wengi wana dawa.

naona nimejieleza vya kutosha.
 
Kwa dunia ya sasa, magonjwa yanayo tokana na kemikali, iwe kwenye chakula, matunda, vivnywaji, vipodozi, nk ni vitu ambavyo aviepukiki, Cha msingi ni kuangalia kiasi Cha matumizi, na ndiyo maana kwa sasa kuna mifumuko ya kansa tofauti tofauti.
 
Acha uongo.. Kwanza sijui hata kama uliwahi kupata D ya Kemia iwapo ulipita shule.
Hakuna shirika la maji hapa nchini linalotuumia madini ya Floride kusafishia maji.
Jiji la Dar kwa mfano wanatumia Aluminium Sulphate, Sodium Carbonate na Polymer blend katika kusafishia maji safi na maji taka.
Morogoro wanatumia Calcium Hypochlorite na Aluminium Sulphate...
 
Ni swala gumu sana kwani haijathibitishwa kwa 100% isitoshe nchi nyingi sana bado zinatumia Fluoride kwenye maji ya kunywa ikiwemo USA yenyewe na nchi nyingine nyingi zilizoendelea!

Lengo la kuweka Fluoride siyo kusafisha Maji kama ulivyosema bali ni kuzuia ugonjwa wa Meno au wanaamini hivyo!

Usisahau pia kila Dawa ya meno uitumiayo ina Fluoride ndani yake, sasa tuache kupiga mswaki kutumia Dawa ya neno kama Colgate& Co.?

Sio zote zenye fluoride,
Dawa za meno za forever living ,hazina fluoride.Mie nilipojiunga na forever living ,hii ni moja ya faida ambayo niliipata.Watoto wadogo ndio wanaoathirika zaidi,maana wakipiga mswaki hupenda kumeza dawa,sasa iwapo unatumia zenye fluoride ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom