Hivi TCRA na simu feki ni faida kwa nani?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
TCRA wanasema kufikia mwezi wa sita watafunga simu feki zote hivi najiuliza hivi TCRA wanafanya kazi kwa maslahi ya nani?

yawezekana sijaeleweka lakini kimsingi mimi naona TCRA kutumiwa na makampuni makubwa yaliyo kwenye biashara za mawasiliano zaidi kuliko kulinda maslahi wa watanzania.

hivi tujiulize tanzania kuna simu ngapi hizi zinazoitwa feki na zimegarimu shilingi ngapi kuzinunua simu hizo na kuziingiza nchini.

leo hii kwa tamko la TCRA simu hizi kufikia mwezi wa sita zote zinaexpire then eti watanzania hawa watafute fedha nyingine kununua simu nyingine. michezo hii hufanywa na makampuni ya bidhaa kwa kutaka kuendelea kufanya biashara pale wanapoona bidhaa iliyokuwa sokoni wateja wamepungua na wateja bidhaa walizonazo bado zina mda mrefu huamua kuja na mbinu ya kuleta ama bidhaa mpya yenye features zaidi au kuziondoa sokoni bidhaa zilizokuwepo.

mimi naona TCRA imeingia kwenye mtego huohuo ambao tayari tunafanyiwa na makampuni ya huduma za simu kwa kila siku kuja na bidhaa mpya na kuondoa bidhaa za zamani sokoni na kwao lengo ni ili waendelee kuuza.

hivi TCRA wamepima hasara watakayowaingizia watanzania na kulinganisha na faida hizo wanazoziongea eti kuzuia wizi na nini? je haukuwezekana kuzuia hasara hiyo kwa kusema hatuna faida yoyote kuwalazimisha watanzania kutupa simu zao za zamani na kununua mpya kutoka huko nje mfano kusema tunaanza kuzuia simu feki kuingia na kila mtanzania ambaye simu yake ikiharibika ni lazima anunue mpya.

inashangaza kuona vyombo vyetu vinashawisiwa na makampuni ya biashara na kufanya maamuzi ya kuingizia wananchi hasara na kuyaingizia makampuni ya biashara faida ya ng'ambo faida.

hivi hawa wanatumia kodi ya nani ? na wapo kwa maslahi ya nani?
 
Hili nalo neno. Walikuwa wapi tangu mwanzo kuzuia hizo simu zisiingizwe nchini? Uzi huu bila shaka unaukweli fulani. Watanzania wataingia hasara ya kununua simu mpya aidha kwa uzembe au makusudi tu yaliyofanyika na yanayotaka kufanyika sasa. Wange
acha hizo simu wanazoziita ''fake'' zika ''phase out '' zenyewe.
 
Vitu vingi feki vina madhara maradufu kwa afya...
Unajua mionzi ya simu ina madhara na madhara Yale uzidi zaidi pale material yanayotumika yakiwa na kiwango duni..

So haijalishi tumechelewa au tumewahi simu feki ni sharti ziblockiwe....

Poleni
 
Mionzi ya simu ina madhara haswa kama simu ni fake? mkuu ebu tutoe tongo tongo zaidi? Mana mimi najua mionzi inategemea na Frequency ya transmitter inayozalisha Na simu za kichina transmitter zake zina less power actually hata kuradiate mionzi kwa km 2 ni shida ivo kama uko mbali na base station(Mast) ni ngumu kuwa effectively na unae wasiliana nae , Kidogo inshu ya display sio salama sana kwa macho tofauti na original device ambazo zina sense brightness na kujicontrol yenyewe kiasi cha mwangaza kutokana na hali ya hewa iliopo either giza or mwanga,
 
Moja ya faida ni usalama. Si kazi rahisi kufuatilia simu fake iliyotumika kwenye wizi, ujangili au uvunjaji wa sheria wa aina yoyote. Mhalifu hata akibadili line lakini kama ni simu ile ile atajulikana kwa kutumia IMEI.
 
