Hivi Tanzania kila jambo lazima tuzaminiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Tanzania kila jambo lazima tuzaminiwe?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by mbweta, Oct 7, 2011.

 1. m

  mbweta JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mara ya kwanza kulikuwa na tangazo la kuvunja ukimya hasa kipind cha kombe la dunia lilidhaminiwa na watu wa marekani, saiz kuna tangazo/mabango ya funga mkanda limedhaniwa na watu wa umoja wa ulaya yani sie kufunga mkanda au kuvunja ukimya mpaka mtu atuambie?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Watanzania ni washobokaji. Na wala siyo Watanzania tu. Niseme Waafika kwa ujumla wetu.

  Sasa nimepata nyepesi kuwa Obama anakuja Tanzania mwezi huu. Subiri uone jinsi tutakavyoshoboka. Tutashoboka mpaka tutatia aibu.

  Subiri uone watu watakavyomsifia mke wa Obama. Watasema sijui mzuri (ingawa binafsi sidhani kama ni mzuri hivyo manake hata taji la miss Harvard hawezi kushinda)….watasema eti anajua kuvaa….wakati anavaa kawaida tu.

  You heard it here first…mark my words.
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Acha wivu wa kike
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hujanikera bado. Jaribu tena.
   
 5. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO by Nyani Ngabu,
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Swadaaktaa!
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mimi siwezi kujumuisha "Miafrika" yote katika kapu moja, kila taifa la Afrika lina mambo yake. Lakini ninaweza kusema "Mitanzania ndivyo tulivyo kwa kufadhiliwa". Mfano mzuri ni suti za Vasco da Gama.
  Mbali ya kufadhiliwa katika bajeti yetu, bado hatuoni haya kufadhiliwa hata kuzoa taka tunazozalisha wenyewe, tena sisemi kwenye kilimo, elimu, afya, maji, barabara. Laiti tungelikuwa na haya kidogo pamoja na nadhari, tungeelekeza nguvu zetu zote katika elimu na afya. Lakini wapi!
  Ikiwa kufadhiliwa ni utumwa, hivyo ndivyo tulivyo "Mitanzania" (ashakum sio matusi).
   
Loading...