Ukizoe sana kusoma habari za udaku.. na ukiwa mshabiki mkubwa wa post za mange kimambi.. matokeo yake huwa bayana.!!
kama hujaelewa post yangu nikusaidie kidogo..
Yamkini kukawa na ukweli kuwa Iqbal inaanza na Herufi I na hata Ahamadiya inaanza na Herufi A. ambayo mhusika alikuwa mfuasi wake...
lakini pia IA inaweza kuwa na mwanzo wa Majina ama maneno mengine yaliyo na maana iliyo jificha..
Hoja yangu ipo katika "Redio ya Taifa" TBC na kuwa habari zinazotoka katika redio hii huchukuliwa kwa makini zaidi ikiwa na maana kuwa ni chombo cha Umma sio binafsi..
Sasa kama Rais wa Nchi akihutubia Watanzania alisema mtunzi wa Jina hili aliamua kutumia herufi za mwisho kwa jina TANZANIA ili liendane na majina ya nchi nyingi zikiishia hivyo..
Kisha mtangazaji wa Redio ya Taifa akatangaza kuwa Herufi hizo zimeficha "jina" la mhusika na "ufuasi" wake katika dhehebu lake..
je kipi ni Sahihi? Kwanini muandishi hakuenda sambamba na hotuba ya Rais?
Je rais alikuwa muongo aliwadanganya Watanzania hali akijua ukweli?
au Mtangazaji anajua ukweli ila alimficha Rais?
je zipi ni athari za matangazo haya kwa Taifa letu?
Sent using
Jamii Forums mobile app