WAMEAMKA. ITASAIDIA wale wenye vipato vya chini, wengi ndio wanamiliki hizo simu tena mbili mbili kucha kujaza vocha. Wataumia kidogo kwa kununua nyingine (sijui bei zitashuka). Inatakiwa TCRA wasimamie zinazoingia upande wa bei
 
Moja ya faida ni usalama. Si kazi rahisi kufuatilia simu fake iliyotumika kwenye wizi, ujangili au uvunjaji wa sheria wa aina yoyote. Mhalifu hata akibadili line lakini kama ni simu ile ile atajulikana kwa kutumia IMEI.

Umejibu jibu ambalo sikuwahi kulifikiria hapo kabla, hili nadhani ndo liwe jibu kuu kwa hilo swali.

Thank you for this useful post.
 
Moja ya faida ni usalama. Si kazi rahisi kufuatilia simu fake iliyotumika kwenye wizi, ujangili au uvunjaji wa sheria wa aina yoyote. Mhalifu hata akibadili line lakini kama ni simu ile ile atajulikana kwa kutumia IMEI.
Kwasababu hii ya usalama, naungana na wewe. Ila kuhusu madhara sijui afya. Nakataa. Maana Kuna janga linaitwa sigara. Ni hatari kuliko chochote. Watu wanalia na madawa. Lakini hawajui kuwa chanzo cha yote ni sigara
 
Me kusema simu fake siwaelewi kabisa .ila ningependa waseme IMEI fake ndo wanadeal nazo coz kweny mind y watanzania wanajua simu fake ni simu hambayo haina ubora au vimeo
 
hizi ni hadithi za abunuwasi nani anaweza kusema kiwango cha mionzi kilichoko katika hizo simu zinazozuiwa ni kiasi gani? simu zinazoruhusiwa ni mionzi ni kiasi gani? tuangalie madhara mtu anayoweza kuyapata.

wafanya biashara watumia stori kuwashawishi vitu vyao.

ki msingi mimi naweza kukubali kuwa watu waliowekeza kwenye utafiti walindwe ili swala la utafiti liwe endelevu lakini sisi nchi masikini tukijiweka kimbelembele eti kulinda tafiti tunajiingiza kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi kuliko yale tunayoyaepuka.

hili haliwezi kuamuriwa na mtu anayeona upande mmoja eti wa mionzi ambayo hii imekaa kiproganda zaidi au kuzuia wizi wa simu.

tupime kwa kila jambo na tuamue kwa interest zetu wenyewe na sio kuwasikiliza wanaokalili tu bila kuingiza kile walichokalili kwenye jamii zao na kukifanyia tathmini katika hali halisi ya maisha.

Vitu vingi feki vina madhara maradufu kwa afya...
Unajua mionzi ya simu ina madhara na madhara Yale uzidi zaidi pale material yanayotumika yakiwa na kiwango duni..

So haijalishi tumechelewa au tumewahi simu feki ni sharti ziblockiwe....

Poleni
 
unachokisema swali langu umelinganisha na hasara ambazo tunazipata kutokana na maamuzi haya?

hivi unajua simu zilizoko nchini zilizoko katika kundi hili unajua zina thamani kiasi gani?

je unajua hiyo fedha ambayo tumeleta nchini tukaziacha zikawa nyingi sasa tunawaambia watanzania tupa tukusanye fedha tukanunue nyingine hukohuko wanakotengeneza.

tukizinunua na hizo wanakuja na wimbo mwingine kumetolewa toleo lenye mionzi midogo zaidi kuliko tunazoziagiza sasa wanaibuka tena TCRA tupa hizo nunua nyingine?

majuzi tumetupa TV nyingi tu, hatujui tunaenda wapi maana yawezekana wajanja wakaja tena wakaibukia TBS unajua magari ambayo sio aoutoatic au yanayotumia CC fulani yana madhara then tunasikia tupeni.

mimi nilishawishika kusema ni muda sasa tukadai fidia kwa taasisi husika lakini hilo halitusaidii maana hiyo ni fedha yetu wenyewe hata tunayoenda kudai fidia na wajanja wao wako wanatengeneza masoko.

