Kwa sasa nchini kwetu hupati huduma Hati ya kusafiria, kusajiri kampuni au kusajili laini ya simu bila kitambulisho cha uraia.
Binafsi leo ni karibia mwaka mzima toka niandikishwe kupata kitambulisho cha uraia lakini bado sijakipata pamoja na kupiga safari zaidi ya mara saba kwenye ofisi za NIDA na jibu nililolipata kwa siku zote hizo ni SUBIRIA HAKIJAWA TAYARI.
Ilitolewa code ya kuulizia namba ya hicho kitambulisho kwa simu *152*00# kwa maana ya kwamba ukiwa na namba tu inatosha kupata huduma. Hiyo nayo wameshakula shs 10 zangu mara zaidi hata ya ishirini hamna kitu.
Niko mjini Mwanza na ofisi za NIDA ziko Mkolani, ukienda ile ofisi hadi imekuwa kero, watu wamejaa toka asubuhi mpaka wanafunga.
Kuna wakati najiuliza,hivi hivi vitambulisho waliotakiwa kuvipata bila usumbufu ni wafanyakazi wa serikalini tu? Maana wao waliandikishwa maofisini kwao na wakapewa tu haraka.
Kuna ambao hawakujiandikisha na wamekuwa wakienda ofisini NIDA penyewe,wanavipata tu ndani ya wiki lakini ukiwauliza wanakuambia hii Tanzania ukifuata utaratibu utahangaika mno,inasemekana wanatoa shs 100,000 na wanapata faster! Sasa sie ambao hatuna hiyo 100,000 maana yake ni nini?
Laini zetu za simu wa watazifunga maana muda uliotolewa ni mwezi wa 12 na kwa dalili zinazoonekana NIDA hata hawana plan B ya kuharakisha hilo zoezi maana yaonekana nako ni kamradi watu wanajipigia hela na kuongeza kipato.
pia hatuwezi kufungua kampuni maana BRELA nao wanahitaji kitambulisho cha uraia. Na pia hatuwezi kupata hati ya kusafiria kwa sababu masharti ni kuwa na kitambulisho ya uraia.
Nafikiria sana na kuwaza, hivi hizi taasisis ziko chini ya serikali tofauti? Kulikuwa na uharaka gani wa kuweka hayo masharti wakati ukweli wanaujua kuwa watanzania asilimia kubwa hawajapata hivyo vitambulisho vya uraia?
Hivi, wakuu wa wilaya na mikoa hawaoni mlundikano wa watu kwenye ofisi za NIDA na kutoa ukweli wa hivyo vitambulisho?
Kwanini NIDA wasingeachwa wamalize zoezi japo kwa asilimia 80% ya watanzania wawe na vitambulisho ndiyo masharti yawekwe?