tunahitaji taasisi strong ya kusimamia uchumi.

tumeacha masoko yako holela mfano magari yakiongezeka sisi tunakimbia kuongeza ukubwa wa barabara, kwa nini tusijiulize hivi kwa uchumi wetu na mahitaji yetu tuko chini ya mahitaji au tumepita? na tufanye nini tuongeze barabra ndio kidogo au tubade matumizi ya magari?

mtu anakuja na hoja ya bidhaa fulani feki nani anapima impact za maamuzi yoyote tunayoyafanya ili kuhahakisha tunapata maamuzi yenye tija kwa jamii na sio kuepuka mionzi ukaongeza umasikini!

na thamani kiasi
Moja ya faida ni usalama. Si kazi rahisi kufuatilia simu fake iliyotumika kwenye wizi, ujangili au uvunjaji wa sheria wa aina yoyote. Mhalifu hata akibadili line lakini kama ni simu ile ile atajulikana kwa kutumia IMEI.
 
unachokisema swali langu umelinganisha na hasara ambazo tunazipata kutokana na maamuzi haya?

hivi unajua simu zilizoko nchini zilizoko katika kundi hili unajua zina thamani kiasi gani?

je unajua hiyo fedha ambayo tumeleta nchini tukaziacha zikawa nyingi sasa tunawaambia watanzania tupa tukusanye fedha tukanunue nyingine hukohuko wanakotengeneza.

tukizinunua na hizo wanakuja na wimbo mwingine kumetolewa toleo lenye mionzi midogo zaidi kuliko tunazoziagiza sasa wanaibuka tena TCRA tupa hizo nunua nyingine?

majuzi tumetupa TV nyingi tu, hatujui tunaenda wapi maana yawezekana wajanja wakaja tena wakaibukia TBS unajua magari ambayo sio aoutoatic au yanayotumia CC fulani yana madhara then tunasikia tupeni.

mimi nilishawishika kusema ni muda sasa tukadai fidia kwa taasisi husika lakini hilo halitusaidii maana hiyo ni fedha yetu wenyewe hata tunayoenda kudai fidia na wajanja wao wako wanatengeneza masoko.

tunahitaji taasisi strong ya kusimamia uchumi.

tumeacha masoko yako holela mfano magari yakiongezeka sisi tunakimbia kuongeza ukubwa wa barabara, kwa nini tusijiulize hivi kwa uchumi wetu na mahitaji yetu tuko chini ya mahitaji au tumepita? na tufanye nini tuongeze barabra ndio kidogo au tubade matumizi ya magari?

mtu anakuja na hoja ya bidhaa fulani feki nani anapima impact za maamuzi yoyote tunayoyafanya ili kuhahakisha tunapata maamuzi yenye tija kwa jamii na sio kuepuka mionzi ukaongeza umasikini!

na thamani kiasi
Lazima tufike mahali twende na dunia kiteknologia. Hatuwezi kubaki nyuma. Hivi simu inatumiwa miaka mingapi? Kwenye shift ya aina hiyo lazima hasara ziwepo lakini overall faida ni kubwa
 
Sijui kwa nini watanzania hamuoni impact ya haya?

ebu jiulize wewe nyumbani kwani una vitu vingapi ambavyo viko bellow standard. alafu leo hii ukiambiwa achana na hivyo vitu ununue vingine vilivyoko kwenye standard je wanakusaidia au wanakutia umasikini?

the same kwa taifa, jiulize maamuzi haya yana athari gani katika uchumi wetu.

inavyoonekana kila mwaka sasa itabidi tutafute foreign currency kubadilisha electronics products.

hivi tunauza madini yanaisha mfano mgodi mmoja nzega ulifungwa then badala ya kuwa tunanunua mashines kwa foreign currency tunazozipata eti sisi tunatumia kubadili electronics products na hiyo munaita kwenda na dunia ya sasa???????

tatizo la watanzania huwa tunapenda kusema tumekuwa nchi ya kwanza barani afrika kufanya jambo fulani hatuangalii maisha ya watu.

kwenda na ulimwengu wa sasa ni living standard ya watu ambayo inaangalia kila kitu katika maisha ya mtu.

kama ambavyo leo hii wakisema taa zote nyumbani kwako hazifai zina mionzi nunua taa mpya, friji halifai nunu la kisasa na mengine yanavyoweza kuathiri maisha yako maana budget iko palepale ndivyo maamuzi haya yanavyoathiri uchumi wa nchi.

inahitajika kubalansi kwa kuangalia faida na hasara katika nyanja zote na ndio kufanya maamuzi na kama tungekuwa tunatengeneza wenyewe yawezekana isingekuwa tatizo sana maana tunalenga kutengeza ajira za vijana wetu.

overall faida kubwa ipi maana unaangalia kwa short site kwa kufocus upande mmoja wa technolojia bila kuangalia jinsi ambavyo fedha ambazo zingetumika kwa mambo muhimu mengine tunazilazimisha kurudi kwenye huduma tuliyonayo eti kisa ni kwenda na wakati.

We deserve better than below

We deserve better than below standard products. Huo uwe mwanzo tu. Kwa nini uwe na simu fake wakati kwa hela hiyo hiyo unaweza kupata kilichobora?
Kitu kingine elewa hizo substandard na fake products mara hata kodi hazilipiwi huingizwa kwa ujanja.
Mahali fulani lazima kuanzia kuondoa fake products. There is no alternative.
 
Me kusema simu fake siwaelewi kabisa .ila ningependa waseme IMEI fake ndo wanadeal nazo coz kweny mind y watanzania wanajua simu fake ni simu hambayo haina ubora au vimeo
*#06#
Itakuja IMEI ya simu yako.. Tuma hizo namba za imei të 15090 kisha jibu likirudi angalia kama linafanana na maandishi yaliyo po kwenye simu yako unaoa battery MI Kuna kimeo nimetuma imei yake bila hata kukagua imei jibu kuwa simu yangu ni bandia so hapa NADUNDULIZA pesa za simu
 
hizi ni hadithi za abunuwasi nani anaweza kusema kiwango cha mionzi kilichoko katika hizo simu zinazozuiwa ni kiasi gani? simu zinazoruhusiwa ni mionzi ni kiasi gani? tuangalie madhara mtu anayoweza kuyapata.

wafanya biashara watumia stori kuwashawishi vitu vyao.

ki msingi mimi naweza kukubali kuwa watu waliowekeza kwenye utafiti walindwe ili swala la utafiti liwe endelevu lakini sisi nchi masikini tukijiweka kimbelembele eti kulinda tafiti tunajiingiza kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi kuliko yale tunayoyaepuka.

hili haliwezi kuamuriwa na mtu anayeona upande mmoja eti wa mionzi ambayo hii imekaa kiproganda zaidi au kuzuia wizi wa simu.

tupime kwa kila jambo na tuamue kwa interest zetu wenyewe na sio kuwasikiliza wanaokalili tu bila kuingiza kile walichokalili kwenye jamii zao na kukifanyia tathmini katika hali halisi ya maisha.
Sentensi niliyoweka nyekundu! Ni kweli kabisa i.e. Hakuna awezae kusema kiwango cha mionzi kilicho katika hizo simu. Hii ni kwasababu hazifanyiwa quality check kama zinazotengenezwa kiwandani. Watengenezaji wa simu feki hawafuati utaalamu na standard zinazoongoza viwanda vya simu. Wao wanatumia short cut ili kubana matumizi. Na hii ndio hatari kubwa! Na hii ndio inafanya zipigwe marufuku! Upo hapo? Kama unashindwa kuelewa basi linganisha na dawa zinazotengenezwa mitaani vs viwandani. Utaamini dawa iliyotengenezwa uchochoroni bila kufuata kanuni za utengenezaji? Bila shaka hapana!
 
Back
Top Bottom